Wanaotaka kuanza kusoma CPA karibuni tushauriane

Inawezekana kusoma masomo 6 na kufanikiwa???
Yes ni nguvu na uwezo wako tu mkuu, ila kama upo kazini, au busy na issues nyingine na masomo 6 tena kidogo itakubidi uwe unalala na viatu maana si mchezo.

Ila kuna wanaoweza and you could be among them mkuu
 
Vipi lakini pepa zao?!!maana naskia balaa na nusu nataka nianze foundation next year if God wish!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli pepa ni maandalizi dear, ukijiandaa vizuri pepa inaenda ila kama unafanya zimamoto unaanza kusoma a week before pepa akii lazima upigwe na kitu kizito. Tena foundation kuna hadi multiple choices and matching items japo zinachanganya hizo huelewi it's A or B ila zinafanyika.

Nikuchekeshe, venue zao zina Ac kalii nilivoingia nilikua hadi nashake baridi , ila baada ya kuanza kufanya pepa niliskia kusweat balaa😂😂🙌

Kila rakheri anza tu na once ukishaanza basi inazidi kukuvutia hadi utajikuta upo final level
 
Wee...hukoo multiple choice Mimi ndo shiida iliko![emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]...I can image...unapatwa na joto ghafla daahh!
Mungu akusaidie sana!
Naimani utafanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee B1...Naomba nipate papers na maswali nikomae nayo.
Inanisumbua sana, mtihani wa juzi wenyewe nimevuruga

Please niforwadie pm.
 
Hongera sana, kinachotesa wengi huwa ni majukumu mengi kuanzia, familia, shule pia ukishakaa mda mrefu like 5 na 10 years ukirudi shule unakuwa little bit slow,ni vizuri watu wakiweza ukimaliza bachelor uunge hizo CPA, masters or whatever ukiwa bado akili haina mambo mengi waweza toboa kirahisi kuliko usome huku kazini, mara majukumu ya kifamilia aisee utaimba haleluya
 

Habari, nina BBA Accounting nilikua nahitaji kufanya CPA, lakini kwa muda nimekuwa nikikutana na ushauri tofauti kuwa ACCA ni nzuri zaidi ya CPA bila maelezo maalum. (Ninaomba maelezo juu ya hili)

2. Pia ninauliza kwa centre nzuri Arusha kwa ajili ya CPA ni ipi? Na kama ninaweza kupata tutor online badala ya kwenda kwenye centre?

3. Ninaomba kufahamishwa pia, ninategemea kujisajili Sasa kwa ajili ya mitihani ya mwezi wa 5, je ninaweza kupata exemption?

4. Ninaomba mtu wa Arusha ambaye anaweza kunisaidia materials ya intermediate na final tafadhali

5. Ushauri mwingine wowote kabla ya kuanza kusoma ninaomba mnipe hapa
Ahsanteni
 
Kwa mimi nnavofahamu, ACCA na CPA ni kama zinaelekeana tu, sijui tofauti iko wapi labda waliopata wanaweza toa maelezo kidogo. Japo naona kama ACCA si famous sana kama CPA 🤔.

Pia BBA Accounting ni unaanzia intermediate level 6 subjects.

Mliopo Arusha msaidieni mkuu center nzuri for review Classes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…