Mr Confidential
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,532
- 2,415
Ziko subjective based on unaanzia level ipi.Naomba unisaidie kufahamu gharama za ACCA ni bei ngapi mkuu?!!
Ngoja niandike fees applicable Under normal circumstances .
PART A: INITIAL COSTS
1. Initial Registration: £36
2. First year subscription fee: £63
note 1: ukijiregister afu ukachelewa kulipa fee, Jina lako litafutwa. Ukitaka kurudi kuregister upya fee itakua £89
note 2: subscription fee ni £122 (kila mwaka). Ila kwa mwaka wa Kwanza ndo Kuna punguzo, utalipa hiyo £ 63.
Haya tuendelee Sasa,
PART B: EXEMPTION FEES
Hizi ni ni fee unalipa kwaajili ya msamaha wa kufanya mitihani kadhaa. Assumption ni kwamba umeshaifanya ukiwa chuoni au somewhere else.
1. Applied Knowledge exams: £40 @subject.
Haya masomo yako matatu.
(a) Business and Technology
(b) Management Accounting
(c) Financial Accounting
note: kibongo-bongo tunaita FOUNDATION LEVEL
2. Applied skills exams: £58 @subject
Haya yapo sita.
(a) Corporate and Business Law
(b) Performance Management
(c) Taxation
(d) Financial Reporting
(e) Auditing and Assurance
(f) Financial Management
note: ki-kwetukwetu tunaita INTERMEDIATE LEVEL
PART C: EXAMINATION FEES
(Kwa mitihani ya Sept 2023)
1. Applied Skills exams : £ 135 per subject
Deadline ya kulipa ni 31st July 2023
Ukichelewa kulipa hadi 7th August utalipa £345 per subject
2. Ethical and professional skills module: £75
3. Strategic Professional (Essential) : Haya yapo mawili tu, na ni lazima kufanya regardless of any circumstance
*Strategic Business Leader : £ 238
*Strategic Business Reporting : £ 170
4. Strategic Professional (Options) : Haya yapo manne, unachagua mawili. £170 per subject
*Advanced Financial Management (AFM)
*Advanced Performance Management(APM)
*Advanced Taxation (ATX)
*Advanced Auditing and Assurance (AAA)
I hope nimekujibu.
#CPA-T Mr Confidential