Tofauti ya CPA na ACCA ni ipi
ACCA NI NINI?
ACCA ni Kifupi cha Association of Chartered Certified Accountants ambayo ni Bodi Kubwa (kuliko zote) ya Kimataifa ya Uhasibu Duniani ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Makao makuu ya Bodi hii yako Uingereza, Katika Jiji la Adelphi, London, Anuani yao ni hii hapa: ACCA, The Adelphi, 1-11 John Adam Street, London, WC2N 6AU, Namba ya simu: +44 (0)20 7059 5000.
Hii ndiyo Bodi Kubwa na inayokuwa kwa haraka zaidi Duniani yenye wanachama zaidi ya 208,000 na wanafunzi zaidi ya 503,000 ndani ya nchi 179 duniani kote.
KWA NINI MTU ASOME ACCA? Kwa ufupi tu ni kwamba:-
Inakuwezesha kuwa “Chartered Certified Accountant”. Kuwa Chartered maana yake ni mtu ambaye amethibitishwa na Bodi ya Watalaam kuwa ana Ujuzi na Weledi katika Fani Fulani na amepata Cheti cha Uthibitisho kutoka katika Bodi hiyo. Kwa hiyo mtu akitumia maneno ACCA baada ya herufi za jina lake, inaonyesha kwamba mtu huyo ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika sekta ya Uhasibu na Fedha pamoja na Utawala katika Biashara ya aina yoyote ile.
Inakupa matarajio makubwa ya kupata ajira nzuri mahala popote duniani kwa kuwa una uwezo wa kufanya kazi katika biashara ya aina yoy0te ile.
Inawapa uhakika waajiri kuwa una uwezo mkubwa wa Kukabidhiwa Majukumu Makubwa ya Kiutendaji (Senior Management Positions).
Mitihani inafanyika Mara NNE kwa mwaka mzima, yaani March, June, September na December kila mwaka. Hivyo unaweza kumaliza mapema ukiamua.