Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Katika operesheni za mwishonimwishoni chini ya uongozi wa Freeman Mbowe kama mwenyekiti wa chama ni hii operesheni ya No Reforms no Election.
Operesheni hii ilipitishwa na vikao vyote vikuu vya chama kuanzia kamati kuu hadi mkutano mkuu Taifa, tena chini ya uenyekiti wa Mbowe.
Kinachoshangaza umma, ni pale kundi la wanachadema waliokuwa wakimuunga mkono Mbowe katika uchaguzi uliopita, ndiyo leo wanaojitokeza na kuikana hii operesheni ya chama. Hili jambo linawaacha Watanzania na wanachadema mdomo wazi na wanajiuliza yafuatayo:
1. Mbona hili kundi halijawahi kujitokeza kumkatalia Mwenyekiti Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza No Reforms no Election, ila leo akizungumza Mwenyekiti Lissu kundi hilo halitaki operesheni hiyo ya chama?
Hili jambo tunajiuliza, inakuwaje No reforms no election ya Mbowe iwe ni sawa kwao, ila no reforms no election ya Lissu iwe haramu. Ina maana wanataka kuwaambia Watanzania kuwa Mbowe alikuwa na ndimi mbili kwa hiyo hakumaanisha alichokuwa akikisema kwa hiyo walimvumilia tu wakijua kuwa atabadili gia angani?
2. Hili Kundi litupe tafsiri ya No Reforms no election ni nini.
Kiingereza kiko wazi, No reforms, no Election maana yake ni kuwa kama hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Hebu hili kundi lije litwambie hiyo ya kwao ya "No reforms, there is election" wameipata wapi, imepitishwa na kikao gani cha chama.
3. Hili kundi lina chuki dhidi ya Uongozi wa Lissu, Limezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.
Ukiwaangalia wengi wao, ni wale waliokuwa wakiishi kwa mbeleko ya Mbowe, wameishi ktk chama na kujimilikisha chama kwa muda mrefu, wakadhani ni kijiwe cha babu, au baiskeli ya mjomba. Ni watu wanaompenda Mbowe zaidi kuliko chama na hii ni kwa sababu aliwapa kula, leo mrija umekatwa, wana hasira, wana gubu, kwa hiyo hasira zao wanazielekeza kumkwamisha Mwenyekiti halali aliyechaguliwa na wanachadema. Lakini watambue tu kuwa watanzania wanawapuuza na soon watakuwa maadui wa wananchi kwa sababu wanataka kukwamisha uongozi mpya wa chama ambao wananchi wana matumaini nao ya kuleta mabadilko.
4. Mbowe asipojitokeza na kukemea kundi la wafuasi wake kukwamisha maamuzi ya chama maana yake naye anahusika yuko nyuma yao.
Mbowe ni kiongozi wa chama bado, na yeye ni mjumbe wa kamati kuu. Kwa nafasi yake aliyohudumu kwa miaka 21 hana budi kukisaidia chama kisimamie maamuzi yake halali tena yaliyofanyika chini ya uongozi wake. Kama akikaa kimya huku wanaoleta chokochoko hizi ni watu waliokuwa wanamuunga mkono, basi hii itamaanisha kuwa Mbowe yuko katika kundi hilo, na yeye anashiriki kumhujumu mwenyekiti mpya na watanzania watamuona msaliti.
5. Pesa ya CCM inatafutiwa matumizi.
Ni nani asiyejua kuwa CCM inapenyeza mpunga ili kuharibu Chadema, nani amesahau pesa za madalali walizokuwa wanagawa kama pipi ili kupanga safu za uongozi wa Chadema. Kama CCM inawadai madalali chenji yake baada ya madalali kufeli katika uchaguzi mkuu wa chama basi madalali wakazitafute hizo pesa wazirudishe. Hii ya kujaribu kufanya final push ya kukivuruga chama ili kujustify matumizi ya pesa za kununuliwa, itafeli. Madalali wakale walipopeleka mboga.
Tena wanajiita eti G-55, jina la wabunge wa CCM. Hii inaonyesha namna gani hili kundi linavyowaza kiCCM CCM. Tumezoea wanachadema wakiitwa makamanda, hawa wanajiita G-55. Hamna kitu hapo!
6.Watanzania na Wanachadema wana Imani na Tundu Lissu na maamuzi ya vikao vya chama.
Hiki chama cha CHADEMA kina jasho la watsnzania wengi sana. Hii siyo kampuni ya biashara. Hiki ni chama cha ukombozi mpya wa Watsnzania. Anapoinuka kiongozi anayemaanisha kama Lissu, Watanzania wanaona, wanajua, na wanamuunga mkono. Lissu hafanyi kile kilicho nje ya maamuzi ya chama, anatekeleza kile kilichoamuliwa na chama. Sasa kama hawa wanaotaka uchaguzi bila reforms wanaona wanakereka na maamuzi ya kikao cha MKUTANO MKUU TAIFA wa chama ya NO REFORMS NO ELECTION basi wasubiri mkutano mkuu mwingine wa chama wajenge hoja yao ya kutaka kikao hicho kibadili mtizamo, lakini siyo kushinikiza uongozi wa sasa wa chama Usitekeleze maazimio ya Wenye chama yasni mkutano mkuu wa chama Taifa !