PreGE2025 Wanaotaka kukwamisha operation ya chama ya "No Reforms no Election" wanaharibu Legacy ya Freeman Mbowe

PreGE2025 Wanaotaka kukwamisha operation ya chama ya "No Reforms no Election" wanaharibu Legacy ya Freeman Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tuliwatahadhalisha kabla ya uchaguzi wenu kuwa Chadema bila Mbowe hakuna chama mkabisha. Leo kila Lissu akiongea No Reform, No Election HAELEWEKI anaongea nini zaidi ya kutemea maiki mate. Sasa mnarudi kwa Mbowe! Ooh! Mbowe alisema! Mbowe alisema! Mbona Mbowe huyu huyu aliongelea kuhusu maridhiano na hamyataki na hamyazingumzii?

Mbowe shikilia hapo hapo mpaka waje Hai kupiga magoti! Nyambafu!!
mpuuzi wewe. kama unaweza kumuelewa babu WASIRA utashindwa kumuyelewa lisu. wewe una matatizo yako binafsi. nenda hai kwa mbowe akakunaniliooo
 
Ndani ya chadema kuna CCM wengi sana ...tatizo ni mfumo wa chama kuchagua viongozi ni dhaifu hivyo kutoa mwanya wa mapandikizi na transformation
na ndani ya CCM na Serikali yake kuna CDM wengi!
 
Ni bora uchaguzi mkuu usifanyike hizo pesa zipelekwe kwenye mahitaji ya msingi kwa wananchi...

Kufanya uchaguzi kihunihuni ni uzwazwa na kupoteza pesa wakati tayari sisiemu wana matokeo mfukoni.
 
Umemaliza yote Mkuu, Mbowe atoke hadharani alikane hili kundi kwani linamchafua na itaonekana kuwa hata zile tuhuma za B 12 za Mama Abdul ni kweli, sasa kwa vile hazikufanikisha lengo la kumpa uenyekiti sasa ndiyo zinatumika kuvuruga Chama ili ionekane Lissu ameshindwa ili yeye arudishwe kwa mlango wa nyuma kukidhi matakwa ya Mama Abdul.
Mbowe wa nini tena?ajitokeze ili mumuite Nkurunzinza,mlamba asali?
😀😀
 
Katika operesheni za mwishonimwishoni chini ya uongozi wa Freeman Mbowe kama mwenyekiti wa chama ni hii operesheni ya No Reforms no Election.
Hapana. Hii alikuwa bado anaitafutia njia ya kui-'manage', kwa njia zile zile za kilaghai alizokuwa amejifunza toka kwa mama. Mbowe hakuwa na msukumo wa hiyo 'No Reform, No Election', bali alikuwa bado hajasuka njia ya kuififisha
Hii ilikuwa imelazimishwa kwake ndani ya cjhama.
 
Wale jamaa wamejenga hoja za msingi sana kwenye ule waraka wao. Busara ni Lisu na watu wake kuzichukua na kuona namna ya kuzifanyia kazi ila kama chadema itashupaza shingo basi Lisu atapata ugumu sana kuongoza. Ndo ajue Mbowe alikuwa akili kubwa ndo chadema akawepo muda wote huo sio yeye na majazba ya siasa
Mkuu 'Sunset', kuna hoja zipi za msingi katika mkanganyiko huo?
Wao ni bora wazuie matokeo kuliko kuzuia chanzo cha matokeo haya chafu!
Kundi hilo lipo CCM. Hawa hawana tofauti yoyote na wasaka fursa binafsi waliomo ndani ya chama cha mapinduzi.
 
Wale ndo madalali wa siasa.

Mungu fundi sana. Ameamua kuwaumbua ili Watanzania tuwajue maadui wanaozuia mabadiliko ya kweli kwa Watanzania ni kina nani.
Ukweli ni kwamba hawa wamekirahisishia chama njia za kujisafisha na kujitenga kabisa na machicha yaliyokuwa yakikivuruga chama.
Kilicho baki sasa ni kutafuta njia nzuri tu za kuyachuja haya machicha yasilete rabsha ndani ya chama.
Hili ni kundi lililo tayari kutumiwa na CCM kuivuruga CHADEMA Mpya.
 
Kinachoshangaza umma, ni pale kundi la wanachadema waliokuwa wakimuunga mkono Mbowe katika uchaguzi uliopita, ndiyo leo wanaojitokeza na kuikana hii operesheni ya chama. Hili jambo linawaacha Watanzania na wanachadema mdomo wazi na wanajiuliza yafuatayo:
Mkuu 'Missile', hujapoteza hata chembe ya umahiri wako wa kujenga hoja humu JF.
Mfano mzuri ni huu ufafanuzi ulio uweka katika maneno hayo hapo juu.

Maana yake ni kwamba Mbowe na kundi lake walipokuwa wakipoteza kura katika vikao hivyo ni kwamba tayari wajumbe wengi walishja achana kabisa na zile ngonjera za "Maridhiano", ambazo tayari zilikuwa zimemnasa Mwenyekiti na baadhi ya hao waliokuwa nyuma yake.
Maana yake ni kwamba alikuwa hana njia ya kuzuia kura hizo zitoe matokeo ya namna hiyo.
Sasa kwa "busara" anazosifiwa nazo, Mbowe, kama Samia alivyo, akaweka matumaini ya kutumia ujanja/ulaghai na kununua muda ili zipatikane njia za kufifisha matokeo ya kura hizo.
Kwa bahati mbaya kwao, huo muda na janja hazikupewa nafasi ndani ya chama kwa kuwaengua moja kwa moja toka kwenye uongozi.
Hof iliyopo sasa ni kama Mbowe na kundi lake hili wataweza kutumiwa na CCM kuendelea kuvuruga mipango ya chama hicho chini ya uongozi mpya.
 
1. Mbona hili kundi halijawahi kujitokeza kumkatalia Mwenyekiti Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza No Reforms no Election, ila leo akizungumza Mwenyekiti Lissu kundi hilo halitaki operesheni hiyo ya chama?

Hili jambo tunajiuliza, inakuwaje No reforms no election ya Mbowe iwe ni sawa kwao, ila no reforms no election ya Lissu iwe haramu. Ina maana wanataka kuwaambia Watanzania kuwa Mbowe alikuwa na ndimi mbili kwa hiyo hakumaanisha alichokuwa akikisema kwa hiyo walimvumilia tu wakijua kuwa atabadili gia angani?
Sahihi kabisa. Na ukitaka kujuwa angalia mambo ya aina hiyo yanavyo fanyika ndani ya CCM. Samia akijiteua kuwa mgombea kwa kuwastukiza wajumbe wote, kuna nani tena wa kuhoji. Wote inawalazimu kupiga makofi na kujionyesha wa furaha kuu!
Mbowe na kundi lake alikuwa anatumia 'template' ile ile inayo tumiwa na Samia huko ndani ya CCM.
Alicho kosea Mbowe, ni kuruhusu uchaguzi ufanyike. Bila shaka hadi leo atakuwa analijutia sana hilo.
 
3. Hili kundi lina chuki dhidi ya Uongozi wa Lissu, Limezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.

Ukiwaangalia wengi wao, ni wale waliokuwa wakiishi kwa mbeleko ya Mbowe, wameishi ktk chama na kujimilikisha chama kwa muda mrefu, wakadhani ni kijiwe cha babu, au baiskeli ya mjomba. Ni watu wanaompenda Mbowe zaidi kuliko chama na hii ni kwa sababu aliwapa kula, leo mrija umekatwa, wana hasira, wana gubu, kwa hiyo hasira zao wanazielekeza kumkwamisha Mwenyekiti halali aliyechaguliwa na wanachadema. Lakini watambue tu kuwa watanzania wanawapuuza na soon watakuwa maadui wa wananchi kwa sababu wanataka kukwamisha uongozi mpya wa chama ambao wananchi wana matumaini nao ya kuleta mabadilko.
Perfect. Mfumo ule ule uliopo ndani ya CCM, 'Patronage' toka kwa fadhila za Mwenyekiti, ndio huo huo uliokuwa unajengeka ndani ya CHADEMA chini ya Mbowe
 
4. Mbowe asipojitokeza na kukemea kundi la wafuasi wake kukwamisha maamuzi ya chama maana yake naye anahusika yuko nyuma yao.

Mbowe ni kiongozi wa chama bado, na yeye ni mjumbe wa kamati kuu. Kwa nafasi yake aliyohudumu kwa miaka 21 hana budi kukisaidia chama kisimamie maamuzi yake halali tena yaliyofanyika chini ya uongozi wake. Kama akikaa kimya huku wanaoleta chokochoko hizi ni watu waliokuwa wanamuunga mkono, basi hii itamaanisha kuwa Mbowe yuko katika kundi hilo, na yeye anashiriki kumhujumu mwenyekiti mpya na watanzania watamuona msaliti.
Niseme tu bila wasiwasi wowote, kwamba utasubiri sana kusikia Mbowe akilikemea kundi hili. Mbowe alijizamisha sana katika uhusiano wake na Samia kwa sababu ambazo ni vigumu kuzijuwa.
Mbowe hawezi kwa moyo safi, na dhati kabisa kuonyesha kutengana na Samia. Ni bora kukaa kimya na kufanya mambo chini chini kuliko kuonekana akifanya juhudi za kumwangusha Samia.
 
6.Watanzania na Wanachadema wana Imani na Tundu Lissu na maamuzi ya vikao vya chama.

Hiki chama cha CHADEMA kina jasho la watsnzania wengi sana. Hii siyo kampuni ya biashara. Hiki ni chama cha ukombozi mpya wa Watsnzania. Anapoinuka kiongozi anayemaanisha kama Lissu, Watanzania wanaona, wanajua, na wanamuunga mkono. Lissu hafanyi kile kilicho nje ya maamuzi ya chama, anatekeleza kile kilichoamuliwa na chama. Sasa kama hawa wanaotaka uchaguzi bila reforms wanaona wanakereka na maamuzi ya kikao cha MKUTANO MKUU TAIFA wa chama ya NO REFORMS NO ELECTION basi wasubiri mkutano mkuu mwingine wa chama wajenge hoja yao ya kutaka kikao hicho kibadili mtizamo, lakini siyo kushinikiza uongozi wa sasa wa chama Usitekeleze maazimio ya Wenye chama yasni mkutano mkuu wa chama Taifa !
Hatari kubwa ipo hapa.
Pamoja na umahiri alio nao Tundu Lissu katika kueleza maamuzi yaliyo fanyika ndani ya chama na kusimamia utekelezaji wake, CHADEMA haina budi kuhakikisha kuwa ndani ya chama hicho kunakuwepo na viongozi wa aina hiyo wengi. CCM wanapo jaribu kuhudumu chama na kumshambulia Lissu wakute amezungukwa na ukuta mzito wa vionzozi wasio tetereka katika msimamo wa chama chao.
Hawa viongozi ni lazima wawe kila mahali, hata kule kwenye Kanda, Majimboni, hadi mitaani.
Chama kisiwe cha Tundu Lissu tena, kama ilivyo kuwa cha Mbowe. Chama ni lazima kiwe cha wanachama wanaoelewa kinacho simamiwa na chama chao.
Hii ni moja ya kazi anayo takiwa kuifanya Tundu Lissu, kwa ushirikiano na viongozi wenzake wa ngazi za juu. Chama kikiwa cha wanachama, moja kwa moja kinakuwa cha wananchi wa Tanzania.
 
Mkuu 'Sunset', kuna hoja zipi za msingi katika mkanganyiko huo?
Wao ni bora wazuie matokeo kuliko kuzuia chanzo cha matokeo haya chafu!
Kundi hilo lipo CCM. Hawa hawana tofauti yoyote na wasaka fursa binafsi waliomo ndani ya chama cha mapinduzi.
Basi ni dhahili chadema haija-heal kutoka kwenye madonda ya u-team Mbowe na Lisu. Chama kina kazi kubwa ya kufanya alafu Mbowe underground ana nguvu sana na wafuasi wake wako strategic kuliko yeam Lisu. Ipo kazi ya kufanya hawa walioleta hoja si wa kubezwa lazima kuwe na mkakati wa kudeal na hiki walichoanzisha
 
Hatari kubwa ipo hapa.
Pamoja na umahiri alio nao Tundu Lissu katika kueleza maamuzi yaliyo fanyika ndani ya chama na kusimamia utekelezaji wake, CHADEMA haina budi kuhakikisha kuwa ndani ya chama hicho kunakuwepo na viongozi wa aina hiyo wengi. CCM wanapo jaribu kuhudumu chama na kumshambulia Lissu wakute amezungukwa na ukuta mzito wa vionzozi wasio tetereka katika msimamo wa chama chao.
Hawa viongozi ni lazima wawe kila mahali, hata kule kwenye Kanda, Majimboni, hadi mitaani.
Chama kisiwe cha Tundu Lissu tena, kama ilivyo kuwa cha Mbowe. Chama ni lazima kiwe cha wanachama wanaoelewa kinacho simamiwa na chama chao.
Hii ni moja ya kazi anayo takiwa kuifanya Tundu Lissu, kwa ushirikiano na viongozi wenzake wa ngazi za juu. Chama kikiwa cha wanachama, moja kwa moja kinakuwa cha wananchi wa Tanzania.

Mkuu Kalamu asante sana kwa analysis nzuri ya mada iliyo ubaoni.

Hili kundi la Mbowe lazima lijue kuwa sababu moja wapo kuu ya WanaCHADEMA kumbwaga Mbowe ni kuwa walikuwa wamechoka na "old same politics" za kubweka sana hadharani kumbe behind the scene unakula njama za kuendelea na "business as usual". Kiufupi wakichoshwa na siasa za kubadili gia angani!.

Lissu alivyodadavua agenda ya No Reforms No Election, Wajumbe wakamuelewa zaidi kuliko walivyomuelewa Mbowe na wakamchagua.

Sasa elections zina condequences, hao watu wa Mbowe wamepoteza uchaguzi, hawaaniniki na wananchi na wanachadema kwa hiyo ni either wamsaidie Mwenyekiti wa sasa kwa ajili ya maslahi mapana ya chama, au wajipange kushawishi vikao halali vya chama vibadili mtizamo, au vingoje vikao vingine vya chama wapeleke hoja ya ushawishi ili hoja yao ipate baraka. Lakini kwa sasa, NO REFORMS NO ELECTION ni maamuzi ya Kikao cha juu kabisa cha chama yaani Mkutano Mkuu Taifa!.
 
Ebu nipe impact ya No Reform, No Election huko Kanda ya Nyada. Kuna mtu kasema hatapiga kura? Kuna Wana Chadema wamesema hawatagombea? Kama ni hivyo kikao na wataka kugombea lilikuwa cha nini kama wameilewa No Reform, No Election?

Usisubiri impact, changia impact itokee.

It can be done, play your part!
 
C
Basi ni dhahili chadema haija-heal kutoka kwenye madonda ya u-team Mbowe na Lisu. Chama kina kazi kubwa ya kufanya alafu Mbowe underground ana nguvu sana na wafuasi wake wako strategic kuliko yeam Lisu. Ipo kazi ya kufanya hawa walioleta hoja si wa kubezwa lazima kuwe na mkakati wa kudeal na hiki walichoanzisha
HADEMA haisubiri huruma za CCM katika nyuso zake mbalimbali kupona (to heal).
Kazi kubwa pekee iliyopo sasa hivi mbele ya CHADEMA Mpya chini ya uongozi Mpya, ni kufanya kazi na waTanzania kuleta mabadiliko chanya. Ni wananchi pekee watakao iwezesha CHADEMA kuheshimika na kutimiza malengo ya kuleta mabadiliko katika mfumo wa chaguzi za nchi hii. Hayo ya akina Mbowe na wafadhili wao toka CCM, hizo ni 'side shows' tu zisizoweza kuzuia chochote.

Mimi sijui huyo "Mbowe wa underground, mwenye nguvu sana" unamnunua duka gani wakati huu! Pengine hizi ni fikra tu za matumaini zinazo stawishwa huko ndani ya CCM. Asipochukua tahadhali, hata hizo sifa chache alizo salia nazo zitageuka na kumtia fedheha kubwa. "'Strategic"? Mbowe kuwa na 'strategy? Ingekuwa hivyo asinge kubali kujichotea fedheha na kujivunjia heshima kwa kung'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa chama. Sioni u"strategic' wowote na hatua hiyo aliyo ichukua wakati huo, na wala sioni anavyo weza kujiondoa kwenye aibu ya kufanywa kibaraka wa Samia.
All-in-All, sioni point yoyote ya maana ya kumnyanyua Mbowe kutoka kwenye aibu kubwa aliyo jichotea mwenyewe.
Kama upo karibu naye, mkuu 'suset' ni vizuri kumshauri akae pembeni bila ya kuvuruga chama alicho kitumikia kwa muda mrefu.
 
MBOWE ni mwizi na msalit wa Watanzania .... MBOWE anapaswa kuzomewa na KILA mtu. MBOWE ameitumia chadema kujinufaisha yeye na kikundi kidogo cha wapuuzi.
 
Back
Top Bottom