Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Mpo Salama bandugu!
Moja ya mambo yanayofanya hii nchi ionekane ni ngumu ni pamoja na mtu kupewa sifa za Uongo.
Mfano; nchi hii kuna watu utaambiwa wanaushawishi au wanapendwa lakini ukifuatilia uhalisia wa Jambo hilo sio kweli. Utagundua sio kwamba wanapendwa Bali wanatumia Rushwa na kuhonga baadhi ya watu ili waandikwe mitandaoni au kwenye Media kwamba wanapendwa na Wana ushawishi.
Moja ya athari mbaya ya Mtu kupewa sifa za Uongo ni uwepo wa Rushwa. Mtu asiye na ushawishi au sifa atatumia Rushwa au mabavu kujifanya anakubalika ilhali ukweli ni kuwa yeye mwenyewe anajua hakubaliki. Hana ushawishi wowote.
Hii hupelekea baadhi ya wahusika wasio na sifa za kweli za ushawishi kuratibu matukio bandia na kuita vyombo vya habari ili kuonyesha anapendwa.
Watu wenye uwezo na ushawishi hupendelea ukweli na HAKI viwe mbele Yao. Hawahitaji Pesa kushawishi watu Bali uwezo wao wa ushawishi, hulka na Haiba ya kupendwa kwao ndio nguzo muhimu.
Sifa bandia ndio huzalisha Usultani, umalkia, umangimeza, na undugunization.
Watu Bora hawawezi kuwapendelea marafiki Zao au watoto wao wasio na uwezo Kisa tuu mahusiano waliyonayo.
Ndio sababu, watu wasio na sifa za kweli sio ajabu ukaona akamuweka Mkewe au hawara wake, au mtoto wake au family Friends wake licha ya watu hao kukosa uwezo.
Uhalifu unatarajiwa kwa kiwango kikubwa mahali ambapo wahusika waliopewa sifa za Uongo wanapotawala.
Utekaji,
Mauaji,
Rushwa,
Ubambikiaji wa Kesi,
Kuzima Nyota(vipaji na karma) za wengine.
Mtu mwenye uwezo au kipaji kikubwa hawezi kutumia Muda wake kuzima vipaji vidogo.
Ni hakika mtu mwenye kipaji kidogo ambaye anauwezo atatumia nguvu kubwa kumzima mtu mwenye kipaji kikubwa ili kulinda nafasi yake.
Ili jamii iendelee kisiasa, kijamii na kiuchumi ni lazima Ikubali UKWELI kwa sababu kukubali ukweli ni mwanzo wa kutenda HAKI. Na kutenda HAKI ni msingi wa kuinua maendeleo ya Kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k.
Moja ya changamoto kubwa inayokabili bara la Afrika ni pamoja na Watu kupewa sifa zisizo za kweli na hii hupelekea kushika nafasi ambazo hawastahili kuzishika.
Moja ya kiashiria cha kuonyesha jamii Fulani inadhulma, uonevu, ukatili, ni pamoja na Umaskini.
Umaskini hauwezi kukaa pamoja na Watu au Jamii yenye kupenda na kutenda UKWELI na HAKI.
Mchana mwema!