Ukishasema "argument inayotolewa kuhoji legitimacy yake haina mshiko" maana yake kunaweza kuwa na argument yenye mshiko. Ukishakubali kwamba kunaweza kuwa na argument ya legitimacy yenye mshiko, unakubali kwamba hoja ya legitimacy - whether a valid argument or an invalid one- ipo. Kwamba tunaweza kuhoji uhalali wa kiapo kwa msingi wa legitimacy ya misingi ya kiapo.
This is true; lakini the question here is not the legitimacy of the Union. The MPs hawahoji uhalali wa Muungano, maana wakihoji uhalali wa Muungano ni rahisi sana kuthibitisha kuwa ni Muungano halali. Mtu anaweza kuchukizwa na maisha ya ndoa au na vurugu za ndoa bila kulazimika kuhoji uhalali wa ndoa. Na hata watu wanaoamua kuachana wanaweza kufanya hivyo pasipo kulazimika kuhojia uhalali wa ndoa isipokuwa kama wanataka annullment.
Kama yule mtu anayekwambia "ndoa hii si halali kwa sababu huyu mume tapeli, aliponioa aliniambia hana mke na mimi ni mke pekee" na akadai kwamba kiapo chake cha ndoa si halali, basi na hawa wabunge nao wanaweza kutoa argument kwamba walivyoapa waliapa kwa nia nzuri tu, baadaye wakaja kuona mi document kuhusu muungano wakaona wamepelekwa mkenge kuapa kutetea muungano ambao msingi wake ni deception. Kama mtu ana valid arguments hii ni valid reason ya kubatili kiapo.
Absolutely true, lakini Muungano haukuingiwa pasipo uhalali; hawa hawahoji uhalali wa Muungano based on fraud or deception kwani wakihoji hilo wanaweza kufanya hatua nilizozisema hapo juu. Wao wanachohoji ni kutoridhika na Muungano. Well, kutoridhika na maisha ya ndoa hakuondoa validity ya ndoa. Kwamba, mke akikuudhi leo au watoto wakakikukorofisha huwezi kukimbilia kusema "ndoa haipo". Kiapo cha ndoa hakivunjiki au kuvunjwa kwa sababu mtu kapata hasira leo. Mtu anapofunga ndoa - japo si mfano mzuri sana - anadhaniwa kuwa anakubali majukumu na mambo yote yanayotokana na ndoa. Vinginevyo, watu wanaweza wakasema kuwa "nilipoingia kwenye ndoa sikujua kama mwenzangu ataumwa" na akiambiwa si ulisema "katika shida na raha?" na yeye kusema "yeah, lakini siyo shida hizi".
Inategemea na misingi ya kiapo hapo juu. Mfano wa kiapo cha ndoa una apply. Mke akiapa kudumisha ndoa ya mme/mke mmoja na penzi, kwa maelewano kwamba mume naye atafanya hivyo hivyo, baadaye mume akaenda kuoa mke mwingine, ingawa mke aliapa kudumisha ndoa, kitendo cha mume kuvunja kiapo kinampa mke grounds za kuvunja kiapo chake katika talaka.
Well.. unathibitisha ninachokisema kwamba kiapo alichokula mume cha kuwa na mke mmoja kilidhaniwa kuwa anamaanisha. Kwamba, aliposema atakuwa na Mke mmoja mke wake alitakiwa kuamini na hivyo kuamua kwake kwenda nje ni kinyume na kile alichoapa na hivyo kama ulivyosema "kinampa mke" grounds. Hicho ndicho ninachosema. Hawa watu wametaka tuamini kuwa waliposema kuwa watakuwa "waaminifu kwa Jamhuri ya Muungano" walimaanisha hivyo; hawakuapa kuwa watakuwa waaminifu wa Jamhuri ya Zanzibar au ya Tanganyika! HIcho kiapo kuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano kinaingiwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi kama ilivyo kwa viongozi wengine wa serikali ya Zanzibar akiwemo rais wa Zanzibar. Sasa wanapoamua kukivunja (kwa kutaka kuvunja Muungano) wanatupa haki wananchi kudai kuwa watoke kwanza nje ya hivyo viapo.
Nikitumia mfano wako wa ndoa (siupendi kwenye masuala ya muungano) ni sawasawa na mume na mke kukubaliana kuwa katika ndoa ya mke mmoja na mume mmoja. Sasa wakiwa katika ndoa hiyo waliyoapa kuingia mume anaanza kusema "nataka kuoa mke mwingine". Well thats fine lakini yule mke atamuambia huwezi kufanya hivyo ukiwa umenioa mimi! Ukitaka kufanya hivyo hata kutoa kauli za namna hiyo utoke kwenye ndoa hii kwanza. "Huwezi kutaka kuoa mke wa pili, wakati umekula kiapo cha kuwa na mke mmoja".
Lakini nikifuata mtiririko wa hoja yako unasema paraphrasing you - "haijalishi, viapo vinavunjwa"; unasema "kiapo cha mke mmoja na mume mmoja, kinaweza kuvunjwa pasipo matokeo yake". Hapa ndio tunatofautiana.
Kama mtu ana grounds za kuvunja kiapo anavunja vizuri tu.
Of course, lakini not with impunity! wakitaka kuvunja kiapo au viapo vyao wanaweza - ndicho nilichokisema toka mwanzo, lakini wakivunja wawe tayari kulipa gharama yake. Na gharama yake - kwa maoni yangu dhaifu - ni kuwa watoke kwanza Bungeni ili waishi na kuvunjwa kwa kiapo hicho. Hawawezi kuvunja kiapo halafu wakabakia kwenye Bunge hilo hilo ambalo waliapa ndani yake!
Vivyo hivyo, wanaotaka kuvunja muungano wakiweza kuthibitisha kwamba misingi fulani ya kiapo chao imevunjwa, wanaweza kutumia hilo kama sababu nzuri tu ya kuvunja viapo vyao.
Of course, lakini wakishapata huo msingi wa kuvunja kiapo, na wakiamua kuvunja kiapo watoke. Rais akivunja kiapo chake cha Urais hawezi kubakia kuwa Rais. It is that simple. Daktari akivunja kiapo cha udaktari hawezi kuendelea kana kwamba hakukivunja. Wakili akivunja kiapo cha wakili - na anaweza kuwa na legit reason ya kufanya hivyo - bado atawajibishwa kwa kuvunja kiapo hicho.
Kwanini huamini wanaovunja kiapo cha Ubunge wawe tayari kulipia uamuzi wa kuvunja kiapo hicho?
Si lazima, ukibatilisha msingi wa kiapo, na kama una watu wa kutosha waliokuchagua katika contituency yako wana support kuvunja muungano, utakuwa huna haja ya kujiuzulu ubunge.
Hii hoja tuliipitia the other day, wananchi hawawezi kumuunga mkono mbunge kuvunja sheria na yeye akasimama kuvunja sheria kwa vile kaungwa mkono na wananchi. As a matter of fact, it can even be argued - tukikubali hoja hii kidogo - hao wanaotaka Muuungano uvunjwe walifanya poll ya wananchi wao lini, na wananchi waliwapa hiyo mandate ya kutaka kuvunja Muungano lini?
Na kama ni kweli, kwanini huyo Mbunge alipoingia Bungeni aliapa kuwa "mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano" ambayo yeye alitumwa kuja kuivunja? Well ina maana alidanganya - kitu ambacho kinatosha kumvua madaraka yake au hakumaanisha kitu ambacho bado kinaonesha kuwa hakuwa mkweli.
Mbunge ni mtumishi wa wananchi, si wa serikali. Isitoshe, an argument can be made kwamba wananchi hawatakiwi kukaa bila uwakilishi, hata kama ni uwakilishi katika bunge la serikali batili, if that is the process to go to a more legitimate government.
Very true, lakini ni mtumishi wa wananchi kwenye mambo halali tu; hawi mtumishi wa wananchi katika mambo ya uhalifu. Kwa mfano, mbunge hawezi kwenda Bungeni na kutetea uhalifu kwa sababu baadhi ya wananchi wake ni wahalifu.
Point yako inaweza kuwa valid kwa mtu aliye kwenye baraza la mawaziri. It is absurd kusema unaona serikali ya Muungano haina legitimacy wakati wewe mwenyewe umo katika serikali. Lakini hata huyu, kama anafanya kazi kuivunja serikali hii ili kuje kuwa na a more legitimate government, naye anaweza kupata utetezi katika hili.
Point yangu is valid kwa watu wote wenye kula viapo vya ofisi au majukumu fulani.