ngamiamzee
JF-Expert Member
- Jun 6, 2011
- 245
- 18
Ala! Kumbe Kuvunja Muungano kunawezekana Kikatiba!, sasa kumbe tunajadiliana nini hapa!
Kumbe wale wabunge wanaosimama Bungeni na Kutaka Muungano Uvunjike bado wako ndani ya msitari wa kisheria kwa sababu Katiba imetoa nafasi ya kufanya hivyo, ilimradi tu theluthi mbili ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri na Theluthi mbili ya Wawakilishi wawe wameridhia!.
Kumbe wabunge hao "walioapa kuilinda Jamhuri ya Muungano" bado wanaweza kushiriki katika mchakato/kura za kuuvunja huo muungano.
mimi hapo awali nilidhani kwamba mjadala wa kuwepo au kutokuwepo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni off-limit.
Maadamu katiba imeruhusu uwezekano wa kuuvunja huo Muungano tuwaache Wabunge wetu walete maoni ya wananchi bungeni kuhusiana na suala hilo, na ikibidi walete hoja binafsi ya kuwezekana kuupigia kura Muungano.
As usual hujaongea kitu ndugu yangu.Makaimati;2234667]Uhalali wa "muungano" huu haupo tangu pale ulipoundwa maana Articles of Union hazikufuatwa.
Kisiasa, wananchi hatukuulizwa ridhaa yetu iwapo tunataka au laa.
Baraza la Mapinduzi halikuridhia "muungano" huu.
Mkataba wa "muungano" huu umedaiwa Mahkamani na haukutolewa.
Huo ndio uhalali ambao nauzungumzia.
Angalai unavyoji contradict, mara Nyerere kaleta mapinduzi mara Wzbar wanatumia fursa, mara Watanganyika wamelala. Do you real know what you want to say or write. Nakushauri ulete hoja zenye mashiko, hadithi na majungu rudisha huko Mzalendo. Please, unazidi kuvuruga mada kwa hoja usizoweza kujibu. Kama mapinduzi yana mkono wa Nyerere, mnampongeza au kumlaumu? Kila mwaka jan 12 mnasherehekea, kwanini msimpongeze Nyerere kuwatoa utumwani. Yaani wewe unayeitaka Zbar huijui Zbar wala historia yake. Unajua unachokitaka lakini? Rudi mzalendoWazanzbari kwa makundi walihamia bara baada ya Mapinduzi ambayo mkono wa Nyerere umo. Walikimbia mateso waliokutishwa na wakakimbilia hapo karibu na ambapo walihakikishiwa usalama wao. Ujue kuwa Wazanzibari wapo sehemu nyingi duniani ingawa si uomgo kuwa hapo bara wako wengi. Wazanzibari wametumia fursa ambayo nyinyi hamkuiona kabla. Ni hivi karibuni tu ndio mmeanza kuzinduka katika usingizi wenu mzito
GHIBUU, nakumbuka ni Mansur huyu huyu aliyevalia njuga suala la mafuta, kwa vile najua unaelewa fika, kuhusu nguvu na jeuri ya Mhe. Mansur inakotokea mpaka kumpa ujasiri na kuzungumza kwa kiburi hoja za Muungano.Na Mwinyi Sadallah 15th July 2011
Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid
Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid, amevunja ukereketwa na kusema mfumo wa serikali mbili katika sura ya Muungano umepitwa na wakati na kwamba, sasa unaruhusu kuwapo kwa serikali tatu.
"Hapa mpango wa serikali moja hatutaki kulisikia. Mfumo huu butu wa serikali mbili. Sasa basi twende kwa jambo, ambalo kila mmoja wetu analizungumza, la serikali tatu na mengineyo," alisema Mansoor katika mchango wake kwa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati.
Alisema sura ya sasa ya Muungano imegeuka ndoana kwa Zanzibar na inatumika kuwa uwanja wa vitisho kwa Zanzibar inapodai haki zake kama nchi iliyochangia kuundwa kwa Tanzania baada ya kuungana na Tanganyika.
Alisema inashangaza kuibuka kwa viongozi katika Bunge la Muungano kushikia bango suala la mafuta kuwa si raslimali ya Zanizbar kwa maelezo kuwa yapo katika mpaka wa bahari kati ya Tanga na Zanzibar.
"Mimi sitaki kuwataja kwa majina, lakini niseme nawaonea huruma tu, wameishiwa. Lakini hawa ni wale wenye fikra za miaka hiyo ya kutisha Zanzibar hii kwamba wanaona kusimama bwana mkubwa, watu wanaanza kutetemeka,…huku hayo yamepitwa na wakati," alisema Mansoor.
Ingawa hakuwataja, lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hivi karibuni kwa nyakati tofauti kila mmoja alitoa kauli ya kukemea tabia ya kuzungumza suala la Muungano kwa jazba na kuonya kuwa kuanzisha mfumo wa serikali tatu ni kuunda mpinzani dhidi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Mansoor alisema ili kuondokana na vitisho vinavyotolewa dhidi ya Zanzibar, kazi kubwa inayowakabili wawakilishi, akiwamo yeye, ni kuwandaa Wazanzibari juu ya namna ya kushiriki kwa ufanisi katika utoaji maoni ya katiba mpya.
"Tukawaelimishe na kuwaandaa Wazanzibari namna ya kujadili na kuzungumza upya makubaliano ya Muungano," alisema Mansoor ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Mweka Hazina wa CCM na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM).
Aliongeza kama wapo Wazanzibari wanaogopa kuanzisha suala hilo, kwa kauli hii yeye ndio anaanzisha mchakato huo. Kuhusu suala la mafuta na gesi asilia, alisema uamuzi uliopitishwa na BLM na Baraza la Wawakilishi (BLW) wa kuiondoa sekta hiyo katika orodha ya mambo ya Muungano ndio wa mwisho wa malumbano yanayohusu suala hilo.
CHANZO: NIPASHE
GHIBUU, nakumbuka ni Mansur huyu huyu aliyevalia njuga suala la mafuta, kwa vile najua unaelewa fika, kuhusu nguvu na jeuri ya Mhe. Mansur inakotokea mpaka kumpa ujasiri na kuzungumza kwa kiburi hoja za Muungano.Kwa kukusaidieni tuu, yako mambo ya kujadili kuhusu muungano, na yako mambo ambayo sio ya kujadili, miongoni mwa mambo ambayo hayana mdadala, ni suala la mafuta na hili la serikali tatu.Please mark my words, sisi bara, tumekuachieni Wazanzibari mpige kelele zote kuhusu mafuta, kwa vile mpaka sasa, mafuta hayo mnayoyapigia kelele ni yale ya kujaa kwenye kinibu tuu!, lakini ikija kukutikana Zanzibar kuna mafuta ya ukweli, ya kuchimbwa na kuchimbika, basi hao vizabi zabina wote, wanaopiga kelele, watazibwa midomo, Zanzibar si nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo mafuta ni rasilimali ya Taifa. Na hizi choko choko za kuuchokoa muungano kwa hoja za serikali tatu, zitakufikisheni pabaya, badala ya 3, tutakupeni moja, na Zanzibar itageuka mkoa wa visiwani wenye vilaya mbili za Unguja na Pemba!.Nyie haya, endeleeni, msije kulalamika eti hamkujua, nimekwisha waambieni!.
Hivi wewe nini kinakupa jeuri ya kutuiongelea sote? Mimi ni mtanganyika tena nna uhakika kabla yako na naona Muungano wa sasa una mapungufu. Zanzibar ni nchi, sisi Tanganyika yetu I wapi? Tunaitaka haraka sana. Namuunga mkono Yussuf Himid.
Mkuu Tanzania sio nchi ya kwanza kuungana na muungano wao ukawa halali. Hizo taratibu ulizozisema, mimi naomba unipe nchi ambazo imezipitia zote hivyo kuweka mfumo kamili wa uhalali ktk Muungano wa nchi mbili laa sivyo ni mawazo yako wewe mwenyewe. Act of Union pia inategemea na kila nchi, Uingereza wao wameunganisha koloni zao ambazo zote zilikuwa na mtawala mmoja. Wao wana serikali lakini chini ya Utawala wa Queen, hivyo historia ya nchi hiyo ndiyo inatunga muundowa act..
Mkuu Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika January tarehe 12 1964, na hiyo artical of Union imepitishwa tarehe 22 April 1964 ulitaka bunge lipi lipitishe kisheria maanake sijui kama kuna bunge hapo..Ulitaka muungano ufanyike baada ya Zanzibar kufanya uchaguzi mwingine wa wabunge au huelewi kama yale yalikuwa Mapinduzi kukiondoa chama cha Hizbu hivyo kuondoa demokrasia na kuvunjika kwa vyama.
Ridhaa ipi ya wananchi unayozungumzia haswa, mbona hamsemi hata Mapinduzi yalihitaji ridhaa ya wananchi isipokuwa muungano na artical of Union hali wengi wanaochombeza leo hii walikuwa wafuasi wa Hizbu?. jamani mbona mnachanganya vitu kiasi kwamba mnaonyesha hamfahamu nini Mapinduzi na kwamba baraza la Mapinduzi ndilo pekee lilokuwa na nguvu na mamlaka ya kuamua nchi inakwenda wapi.
GHIBUU, nakumbuka ni Mansur huyu huyu aliyevalia njuga suala la mafuta, kwa vile najua unaelewa fika, kuhusu nguvu na jeuri ya Mhe. Mansur inakotokea mpaka kumpa ujasiri na kuzungumza kwa kiburi hoja za Muungano.
Kwa kukusaidieni tuu, yako mambo ya kujadili kuhusu muungano, na yako mambo ambayo sio ya kujadili, miongoni mwa mambo ambayo hayana mdadala, ni suala la mafuta na hili la serikali tatu.
Please mark my words, sisi bara, tumekuachieni Wazanzibari mpige kelele zote kuhusu mafuta, kwa vile mpaka sasa, mafuta hayo mnayoyapigia kelele ni yale ya kujaa kwenye kinibu tuu!, lakini ikija kukutikana Zanzibar kuna mafuta ya ukweli, ya kuchimbwa na kuchimbika, basi hao vizabi zabina wote, wanaopiga kelele, watazibwa midomo, Zanzibar si nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo mafuta ni rasilimali ya Taifa. Na hizi choko choko za kuuchokoa muungano kwa hoja za serikali tatu, zitakufikisheni pabaya, badala ya 3, tutakupeni moja, na Zanzibar itageuka mkoa wa visiwani wenye vilaya mbili za Unguja na Pemba!.
Nyie haya, endeleeni, msije kulalamika eti hamkujua, nimekwisha waambieni!.
Excellent!
Tumekaa pamoja kwa miaka 50. Bila kujali uhalali au uharamu wa muungano kuna vitu vinaitwa Intermmariage,Cultural mingling, investment and dependence in government level. Ni kwa msingi huo lazima uwepo utaratibu wenye nidhamu katika kufikia suluhisho.
Kinachojitokeza ni watu kutaka kukiuka taratibu kwa nia ya kuchochea. Tanganyika kama Wzbar wamechoshwa na malalamiko dhidi yao.
Taratibu zinaruhusu hoja zijadiliwe, lakini utaratibu wa kuamka na kusema tuvunje muungano tena kwa yule yule aliyekubali sera za chama chake na katiba chini ya kiapo ni aina ya 'uasi'. Kwani kuna ugumu gani kufuata taratibu kufikia hitimisho?
Suala la serikali 3 kwa sasa ni ndoto. Kwa umimi wa Wzbar, Wabara nao wamejifunza. Swali ni je hizo serikali tatu zinagharamiwa vipi na zinafanyaje kazi? Nini role ya serikali ya shirikisho na rais wake hasa ukizingatia ubinafsi uliotawala.
Waswahili wanasema, mwiba hutoka mahali ulipoingilia, kwanini tutake kutoa mwiba jichoni tukijua uliingia mguuni!
Naomba upitie kijitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania - kipo hapa. Nashukuru kuwaona siku hizi kina Sitta na wenzie wameanza kureason kwa namna ile ile ya Nyerere. Ninachokisema hapa ndicho Nyerere pia alikisema. Sera ya CCM ni serikali mbili, wabunge wake 55 hawakuwa na mandate ya kuja na serikali tatu. Aliwaambia wakitaka kwenda serikali tatu, lazima kwanza wabadilishe sera ya serikali mbili.
Eeh-mhh Campanero nakusoma vizuri, lakini ndiyo suruali inayotusitiri, ile mpya walifanya window shopping wametoweka na hatujui tutaipata lini.Mwanakijiji Katiba haina uhalali ndio maana wanaivunja. Tuunde Katiba mpya yenye uhalali. Kisha tutawawajibisha wakiifanyia (huu) uhaini.
Mwanakijiji Katiba haina uhalali ndio maana wanaivunja. Tuunde Katiba mpya yenye uhalali. Kisha tutawawajibisha wakiifanyia (huu) uhaini.
Mzee kama Katiba ya sasa wameshindwa kuillinda ni kitu gani kitawafanya waitete hiyo nyingine? Kama tunashindwa hata kuwaambia watoke Bungeni sasa tutaweza vipi huko mbeleni? Nyerere aliuliza hoja hii hii kwenye UWHT.