DOKEZO Wanaotangaza kuuza Viwanja kwenye Vituo vya Daladala na spika zao walipie kodi ili iboreshe vituo vya hivyo

DOKEZO Wanaotangaza kuuza Viwanja kwenye Vituo vya Daladala na spika zao walipie kodi ili iboreshe vituo vya hivyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Haya Matangazo ya viwanja "Vinauzwa na Hati" yanayosikika karibu kila kituo cha daladala hapa mjini Dar kupitia sauti kubwa kutoka kwenye spika zilizowekwa, ni kero kubwa kwa abiria na wananchi kwa ujumla. Kila ukigeuka, unaskia matangazo yanayohusiana na viwanja vinavyouzwa, na hivyo kuondoa utulivu wa eneo hilo kutokana na kelele zisizo na tija, hasa katika maeneo yenye shughuli nyingi.

Pendekezo langu ni kuwa mamlaka zikusanye kodi kutoka kwa wamiliki wa matangazo hayo, na fedha hizo zitumike kuboresha miundombinu ya vituo hivyo ili kuwe na mazingira bora zaidi kwa abiria wanaotangaziwa.
1733216070315.png
 
Chanzo kizuri cha mapato kuliko kile cha kuwachaji watu mikojo yao
Kabisa mkuu, inaweza kusaidia kupunguza kero na kuboresha huduma kwa abiria, huku likichangia maendeleo ya maeneo hayo kwa ujumla
 
Kuna wale wanauza viwanja mkuranga na mlandizi na vikirikuu vyao "nunua kiwanja kwa shilingi laki 5 na upewe nyongeza"
 
Hivi huwa sio matapeli kweli hao. Mimi siwaamini hao watu hata iweje.
 
Hizo speaker ni noise pollution, zinatesa sana abiria, mateso hayo hayavumiliki, soeaker ziondolewe
 
Back
Top Bottom