DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Walipe ushuru Watawala wajaze mafuta kwenye ma V8 yao.Mtu aliyejitambulisha kuwa Afisa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amesikika akitoa tangazo kwa kutumia kipaza sauti katika Soko la Ilala Boma na Karume akiwataka wauzaji wanaotembeza vitumbua, karanga, kahawa na mifuko kuanza rasmi kulipa ushuru kila siku.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, maelekezo hayo yametolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Aidha, ameeleza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekaidi maelekezo hayo.
kwani wenye maduka au wauza nyanya, mbogamboga n.k kila siku wanapata faida kwenye biashara zao?...Ila mbona wanalipa?Mtu anapata faida ya 2000 alipe ushuru? na kuna kuna siku biashara inadolola
Aan juzi kati tulimbiwa TRA wanakusanya tilioni 30 kwa mwezi....Mtu aliyejitambulisha kuwa Afisa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amesikika akitoa tangazo kwa kutumia kipaza sauti katika Soko la Ilala Boma na Karume akiwataka wauzaji wanaotembeza vitumbua, karanga, kahawa na mifuko kuanza rasmi kulipa ushuru kila siku.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, maelekezo hayo yametolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Aidha, ameeleza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekaidi maelekezo hayo.
Kwa huyu inawezekanaKama ni kweli utakuwa ni utaratibu uliokosa utu hata kidogo, hao wauzaji wa hivyo vitu wana maisha Duni sana!
Makusanyo ya tirioni 30Kama muuza nyanya sokoni anatakiwa kulipa ushuru wa 500 na 200 ya ulinzi shirikishi wa soko kwanini wauza karanga ,sigara, maji,vitumbua n k wasilipe ushuru wa soko?..
Watanzania tuache kujiendekeza, yaani unafanya kazi,unapata kipato halafu hutaki kuchangia chochote kwa maendeleo ya eneo lako...unategemea nani akulipie?