Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Jamaini sijui kama wenzangu huwa mnajiuliza hawa watekaji huwa wanafanya hii kazi ya kupiga mpaka kuua katika mazingira gani na wao wenye mentally huwa wanakuwa katika hali gani.
Najiuliza binadamu wa kawaida unaweza ukashika nondo, kitako cha bunduki, kisu, n.k na ukaanza kumpiga au kumchomo binadamu mwenzako mpaka anakata roho ukiwa na macho makavu na akili tu ya kawaida?
Hata kama umevaa kininja, bila kitu kinachoweza kukuondolea ubinadamu kama bang, n.k, unaweza kuhimili huo ukatili mpaka mtu anakata roho?
Halafu hii shughuli wanaifanyia maporini hata mtu akipiga kelele watu hawasikii au wanaifanyia kwenye vyumba maalumu ambayo ni sound proof au wanawaziba midomo?
Hakika huu ni ushetani wa kiwango cha juu sana na sidhani kama wanaobariki na wanaotekeleza huu unyama watabaki salama hapa duniani.
Na kama baraka zinatoka kwa watawala, wanaweza vipi kushindwa kusaini watu wanyongwe ila wakaridhia uuaji wa aina hii?
Na ikitokea inavuja video ya mateso mpaka mtu anakufa, bado kuna watu watatetea hao wauaji na wanaobariki haya mauji?
Mwisho, kama tu binadamu wengine wanaona tabu kutazama maiti, hawa wauaji wanaweza vipi kutoboa macho maiti tena ya mtu waliomua wao wenyewe?
Hakika baadhi ya sisi binadamu ni mashetani wenye umbo la kibinadamu.
Inasikitisha na kuumiza sana!
Soma Pia: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
I can't imagine!!!