Wanaotesa mpaka kuua, huwa wanavuta bangi kwanza au wanaua kavukavu bila kupata chochote cha kuwaondolea ubinadamu na eneo huwa ni sound proof?

Bangi ni Kama kichocheo kwa hao makatili kupata hamasa ya kuwatesa kikatili.

Kuna wavuta bangi wengi sana ambao ni watu wa amani ie. Marastaman wengi wanavuta msuba na ni watu peace sanaa ✌️

Bangi inafanya asili ya mtu iwe wazi, sema wengi ndio wana asili ya uovu, dhana ya kuihusisha bangi na mambo ya ajabu ni dhana potofu
 
Mkuu inauma sana .
Ukiwaza anayefanyiwa hivi ni wewe, baba yako mzazi au ndugu yako wakaribu just imagine? Maumivu unayopata? Na sababu kuu eti kuwa mpinzani....Aisee!!

Kweli kutofautiana kisiasa inapelekea mtu anaacha mjane au watoto yatima? Inafikirisha sana!!!

Hivi inawezekana dunia ya leo watu wote wawe chama kimoja? Dini moja? Kabila moja?

Wauaji mnatukosea sana tunao baki kutufanya tuamini Duniani hapa kuna Miungu watu wakuamua nani aishi nani abaki.

Muda ni suluhisho la tatizo..tujipe muda. Kuna wachache wameamua kutuharibia kabisa Taifa letu kwa masilahi yao mafupi.
Kuna mdau alisema Nchi yetu yenyewe masikini wakutupwa tuna siri gani za maana mpaka tunatekana na kuuana.
 
Utashaangaa mkuu wakati kila siku madini na maliasili zinabebwa kila kukicha.

Kinachofanyika ni kutufanya tuwe woga ili waendelee kuiba na kupeana vyeo.

Amani gani tuliyonayo kama umasikini na ufukara imetawala maeneo mengi Tanzania hii.
 
Jamaini sijui kama wenzangu huwa mnajiuliza hawa watekaji huwa wanafanya hii kazi ya kupiga mpaka kuua katika mazingira gani na wao wenye mentally huwa wanakuwa katika hali gani.

Najiuliza binadamu wa kawaida unaweza ukashika nondo, kitako cha bunduki, kisu, n.k na ukaanza kumpiga au kumchomo binadamu mwenzako mpaka anakata roho ukiwa na macho makavu na akili tu ya kawaida?

Hata kama umevaa kininja, bila kitu kinachoweza kukuondolea ubinadamu kama bang, n.k, unaweza kuhimili huo ukatili mpaka mtu anakata roho?

Halafu hii shughuli wanaifanyia maporini hata mtu akipiga kelele watu hawasikii au wanaifanyia kwenye vyumba maalumu ambayo ni sound proof au wanawaziba midomo?

Hakika huu ni ushetani wa kiwango cha juu sana na sidhani kama wanaobariki na wanaotekeleza huu unyama watabaki salama hapa duniani.

Na kama baraka zinatoka kwa watawala, wanaweza vipi kushindwa kusaini watu wanyongwe ila wakaridhia uuaji wa aina hii?

Na ikitokea inavuja video ya mateso mpaka mtu anakufa, bado kuna watu watatetea hao wauaji na wanaobariki haya mauji?

Mwisho, kama tu binadamu wengine wanaona tabu kutazama maiti, hawa wauaji wanaweza vipi kutoboa macho maiti tena ya mtu waliomua wao wenyewe?

Hakika baadhi ya sisi binadamu ni mashetani wenye umbo la kibinadamu.

Inasikitisha na kuumiza sana!

Soma Pia: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

I can't imagine!!!
Hao ni wahuni flani, unakuta ni mijitu ina rasta ndefu na makoti. Kwa kifupi ni wahuni bangi mtu bangi

Hao ni wahuni marastaman wavuta bangi watupu ndio wako kwenye hizo operation wao ni kupoke maagizo tu
 
Sasa mkuu kama mtu anapata ujasiri wa kumshambulia mwizi ambae hajamwibia chochote kila ameskia tu watu wananadia kelele za wizi nae ameunga tela na kumpiga vibaya mno
Unauliza ujasiri kwa hao watekaji wanaopata malipo kwa kutenda huo unyama?
 
Naomba nikuambie kitu ndugu, hiyo ni kazi, ni fani kama fani zingine.

Kuna watu watu wanasomea kutesa na kuua, kama vile daktari anavyosomea kutibu na kuponya.

Labda niishie hapo kwanza.
Ukifurahia na kushangilia watoto wanavyoshushiwa mabomu huko Gaza, Sudan au pengine kokote, wewe ndani ya moyo/akili yako hauko mbali sana na hawa wauwaji. wewe ni muombaji wa chuo cha uuaji ambaye hukuchaguliwa lakini unasubiri kuomba katika selection ya 4.

Kwa bahati mbaya hapa JF, watu wenye mioyo namna hiyo si wachache. Tukemee aina yeyote ya ukatili wa kutoa roho za wengine bila kujali mipaka.
 
They have trained to be animal.

we hauwezi hata siku moja!
Binadamu anakimbilia madawa ya kulevya, kwa nia ya kupoteza hisia za kibinadamu ili hisia zake zikaribiane sana na mnyama. Hii inamuwezesha huyu binadamu kufanya matendo ya kinyama, wenyewe tukiyaita eti matendo ya kishetani.

Kwa bahati mbaya huko ndiko dunia inakoelekea kufanya kila linalowezekana kwa jina la PESA.
 
Ukifurahia na kushangilia watoto wanavyoshushiwa mabomu huko Gaza, Sudan au pengine kokote, wewe ndani ya moyo/akili yako hauko mbali sana na hawa wauwaji. wewe ni muombaji wa chuo cha uuaji ambaye hukuchaguliwa lakini unasubiri kuomba katika selection ya 4.

Kwa bahati mbaya hapa JF, watu wenye mioyo namna hiyo si wachache. Tukemee aina yeyote ya ukatili wa kutoa roho za wengine bila kujali mipaka.
Kuna watu wanasikitika sana mabomu yanavyopigwa huko Gaza.

Lakini watu haohao wanafurahia sana uhalifu anaoufanya Putin kule ukraine.

Ni double standard, ni ujinga.
 
Back
Top Bottom