Wanaotesa mpaka kuua, huwa wanavuta bangi kwanza au wanaua kavukavu bila kupata chochote cha kuwaondolea ubinadamu na eneo huwa ni sound proof?

Bangi ni Kama kichocheo kwa hao makatili kupata hamasa ya kuwatesa kikatili.

Kuna wavuta bangi wengi sana ambao ni watu wa amani ie. Marastaman wengi wanavuta msuba na ni watu peace sanaa ✌️

Bangi inafanya asili ya mtu iwe wazi, sema wengi ndio wana asili ya uovu, dhana ya kuihusisha bangi na mambo ya ajabu ni dhana potofu
 
Kuna mdau alisema Nchi yetu yenyewe masikini wakutupwa tuna siri gani za maana mpaka tunatekana na kuuana.
 
Kuna mdau alisema Nchi yetu yenyewe masikini wakutupwa tuna siri gani za maana mpaka tunatekana na kuuana.
Utashaangaa mkuu wakati kila siku madini na maliasili zinabebwa kila kukicha.

Kinachofanyika ni kutufanya tuwe woga ili waendelee kuiba na kupeana vyeo.

Amani gani tuliyonayo kama umasikini na ufukara imetawala maeneo mengi Tanzania hii.
 
Hao ni wahuni flani, unakuta ni mijitu ina rasta ndefu na makoti. Kwa kifupi ni wahuni bangi mtu bangi
Hao ni wahuni marastaman wavuta bangi watupu ndio wako kwenye hizo operation wao ni kupoke maagizo tu
 
Sasa mkuu kama mtu anapata ujasiri wa kumshambulia mwizi ambae hajamwibia chochote kila ameskia tu watu wananadia kelele za wizi nae ameunga tela na kumpiga vibaya mno
Unauliza ujasiri kwa hao watekaji wanaopata malipo kwa kutenda huo unyama?
 
Naomba nikuambie kitu ndugu, hiyo ni kazi, ni fani kama fani zingine.

Kuna watu watu wanasomea kutesa na kuua, kama vile daktari anavyosomea kutibu na kuponya.

Labda niishie hapo kwanza.
Ukifurahia na kushangilia watoto wanavyoshushiwa mabomu huko Gaza, Sudan au pengine kokote, wewe ndani ya moyo/akili yako hauko mbali sana na hawa wauwaji. wewe ni muombaji wa chuo cha uuaji ambaye hukuchaguliwa lakini unasubiri kuomba katika selection ya 4.

Kwa bahati mbaya hapa JF, watu wenye mioyo namna hiyo si wachache. Tukemee aina yeyote ya ukatili wa kutoa roho za wengine bila kujali mipaka.
 
They have trained to be animal.

we hauwezi hata siku moja!
Binadamu anakimbilia madawa ya kulevya, kwa nia ya kupoteza hisia za kibinadamu ili hisia zake zikaribiane sana na mnyama. Hii inamuwezesha huyu binadamu kufanya matendo ya kinyama, wenyewe tukiyaita eti matendo ya kishetani.

Kwa bahati mbaya huko ndiko dunia inakoelekea kufanya kila linalowezekana kwa jina la PESA.
 
Kuna watu wanasikitika sana mabomu yanavyopigwa huko Gaza.

Lakini watu haohao wanafurahia sana uhalifu anaoufanya Putin kule ukraine.

Ni double standard, ni ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…