Wanaotuma na kupokea pesa kwa mitandao ya Simu waongezeka

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
WANAOTUMA NA KUPOKEA PESA KWENYE MITANDAO YA SIMU WAMEONGEZEKA

Sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeendelea kukua ambapo takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 73.5 kwa mwezi Aprili, 2024 hadi laini milioni 90.4 mwezi Aprili, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 22.9.

Watumiaji wa intaneti nao wameongezeka kutoka milioni 37.3 kutoka mwezi Aprili, 2024 hadi milioni 49.3 Aprili, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 32.3.

Aidha Watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka milioni 53.7 mwezi Aprili, 2024 hadi Milioni 66.5 Aprili, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 23.9.

Haya ni Mafanikio ya Utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2024/25 kwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari.
 
Attachments

  • publer-1747587740008.mp4
    883.2 KB

Naam imesiaidia sana, wahusika wa hizo tech wazidi kuboresha zaidi. Ziwafikie waliopo zaidi vijijini
 
Back
Top Bottom