Hii dunia inavituko sana, sababu huwezi kumpangia mtu upande upi anaotakiwa kusapoti kati ya Israeli na palestina. Hata MUNGU hajatulazimisha kumpenda na kutii amri zake, Bali ametuacha tuchague wenyewe kati yake yeye MUNGU na shetani.
Na upande mwanadamu atakaouchagua una matokeo yake.
Nije kwako Mkuu usichokijua binadamu mpumbavu ni yule anayelinga kwa kuona kayawin maisha sababu ya uwezo wa pesa aliyonayo huku akijidangaya hiyo ni baraka tosha kwa MUNGU sababu ya uwezo wa kubadili Milo,kuvaa Vizuri,makao mazuri na gari nzuri za kutembelea.
Narudia Tena huu ndio upumbavu mkubwa tulionao binadamu wengi, sababu unachopaswa kulingia ni pumzi ya uhai akiyokupatia Mwenyezi MUNGU, ambayo ikipotea huwezi kuipata maana ina thamani kubwa sana kuliko utajiri au vyakula unavyofurahia Sasa . Sababu tunaishi kwa upendo wa MUNGU.
Ukisoma kitabu cha mathayo sura ya 4 mstari wa 4,"" YESU KRISTO anamwambia ibilisi, kuwa imeandikwa binadamu hataishi kwa mkate tu, Ila kwa kila neno, litokalo katika kinywa cha Mwenyezi MUNGU. Hivyo tujitahidi kuishi kwa kumpendeza MUNGU maana hatujui saa Wala dakika pia utajiri ulionao ambao ndio tegemezi kwa wengine, isiwe ndio fimbo ya kuwanyanyasa wanaokutegemea.
Maana haujui saa Wala dakika utakayondoka duniani pale pumzi hiyo ya uhai aliyokupa MUNGU itakapokata ghafla, na usijidanganye MUNGU atakupokea sababu ulikua maarufu na tajiri, hivyo ukishatambua kuwa utajiri wa dunia haudumu milele napia niwakupita tu. Ishi Vizuri na binadamu wenzio na usiwahukumu kwa maisha yao wanayoishi Kama wew ambavyo hamna anayekupangia namna unavyoendesha maisha yako.