Wanaouza mihogo wanajiita wajarisiamali

Wanaouza mihogo wanajiita wajarisiamali

Tafsiri ya neno ujasiriamali ni kitendo Cha kuumiza akili(brainstorming) na kubuni jambo ambalo halijawahi kuwepo kwa lengo la kuisaidia jamii. Mfano wa ujasiriamali ni kama vile ugunduzi za engine, kompyuta na n.k.

Sasa sikuhizi unakutana na mama muuza mihogo ya kukaangwa au mchicha anajiita mjasiriamali.
Tanzania, nchi yangu 😅
Kuna vitu vingine sio vya kuchukulia serious

Kwa kuwa tunaelewana maisha yanaenda poa tu

Wafanyakazi wa hospital (manesi, watu wa maabara, wafamasia nk + madaktari ) wote wanaitwa madaktari

Maisha yanasonga as long as tunaelewana

Pia sometimes majina hubadilika (informally) kutokana na matumizi

Mfano tulipokuwa boarding huko MAJI tulikuwa tunamaanisha wanawake (hasa wa shule za girls na wao walikuwa wanatuita DAWA)

ACHA KUCOMPLICATE VITU VIDOGOVIDOGO
 
Tafsiri ya neno ujasiriamali ni kitendo Cha kuumiza akili(brainstorming) na kubuni jambo ambalo halijawahi kuwepo kwa lengo la kuisaidia jamii. Mfano wa ujasiriamali ni kama vile ugunduzi za engine, kompyuta na n.k.

Sasa sikuhizi unakutana na mama muuza mihogo ya kukaangwa au mchicha anajiita mjasiriamali.

Tanzania, nchi yangu [emoji28]
Unataka kusema chuo nilidanganywa na mwalimu wangu na Google ilinidanganya ?

Ujasiriamali ni kitendo cha ku add value katika bidhaa, kwa mfano niuze mihogo ya kukaanga niweke na chachandu huu ni ujasiriamali

Simply put, ujasiriamali ni kitendo cha ku add value katika bidhaa ili kujipatia kipato
 
Mo anajiita Mjasiliamali, nikabaki mdomo wazi. Nikajiambia kumbe Mo hana tofauti na mama Ntilie, maana wote wanajiita Wajasiliamali.

Mkuu chuma cha mjerumani nae ametoa ufafanuzi Ujasiliamali kuwa ni kuvumbua na kubuni.

Mwingine akaniambia ili uwe Mjasiliamali ni lazima uzalishe ama uzalishe na kuuza.
 
Hapo umechanganya Innovation na Entrepreneurship. Innovation kwa kiswahili ndo uvumbuzi ambacho ndo umeelezea hapa. Ujasiriamali ni kuanzisha biashara yoyote mpya au kuendeleza iliyopo lakini katika namna ambayo italeta faida. Sifa kuu ya mjasiriamali ni kutoogopa sana hatari zinazoweza kutokea kwenye mchakati wa biashara (Risks). Mjasiriamali sio lazima awe mvumbuzi. Na pia mvumbuzi sio lazima awe mjasiriamali.

Lakini kwa dunia ya sasa wavumbuzi wengi wamekuwa wajasiriamali pia kwa maana ya kuweka uvumbuzi wao kwenye biashara na kuanza kupiga noti ndefu. Wale wavumbuzi ambao hawakuwa wajasiriamali wengi wao waliishia kupata kiasi kidogo cha fedha au pengine kufa maskini huku akiwafaidisha wajasiriamali makini watakaouchukua uvumbuzi wake na kufanya biashara.

Kina Mark Zuckerberg, Bill Gates na wengine ni wavumbuzi na hapohapo wajasiriamali. Wapo wavumbuzi kama kina Newton tunawasifu ila kwenye upande wa biashara hawatajwi kabisa.

Ulivyotaja mihogo nimemkumbuka mama aliyekuwa anatuuzia mihogo pale mtoni karibu na kanisa la St Theresa, Arusha. Mungu ambariki sana yule mama kwa kutuwezesha wanafunzi kwenye suala zima la mihogo. Tuliokuwa tunaenda maktaba ya mkoa na tuition Arusha Sport mtakuwa mnamkumbuka yule mama. Nimalize kwa kusema wewe Restless Hustler ni mtu wa KUPUUZWA kwenye jamii ya watu wastaarabu.
Sifa kuu ya ujasiriamali ni value creation. Kama huja create value kwenye unachofanya huo ni uchuuzi tu.
 
Kwa iyo muuza mihogo tunamuweka kwenye kundi gani sasa?
Muuza mihogo ni mchuuzi ikiwa anainunua ikiwa in Raw form na kuiuza in the same form. No value addition.

Endapo ikatokea huyu muuza mihogo akainunua mihogo na kuimenya akaikausha na kuisaga ikawa unga na kuuza unga wake kwenye package nzuri tunasema ameiongezea thamani. Huyo mtu ni mjasiriamali. Ameongeza thamani.
 
You are very right mkuu. Hio ndio maana halisi ya ujasiriamali. Ndio maana fundi seremala anaitwa mjasiriamali. Ananunua mbao na kuiongezea thamani kwa kubuni bidhaa mbali mbali.
Unataka kusema chuo nilidanganywa na mwalimu wangu na Google ilinidanganya ?

Ujasiriamali ni kitendo cha ku add value katika bidhaa, kwa mfano niuze mihogo ya kukaanga niweke na chachandu huu ni ujasiriamali

Simply put, ujasiriamali ni kitendo cha ku add value katika bidhaa ili kujipatia kipato
 
Tafsiri ya neno ujasiriamali ni kitendo Cha kuumiza akili(brainstorming) na kubuni jambo ambalo halijawahi kuwepo kwa lengo la kuisaidia jamii. Mfano wa ujasiriamali ni kama vile ugunduzi za engine, kompyuta na n.k.

Sasa sikuhizi unakutana na mama muuza mihogo ya kukaangwa au mchicha anajiita mjasiriamali.

Tanzania, nchi yangu 😅
Watz wanachanganya mjasiriamali na mfanyabiashara sana😀😀achana nao hawatokuelewa
 
Tafsiri ya neno ujasiriamali ni kitendo Cha kuumiza akili(brainstorming) na kubuni jambo ambalo halijawahi kuwepo kwa lengo la kuisaidia jamii. Mfano wa ujasiriamali ni kama vile ugunduzi za engine, kompyuta na n.k.

Sasa sikuhizi unakutana na mama muuza mihogo ya kukaangwa au mchicha anajiita mjasiriamali.

Tanzania, nchi yangu 😅
Basi Hata mo na bakressa ni sawa na hao wauza mihogo maana hawajabuni computer Wala machine harafu inaoneka wewe ni first year kwa Padre Pio
 
Kwenye entrepreneurship ndani yake Kuna creativity and innovation achana nao hawatokuelewa ,utapoteza muda kuwaelewesha😀😀
 
kuendesha biashara kwa lengo la kupata faida.

unachokizungumzia wewe ni uvumbuzi(innovation)
Invention ni ugunduzi wa kitu kipya kabsaa ambacho hakikuwahi kiwepo
Innovation ni kuboresha kitu kipya kilichogunduliwa ambacho hakifanyi kazi ama ufanisi wake upo chini basi unakiboresha ili kiweze kua na matumizi halisi (practical applications) na kwa sasa hivi innovation ni kukiboresha kitu kile kile kilichopo sokoni ama kimegunduliwa ila hakipo kwenye matumizi basi unakiboresha ama kukipa thamani kiwe na matumizi ama kitatue changamoto kwenye jamii lakini pia kilete pesa (biashara)
Entrepreneurship ni kubwa zaidi maana yake ni kuconvert invention na innovation into business ili zilete pesa as well as zitatue changamoto kwenye jamii. Innovation ndo starting point ya entrepreneurship
Ina maana sasa, ili uwe mjasiriamali (entrepreneur) lazima uwe innovative (mbunifu) utaanzia kwenye kubuni bidhaa, kuiboresha, kuifanya iwe na thamani na iweze kutatua changamoto, lakini pia ilete pesa kwako. Lakini pia utaenda hadi kwenye kuitafutia soko, namna itakavyomfikia mlaji na mambo mengine kibao humo ndani yote hiyo sasa ni entrepreneurship
Naomba kuwasilisha
 
Hwbu tuoneshe neno kubuni kwa mujibu wa maana hii ya ujasiriamali kwa kingereza. Inaonekana mmesoma kukariri kujibia mtihani na kuelewa.
Screenshot_20230906-231842_1694031573206.jpg
 
Back
Top Bottom