Uchaguzi 2020 Wanaovaa nguo za CCM kwenye mkutano wa Kampeni kwanini baada ya mkutano huzivua kabla ya kurejea makwao?

Uchaguzi 2020 Wanaovaa nguo za CCM kwenye mkutano wa Kampeni kwanini baada ya mkutano huzivua kabla ya kurejea makwao?

Kitu cha ajabu zaidi ni kwamba mkutano wa CCM asilimia kubwa wanaoenda pale unakuta wamevaa nguo za CCM. Tafakari
50% ni wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wanavalishwa hizo nguo ili waende kwenye mikutano.

30% ni wanachama wanaokusanywa mkoa mzima mahali mkutano ulipo.

20% ni wale wanaokwenda kuchukua hizo elfu tano tano wakipewa hivyo lazima wavalishwe na tisheti
 
ccm haina tofauti na mwanaume anayelazimisha mapenzi toka kwa mwanamke (inabaka)!.
 
Swali Hilo muulize mtu wako wa karibu
Habari ndugu

1954 nadhani ndo mwaka uliozaliwa kwa maana iyo we ni Kama baba/ mama yangu.

Najua unamtetea mwenyekiti wetu wa CCM Ila ni mwongo afu hanaga kumbukumbu kwa uongo wa Jana kuwa hakumtumbua Gambo Arusha kwa matumizi mabaya ya ofisi nimeanza kutomuamini kwa maneno yake mengine..

Nakuomba Kama baba/mama yangu tusichague kwa mazoea Tumpe kura za ndio Tundu Lisu 28 10 2020

Chagua Tundu Lisu kwa Haki za Kila mtu na wazee



Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Umejaribu kufananisha lakini umekosa akili kuwa CHADEMA hakuna opportunities wala masirahi.Ukiona mtu yuko Chadema ni kwa moyo wake wote maana hata kampeni tunachagia,hatuna pesa za kugawa

Tafuta mfano Mwingine malaya wa kisiasa
Haaaa wewe ni Chadema wa ukweli...mnaodhani kuwa wengine wote hawana akili isipokuwa ninyi ndio wenye akili...Yaani kwa akili yako uwezekano wa kupata ubunge uwe wa kuteuliwa au kuchaguliwa unaona siyo opportunity??! Ndivyo unavyoamini wewe?! Basi Mimi nakuambia ninao marrafiki watatu mmoja wao nimesoma naye wameingia Chadema kwa kuwa uwezekano wa kupata ubunge ni kubwa..wote walikuwa wabunge Bunge lililopita, ila kwa asilimia Mia moja ni CCM...wakipiga kelele majukwaani kuikandia CCM huwezi kuamini..
 
50% ni wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wanavalishwa hizo nguo ili waende kwenye mikutano.

30% ni wanachama wanaokusanywa mkoa mzima mahali mkutano ulipo.

20% ni wale wanaokwenda kuchukua hizo elfu tano tano wakipewa hivyo lazima wavalishwe na tisheti
Nilikuwa najiuliza hivi inakuwaje hii mikutano ya CCM kila mtu kavaa nguo aa chama yani hamna wananchi wa kawaida wanaoenda kusikiliza tu !
 
Mleta mada ndio maana huolewi umebaki nungayembe mwongo mkubwa wewe kwa hiyo hizo nguo huwa wanavua mkutanoni na kurudi uchi au?

Wewe kuolewa sio rahisi
Wewe lini umeolewa? Unadanga tu hapo Lumumba watu wanajipimia tu kama pombe ya ngomani.
 
Habari ndugu

1954 nadhani ndo mwaka uliozaliwa kwa maana iyo we ni Kama baba/ mama yangu.

Najua unamtetea mwenyekiti wetu wa CCM Ila ni mwongo afu hanaga kumbukumbu kwa uongo wa Jana kuwa hakumtumbua Gambo Arusha kwa matumizi mabaya ya ofisi nimeanza kutomuamini kwa maneno yake mengine..

Nakuomba Kama baba/mama yangu tusichague kwa mazoea Tumpe kura za ndio Tundu Lisu 28 10 2020

Chagua Tundu Lisu kwa Haki za Kila mtu na wazee



Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Tundu Lissu siwezi kumchagua ...wakisimama na Pierre Liquid nitamchagua Liquid awe Rais lakini siyo Lissu mpenda ushoga na kibaraka wa mabeberu...hivi hujui kuwa Lissu ndiye muongo nambari wani na tapeli wa kisiasa asiye na kumbukumbu? Aliwahi kusema ACT Wazalendo siyo wapinzani Bali wametumwa na CCM ...clip yake imo humu JF...aliwahi kusema Magufuli ndiye Rais anayefaa lakini Leo anamponda...aliwahi kusema Rais Magufuli amekutana na wasimamizi wa uchaguzi kosa lililomfanya afungiwe siku Saba kwa uongo...Lissu anataka kuuza nchi kwa mabeberu, sisi Watz tulio wengi hatuwezi kukubali...Jumatano ijayo atashindwa vibaya...nikiona picha ya Lissu binafsi huwa naona Kama nimeona shetani..
 
Shukrani sana mtaalam nilikuwa kwenye harakati za kumtafutia zilizotupwa uwanja wa Mkapa maana zilitapakaa na machupa ya maji, kwako mwalimu Lombo, tuiwekeje hii?
Hii tunaita'fukuza kichaa na makopo yake' na katika imani tunasema'namkataa shetani na mambo yake yoooote'.
 
Mi bado nimeivaa nguo ya ccm na nimelala nimeivaa we nani ujifanye kuwasemea watu? mbuzi we!
Mods huyu mbona anatukana watu kwa jambo ambalo na ushahidi tumeweka hapa?
FB_IMG_1601898597063.jpg
 
Mikutano mingi ya Chama cha Mapinduzi inapomalizika eneo la tukio watu wenye uniform za chama upotea au kuzibadilisha na hivyo kutoonekana wakiwa wamezivaa kurejea makwao.

Miaka ya nyuma mtaani watu walikua wanaona fahari kuzivaa kuanzia bodaboda, mama ntilie, wajumbe na watu wengine. Ilikuwa sawa na mchuano wa Simba na yanga panapotoa droo ambapo kila mmoja uvaa jezi kwenda nayo hata bar au maskani.

Ni kweli kwamba Hawa wanaovaa hizi nguo wanavaa kwakuzipenda au wanavalishwa? Kama wanavalishwa kwanini wanaowavalisha wasiwape masharti ya kwenda nazo nyumbani bila kuzivua?

Hata bodaboda wenye bendera au hata kofia mtaani ambao ni wana CCM wanakosekana? Afadhali vyama vingine ambavyo wapenzi wao watasema wanawindwa na dola, CCM kwanini mmekosa imani na nguo zenu?

Mtu kama anaogopa kuvaa jezi mtaani kwake unamtenganishaje na msaliti? LIPO TATIZO SEHEMU, TULIKOSEA
Wengi wanazivaa juu ya nguo zao. Nafikiri wanapewa siku hiyo hiyo kwenye tukio na kwa sababu maalum waliyoitiwa au kielekezwa kuhudhuria mkutano. Nafikiri pia wengine ni watumishi wa umma.
 
Umejaribu kufananisha lakini umekosa akili kuwa CHADEMA hakuna opportunities wala masirahi.Ukiona mtu yuko Chadema ni kwa moyo wake wote maana hata kampeni tunachagia,hatuna pesa za kugawa

Tafuta mfano Mwingine malaya wa kisiasa
Kwahiyo Mzee Lowassa alikua Chadema kwa moyo na sio opportunity ya kugombea Urais si ndio Mkuu
 
Idadi ya wanaccm waliopo kwenye picha ni saba(7)
Idadi ya wapiga kura halali kwenye picha ni watu wawili (2)

Hii inamaana ile mikutano yao ni 2 ya saba tu (2/7) ndio watakao piga kura.

Yaani kama mkutano ulikuwa na watu 700 watakaopiga kura ni watu 200 tu na hao miambili wana jambo lao la moyoni hivyo idadi inaweza pungua hata kuwa chini ya 200.
 
Mimi pia nilikutana na kiongozi mmoja wa Chadema ambaye tulikuwa wote mahali nikamuuliza kwa mshangao je, na wewe uko huku? Akanijibu kuwa anaganga njaa kwenye opportunities na kwamba wapo wengi huko...akasema hawezi kumpa kura kibaraka na mpenda ushoga..tehteh
Hii umetunga mkuu. Tunga nyingine kwani hii kwangu haina mvuto.
 
Lissu alisema watu wanapewa elfu5 tano kuhudhuria hiyo mikutano lakini wanafunzi pia hulazimishwa maana yake ni kwamba huwa wanapewa hizo nguo ili kutengeneza uniform wanapokuwa pale uwanjani ili nchi na dunia waone wanaungwa mkono sana nchini. sasa matarajio ya mtu uliyempa kitu kidogo akufanyie jambo lako ni pale akifanya tu akimaliza hurudi kawaida yake na sio tanganyika tu ata kule zanzibar.

kwa mfano hizo kampeni maisha ya boda boda yamekuwa nafuu sasa huwa wanatiliwa mafuta kwenye mahonda yao, wakapewa na hizo fulana na kofia wengine apart from mafuta pia hula cash buku 10 au 20 na ubwabwa wakirudi kama kawaida wanapiga.

Haya si mambo ya kutaka majibu ni jambo limezoeleka sana uchaguzi ukikaribia, mtu 1 kule zanzibar alifanya hivi sana kwenye kampeni zake na alikuwa na matumaini makubwa sana lakini kura zake unguja na pemba hakufika ata kura 300 ni ule ujinga tu kwamba machoni mwa watu uonekane una watu lakini aibu na fedheha ni siku ya kuhesabiwa kura zako.
 
Back
Top Bottom