SEHEMU YA KWANZA (1) CHINI KUNA NAMBA-2
(1) Najua miangaiko inachosha poleni na hizi varangati za kushabikia mapambano ya wakuu wa nchi angali hatupati chochote; watupe/watukabidhi nchi tu hii wananchi tuiongoze/tuisimamie wenyewe.
(2)husika na kichwa cha habari
Naomba nianzie mbali kidogo ila kwa ufupi ntaeleza sitawachosha na urefu wa mlolongo huu mtamu ( wanao yabeza/kuyadhalau maisha ya south Africa (ASTROWAY)
(i) 2012- nilihitimu elimu ya kidato fulani (?) na matokeo yakikuwa mabovu sana na hata sikujali kutokana nilijua tu kutokana na mazingira na jitihada dhaifu nilizowekeza- zilipelekea kupata matokeo mafupi na kusababisha kutoendelea na masomo; poleni sana tuliozaliwa katika familia masikini naamini M/MUNGU anatupitisha kwa maksudi ili tujifunze vitu tofauti.. wazazi hawakubeza matokeo.. ila mama alikuwa na imani sana kwamba lazima ntafaulu ila ilikuwa tofauti pole na asante sana mama yangu kwa kuniamini kijana wako.. asante tena mama. DADA zangu walinicheka sana ila leo wanaamka na kuwapikia wanaume ambao hata darasa la saba mtihani na elimu zao za juu ni bure kabsa.. Baba alipata hasara sana .. hivi nyie wakina dada kwa nini lakini kibaya zaidi wanume wenyewe wanawivu hawataki hata wake zao wafanye kazi.. wamepata elimu za sheria na kuziweka kabatini— yote kwa yote nawapenda sana madada zangu.
(ii) kiufupi nilipoishia hiyo elimu zushi (2012) nilikuwa msela sana 2013-2014 hapa nilikuwa haunigusi bro- sister nakuzingua peupe alafu niliakuwa kijana mdogo sana nimelala sana vituo vya polisi: sijisifii ila napenda tujifunze kitu wakuu kwa wadogo zetu.. tuwafunze nashukuru nimetoka katika ujinga huo na nimejifunza mengi asante M/MUNGU. Nashukuru tangu nipitie katika kipindi hicho sijawahi kutumia uraibu/vilevi vyovyote vile japokuwa kampani yangu yote ndio vitu wanavyofurahia wakiwa katika maisha yao ya kila siku.. bange, unga,pombe na midawa mingine
Nisisitize kijana wenu ni mstaarabu sana.
(iii)WASHUKURIWE WASOMI WOTE
Kilichonisaidia kutoka katika utukutu na usela uliyokithiri ni mabrother wa mtaani ambao wasomi wa level flani ya kielimu na fani kabambe: kama watatu wanne hivi nawashukuru sana.. sana maana walijua asili yangu ni ustaharabu na home walikuwa wamesha nishindwa kiufupi maana walikuwa wakiipata fresh. Yaani walikuwa wakifurahi na show ya kijana wao bila kutambua nilijikuta nipo upande wa hao jamaa na bichwa likaanza kuwa gumu kwa madini niliyokuwa nikiyapata kwa mda mfupi.. nikaanza kupata muelekeo 2015 ile ile akili ikapoa sana kama nilikuwa natakiwa nipate muongozo vilee nilipomaliza kile kidato nashukuru sana.. (nionyeshe marafiki zako nikuambie wewe ni Nani?) angalizo msiwapuuze madogo wanaonekana kuwa wasela na kufanya ujinga mtaani ni swala la kuwaongoza tu .. wafate njia sahihi.. nawaomba waongozeni wakuu/wasaidieni
(3) (i)waliniongoza vizuri na kunipa madini kem kem na elimu ya kujitambua.. elimu ya kifedha na zingine nyingi asanteni ma brother.. walikuwa wakiniunga katika project zao kama kijana mtulivu kwa malipo pia.. walikuwa wakipokezana mimi,
Pia walikuwa wakiishi tofauti lakini jioni lazima wakutane kwenye vikao vyao na lazima wanipigie simu niwepo.. kaa karibu na uwaridi unukie.. nilikuwa nipo vizuri kwa madini yao tu kuyasikiliza ilikuwa nikichangamana na watu wengine mtaani walikuwa wanasema mwanetu umekuwa kichwa kinoma mambo magumu kama hayo umeyatoa wapi? Nachekaga sana .
(ii) 2016 brother wangu wa familia moja akapata connection ya kwenda SOUTH AFRICA (SA) kutafuta .. kabla tulipiga story na kukubaliana kama akipata vipesa anipe msaada na mimi wa kwenda huko .. kutafuta kwa lengo la kusaidia familia BABA /MAMA , dada zetu .. watoto wa dada zetu (wapwa) wadogo zetu na ndugu zetu wengine na sisi wenyewe kiujumla..ALHAMDULLILLAH alisota miaka miwili akanivuta na tukawa tunashikamana kuwasaidia wazazi
(iii) kama ndoto baada ya mda mchache tumewasaidia tumewajengea wazazi( wazee) nyumba nzuri ya kisasa na kila siku wana uhakika wa kupata chochote kwa kuendelea kupata kutoka kwa watoto wao wakiume pekee.. Kule nilikuwa najihusisha na masuala ya duka.. muuza duka wa SOUTH AFRICA.. nimejifunza mengi sana huko.. na huko ukijifanya ujanja mwingi utaomba nauli urudi nyumbani tena kwa kelele nyingi za vilio yaani nchi imevurungwa ilee.
Nashukuru sasa nipo DAR kwa mara nyingine mji umezidi kuwa mzuri pongeni MH; MAGU najua haya ni matunda ya enzi zako ulale mahali pema amiina.. na si haba nna mil-3 mfukoni kama yakuja kufanya chochote hapa nchini kama kijana ambaye sijafikisha miaka 30 naweza nikafanya uzushi wowote ule na ukanitoa kwa hiki hiki kiasi changu kidogo cha halali, nimeishi miaka 3 ..SOUTH AFRICA na matokeo ya matunda haya ni kujinyima sana wakuu narudia tena ni kujinyima na kuweka akiba nyingi ya pesa ninayoipata na bila kuangalia matumizi yasiyo ya maana.. napanga ndonga niangalie upepo wa bongo niende tena nawahaidi ntakuwa mtulivu zaidi nilivyokuwa mwanzo huko.. nafikilia sijui ninunue kiwanja ngoja kwanza nitulize kichwa nikipata biashara nzuri ntafanya nikiwa na biashara hapa bongo inaenda na kule inasonga maisha yatakuwa mwanana.. niongozo wakuu please
ANGALIZO: CHANGAMOTO
Ukituliza akili (SA) SOUTH AFRICA unapiga pesa chap chap ufanye chochote kile utatengeneza pesa haraka sana.. kuwa muangalifu tena sana
Vijana wengi sana wezi na majambazi walevi mbwa huko hawasaidii wazazi wao huku.. tunakufa sana kwa bastola na kupigwa visu M/MUNGU nakuomba uwalinde ndugu zangu waliokuwa huko.. INSHAALLAH
Chuki za wenyewe kwa wenyewe kuuwana kutumiana watu kuja kukuua au kukuibia sehemu yako ya biashara.. uchawi kurogana.. wakisikia una miaka mitatu kama SA mimi alafu umerudi nyumbani kazi unayondugu yangu ujipange; kwani watu wana 20yrs wapo na bado hawana kitu.. kutembea na wasichana na wanawake wa ovyo nchi hii unatongozwa na mwanamke kaka kwa siku hata mara 3 .. matumizi ya ovyo niishie hapa.. MATUMIZI YA OVYO HAWAJUI KUTUMIA PESA ZAO, UNAWEZA KUKUTA JITU LINA PESA LAKINI LINA MENTAL HEALTH.. assume una pesa alaf akili huna hawajui wazifanyie nini? Maisha ya nyumbani kwao mabovu mno ila huku inajifaharisha tu .. wazazi walezi ndugu zao hawawasidii.. M/MUNGU NIEPUSHE INSHAALLAH
Natanguliza shukrani wakuu.. nipo DAR tena nimefikia kwa wazee na nashukuru nimewakuta wazima tena wanafurah tele pale mbele sebleni kuna inch 50 yaani wana enjoy... sikuachaga mchumba wala sina mtoto... ah ah ah ah karibuni wakuuu nawapenda. Asanteni kwa kusoma uzi huu. WATUKUFU ASANTENI.HII NI NAMBA (1) SHUKA CHINI KUNA NAMBA (2) kuna coment moja imenishawishi niiandikie namba 2. Karibuni na asanteni.