Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ni tabia iliyozoeleka kwa watawala wetu wa serikali ya awamu ya tano kujihami na kuwaita wazungu wa nchi za nje, kuwa ni mabeberu, wanapokuwa wametukosoa katika uimarishaji wa demokrasia, uhuru wa wananchi kujieleza na tunashauriwa tuzingatie haki za binadamu.
Lakini kitu cha ajabu ni pale wazungu hao hao, "wanapomwaga" pesa zao katika kutusaidia kwenye miradi mbalimbali, tunapiga "U turn" na tunawasifia na kuwaita kuwa hao ni wahisani wetu na wafadhili wa maendeleo!
Tukizingatia kuwa nchi yetu katika utawala huu wa awamu ya tano kumekuwa na ukiukwaji wa hali ya juu sana wa haki za binadamu, kwa wananchi wengi kubambikiwa kesi za utakatishaji pesa na Jeshi letu la Polisi nchini!
Pale ambapo mwananchi ataamua kutumia haki yake ya kikatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 18(1), kwa kutuhubutu kukemea ukiukwaji huo mkubwa wa binadamu, wananchi hao nao watajumuishwa kuwa ni wasaliti wa nchi yetu na ni watu wanaotumiwa na mabeberu wa nje, kwa vile hawafurahii maendeleo yetu!
Watanzania wenzangu hivi mnaona limekaa sawa kweli hili jambo?