Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Baada ya kuwachunguza sana hawa watu, niligundua yafuatayo;
- Huthamini sana kazi (Kazi kwanza)
- Wana amini kwenye matokeo (result oriented)
- Hutimiza malengo ya kila siku/wiki/mwezi na yasipofikiwa hutathimini kujua walipo kwama
- Hufanya kazi kwa weledi na kujituma sana (huingia kazini mapema na kutoka kazini pale tu anapokamilisha malengo ya siku husika)
- Hupatikana kwenye simu muda wote wakihitajika hata iwe jumapili/Siku kuu na asipo pokea hupiga ndani ya muda mfupi kufuatilia
- Hawana visingizio vya kumfanya achelewe au asiingie kazini (Sio waongo)
- Hutoa taarifa rasmi in advance kama hatakuwepo/atachelewa kazini na muda wa uhakika atakao kuwepo ofisini
- Mteja/mgeni wa kikazi akifika ofisini kwake ni mfalme wakati wote; Wapo tayari kuahirisha chochote wamsikilize au kuelekeza mtu wa kumhudumia
- Ni waaminifu sana ( sio wezi). Hata kama ni mlevi akiachiwa Godown la pombe anajiandikia mwenyewe alichokunywa ili akatwe kwenye mshahara