mwanakijiji upo hata huku?? mi nilijua ni politic tuuuu!tooba!!!
Hivi kwanini kina dada wengine wakati wanatwanga, wanatwanga kwa mbwembwe na kupiga makofi kabisa? WEngine wanaimba na nyimbo na miguno juu; haiwezekani kutwanga tu vikaisha? Nazungumzia kutwanga nafaka ambazo zinahitaji wakati mwingine unyunyizie maji ili zitwangike vizuri.
Nimeyaona haya kijijini. Wanaofahamu huu ufundi wa kutwanga.
Wanajipa rythm ya kazi. Kutwanga sio rahisi, ili kupunguza uzito wa kazi, makofi yale yanawapa ka muziki fulani na hivyo kuwapa stamina ya kuendelea na kazi. Ni kama kuimba ukikimbia mchakamchaka.Kwa kweli ni hoja nzito sana; maana nadhani kuna utaalamu fulani unahusika. Watwangaji wanaojifunza utaona wanavyong'ang'ania mtwangio utadhani utawakimbia; lakini wataalam wanaweza hata kupiga soga huku wanatwanga....
Sijui wengine mnazungumzia vitu gani lakini miye nazungumzia kutwanga kutwanga naona wengine mmenda mbali kweli! .. hii fasihi
Sio maji yanaongezwa, bali ni vitone vya maji huyuyiziwa wakati wa process ya kutwanga toka stage ya kukoboa hadi kutwanga unga ili vumbi la unga lisipeperuke, hayo matone ya maji ni kuongeza kuhesiwe na kupunguza vumbi, hata kule kusaga mashineni, maji huongezwa kidogo.Maji yanayoongezwa baada ya kutwanga ni kazi gani?[/FONT]
mm nafikiri wanaonyesha ufundi wao, maana kijijini mara nyingi mziki ni nadra, so
they intertain themselves, ila kuna ambao hata wanakata kata kiuno nakwambia, basi tu
nawaombea furaha
Sijui wengine mnazungumzia vitu gani lakini miye nazungumzia kutwanga kutwanga naona wengine mmenda mbali kweli! .. hii fasihi
Mwenzetu Mmkjj kwani wewe unazungunzia kutwanga kupi maana kutwanga ni kutwanga tu. Pamoja na kwamba siku hizi mashine za kusaga zimetapakaa nchi nzima thanks to IGA ( Income Generating Activities) project au miradi ya kupunguza umaskini, bado kuna raha ya kula chakula cha nafaka za kutwanga mwenyewe hasa kama unataka kutwanga kiasi kidogo tu. Kwa wale wadada au wamama au hata wakaka/wababa wanaotwanga wanatumia ufundi kuhakikisha.kinachotwangwa hakirukiruki. Mfano kama unatwanga vitunguu swaumu kwenye kinu kidogo shurti utie chumvi kidogo. Kama ni nafaka kwenye kinu kikubwa basi huweka maji ili kukoboa na kuhakikisha nafaka inatoka vizuri.TAHADHARI..usizidishe maji maana nafaka badala ya kutoka unga, itatoka urojo na utapata hasara.
KAZI yeyote ile shurti uitafutia namna ya kuifurahia. Hata maofisini mtu huweka mziki umsindikize ili kupunguza shurba. Kadhalika wakina dada wanapotwanga huweza kuimba na kupokezna kwa kurusha na kudaka mitwangio yao kama namna ya kuifurahia kazi.Ndio utamaduni ulivyo.Waaafrika kazi huendana na nyimbo au ngoma.
Nimichanganya wapi na wewe, ujui kuwa mwjj anakiu ya jibu, kuhusiana na wanaotwanga kwa mbwembwe!Nilikuwa nautafuta wimbo huu kwa siku nyingi sana. Kumbe Mshikaji Tizedboy kashauweka kwenye youtube. Nashukuru sana ingawa umechanganya topic.
Nilikuwa siku zote nikisikia wimbo wa Koffi Olomide, basi unanikumbusha huu wa kiu ya jibu.
Kuna sehemy zinafanana sana sana utafikiri mmoja kaiga mwingine. Ila Sikinde walianza kuimba.