Mzee wa kijiji, kwa kweli hata mimi nimeshtushwa na uwepo wako mahali hapa! Ni kama kumuona mwalimu mkuu darasani ile vap! afu mlikuwa mnapiga kelele.
Anywei,
KWa kweli kutwanga kwahitaji utaalamu na mbinu za kujikip busy. Nakumbuka nikienda kulima, tunalima huku ukiimba, tunalima kila mtu na mstari wake, tunalima weee kila mtu na jembe lake..kamwe hambadilishani! walitumia vyema jembe lako, waongeza utundu hapa na pale, wasimama, wainama, walima kiupande upande, tena wasimama tena..wasonga..kuna wakati wajisikia kuchoka basi washusha jembe (au sijui lashuka lenyewe)..wapumzika. Kuna wakati wahisi kama mikono imekauka, basi watilia mikono mate na kazi yaendelea.
Kila mtu kwa jembe lake..
wakati fulani mtaitana, "Aisee nanii" waendeleaje huko kwako..wengine wako mstari wa tano wengine wa pili na siye wakukua hata wa kwanza na tumechoka vilivyo...jembe limeanguka! limekataa kuinuka hata kwa kulishika na kulazimisha kulima..lol!
Mwanakijiji, nadhani hivyo ndo huwa kwa kutwanga...
ni jambo zuri ukilima na kamziki cha taratibu kutoka kwenye karedio kako ka mkulima..ila ndo ivo kwa wa huko kwenu kijijini labda ata kamukulima akuna...so inabidi mtunge rhythm zenu. Labda we waimba mwenzio yuaweka beat..all in ni ili kazi iende, inoge na msichoke haraka.
Na huko ndo kulima kwetu!!!