Wanasaikolojia mbona kazi yenu haionekani? Matukio ya watu kujiua yanashamiri

Wanasaikolojia mbona kazi yenu haionekani? Matukio ya watu kujiua yanashamiri

Digitalman1tz

Member
Joined
May 17, 2015
Posts
91
Reaction score
216
Wanasaikolojia ni watu ambao ni muhimu sana katika afya ya kila mtu nahii nchi huwa kila mwaka inapokea wahitimu wapya wa maswala ya saikologia lakini mimi sijawahi waona.

Kila mwaka huwa tunapata idadi kubwa ya wanafunzi wanajinyonga wanakunywa sumu sababu ya kuogopa mitihani ya taifa ya kidato cha nne na cha sita hivi mnazani hawa watoto wnapenda, Jibu ni hapana ni kwa sababu ya matatizo ya kisaikolojia.

Hivi kwanini tusutumie hii taaluma kama inavyotakiwa kutumika mimi kama kijana nimesoma sehemu mbalimbali pia nimepata kufanya kazi sehemu mbalimbali lakini sijawahi kutana na hawa watu. Mfano kila shule ilitakiwa kuwa namwana saikologia mmoja au zaidi kama ilivyo taaluma ya ualimu maana wanafunzi wanakutana na changamoto mbalimbali ambazo wanahitaji usaidizi wa wanasaikolgia

Vyuoni pia kuna vchangamoto mbalimbali ambazo wanafunzi wanahitaji usaidizi wa kisaikologia juzi juzi nimekutana na habari ya mwanachuo mmoja mkoani Iringa kukamatwa kwa tuhuma za kumnyonga mpenzi wake. Nimeona comment nyingi za wanajamivi waki mshutumu kijana huyo kuto fanya kitende cha kiungwana lakini hapo sio kusaidia kuondoa tatizo ni sawa tu na kelele cha chura hazimzui tembo kunywa maji. Nazani hapo chuoni kungekuwa na mwana saikologia wa mahusiano huyo kijana angeenda kuongea nae na kutatua chanamoto zake hayo yote yasinge tokea.

Nimewahi kufanya kazi katika hospital moja ya wiliya ya moja ya majiji yaliyopo hapa nchini na katika kufanya kazi nilibahatika kufanya kazi katika wodi ya mogonjwa ya kawaida(Medical ward), katika wodi huwa kuna utaratibu wa kuanisha magonjwa kumi yapokea wagonjwa wengi sana nilikina na wodi hiyo kupokea wagonjwa wengi wanaokunywa sumu na nilibahatika kupkea wagonjwa kadhaa walikunywa sumu na asilimia 98 ni vijana laikini cha ajabu mgojwa akisha patiwa matibabu anatakiwa apewe ushauri lakini hospital haina mtaalamu wa saikologia hivi ndivyo tatizo linazidid kuwa kubwa.

Kila mwaka tunapokea idadi ya wafanyakazi wa vyombo vya usalama kuwapiga risasi wenza wao sababu hawapati huduma sahihi ya usauri wa lisaikologia mfano kwanini kila kituo cha polisi kisiwe na mtaalamu wa saikoligia kwa ajili ya wafanya kazi na waarifa sio hivyo kila ofisi ata ikiwa na mtu wa saikologi si vibaya.

Siku za hivi karibuni vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya,bangi,walevi wa kupindukia sababu ya msongo wa wawazo sababu ya matatizo yanayo wakabili mfano ukosefu wa ajila n.k hawa ndo taifa la kesho wanahitaji msaada wa kisaikologia lakini bahati mbaya hawa watu sijui wanajificha wapi kutoa msaada katika jamii au mnazani jamii inahitaji msaada wa kisheria tu ata wa kisaikolojia.

Unakuta watu kwenye jamii wamefanyiwa ukatili mbalimbali wanapewa msaada wa kisheria baada ya sauti kupazwa wakisaikologia mna muachia nani.

Watu wanalalamika kuhusu swala la nguvu za kiume ivi unajua suala la nguvu za kiume linatibika kisaikologia kabisa mimi nishawahi saidia watu kwa njia ya saikologi na wakawa wanafanya tendo vizuri. Vijana wengi wanahitaji msaada wa kisaikologia kwa ajili ya taifa maana naona nguvu kazi inapotea sana kutoka na matatizo ya kisaikolojia.

Yote kwa yote naomba hawa watu wajitokeze kusaidia vijana maana ndo taifa la kesho.
 
Umenena vyema sana, labda hawajui vitengo vinavyohusiana na taaluma zao, ama wametanguliza maslahi mapana mbele kuliko utu.
 
Wao wenyewe wamejawa na stress za kukosa ajira...
 
Back
Top Bottom