Wanasayansi/ Genius Mahiri kupata kutokea Duniani na Mtizamo wao kuhusu Mungu

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Jamaa wawili walikuwa wanasafiri wakiwa wamepanda ngalawa. Haiyumkini kwa wale wasafiri wa baharini wanafaham Rabsha zitokeazo kunako maji.Wakiwa katikati ya bahari hali ikawa si shwari tena. Bahari ilighafirika na kujenga tashwishi juu ya hatima ya safari yao. Walitamani tu angaa wafike ngamani watulize zao nafsi zilizokuwa zimetahayarika kutokana na dhoruba ile majini. Haikuwa rahisi. Mwishoni katika hali hiyo iliyokuwa imejazwa na kimuhemuhe moja akapaza sauti yake akitizama juu na kusema “kama Mungu upo basi na ushuke kuja kutuokoa” hali iliendelea kuwa ya mashaka na taabu kubwa kwao mpaka walipokuja kusikia mlio wa helkopta ikipita angani.

Mmoja kati ya wale jamaa wawili akapiga nduru akiita ile helkopta …. waliokuwa wamepanda kwenye ile helkopta walitizama chini na kuona watu wakiwa wanasukwa sukwa na mawimbi makubwa… asalaaaaaleeeh…! haraka wakashusha kamba na kuwasihi wakamate wapande. Yule mmoja alipanda akishukuru kuwa sasa amepona na yule mwingine alisikitika na kusema “nilikwambia mimi hakuna Mungu... bila hawa binadamu kuja leo ilikuwa tamati ya maisha yetu” HAKUNA MUNGU.

Kumekuwa na watu kadhaa ambao wamekuwa wakijitanabaisha pasipo kificho kuwa wao ni atheist… yaani wasioamini kuwepo nguvu kuu ya kiroho katika maisha yao. Kifupi wasoamini uwepo wa Mungu. Wapo wakisema hivyo kutokana na kusoma sana na mwishowe wakaja kuona kila kitu ni kutokana na uwezo wa mwanadamu hakuna Mungu wala uungu. Leo tuwaangalie baadhi ya wanasayansi Wakubwa waliokuwa wakiamini kuwa Mungu yupo

Albert Einstein (1879-1955) yeye anasema kuwa “ sayansi pasipo Dini ni ulemaa wa kiungo (utupu) na Dini pasipo sayansi inakuwa na upofu” tafsiri isiyo rasmi . (Science without religion is lame, religion without science is blind.") huyu ni mmoja ya wanasayansi walioleta mapinduzi makubwa sana kisayansi katika karne ya 20. Binafsi nimekuwa nikimsoma sana kutokana na mawazo na michango yake kadhaa katika suala zima la sayansi.alikuwa ni very humble na asiye na majivuno. Ana mchango mkubwa sana katika mapinduzi ya elimu yetu kuhusu Time (Muda) Gravity na Conversion of Matter to Energy (E=mc2) aliwahi kukana suala la kutokuwepo Mungu na akaonekana kuamini katika imani aliyokuwa nayo Spinoza kuhusiana na Mungu ambaye alijidhihirisha mwenyewe kupitia katika vitu vinavyoonekana.

Anasema jambo hili hasa ndilo lilokuwa likimhamasisha na kumtia shauku katika sayansi. Aliwahi kusema akimwambia mwanafizikia kijana “nataka kujua jinsi ambavyo Mungu ameiumba hii Dunia… sina shauku ya kujua janga hili au lile, jambo hili au lile .. nataka kujua mawazo ya Mungu katika jambo husika yanayobakia huwa ni maelezo” yeye alikuwa na msemo kuwa Mungu hachezi au kurusha kete kikamali. Kwa maana ya kwanza hakufanya jambo kwa kubahatisha. Kila jambo lilikuwa au lina sababu zake. Na yeye alitaka kujua sababu hizo ambazo alikuwa nazo Mungu.

Max Planck (1858-1947)
Kwa wale wanaopenda sayansi bila shaka watakuwa wamemsikia sana Max Planck. Hasa katika upande wa Physics na nadharia maarufu sana ya Quantum a.k.a “Quantum Theory” aliweza kuelezea kwa kina sana Atomic na Sub- Atomic worlds. Katika moja ya mihadhara yake mwaka 1937 “religion and Naturwissenschaft” Planck alielezea mtizamo wake kuhusu Mungu. Akisema “Mungu yupo kila sehemu…” akaja kusema kuwa “atheist wao wanawekeza akili yao katika vitu tu na alama mbalimbali… Planck alikuwa mzee wa Kanisa mpaka mwaka 1920 alipofariki. Alikuwa akiamini kuwa vyote dini na sayansi vilikuwa vikipigana vita dhidi ya kutovumiliana na pia mashaka kuhusiana na jambo flani, lakini pia vikipigana kinyume na ushirikina’

Michael Faraday (1791-1867)
Mwana wa mhunzi ambaye alikuja kuwa mwanasayansi mkubwa sana karne ya 19 kazi zake katika usumaku na umeme (magnetism and electricity/electric) si kwamba tu zilileta mapinduzi katika Fizikia lakini pia ilikuwa ni mwanga na mwongozo mkubwa katika maisha yetu leo hii. Maisha haya ya leo kwa asilimia kubwa san yanategemea umeme na uhusiano wake na sumaku( matumizi ya simu,kompyuta,websites n.k) Faraday alikuwa ni Mkristo mzuri sana jambo ambalo lilichagiza sana katika maisha yake na kuathiri namna ambavyo alikuw akitafsiri Asili (nature)

Robert Boyle (1791-1867)

Umewahi kusikia “Boyle’s Law “kwenye mambo ya gesi? Lakini pia huyu ni Mwanasayansi aliyeandika machapisho mengi kuhusiana na kemia. Alifanya mihadhara mingi sana na misa akizungumzia pia Ukristo wake na jinsi ambavyo kuna watu wamekuja kuuharibu n.k alitoa pesa kutafsiri Agano jipya kwa lugha ya Kituruki na Irish aliandika maandiko mengi sana akipinga “Atheism” yaani wale waso amini uwepo wa Mungu.

Isaac Newton (1642-1727)
unazingumbuka newton's laws of motion na newton's laws of gravity? unapozungumzia Optics, Mekanik na Hisabati… huyu jamaa alikuwa ni Genius... acha kabisa.alikuwa ni mtu mwenye kipawa cha kipekee kiakili na gunduzi mbalimbali. Katika sayansi zote pamoja na Kemia aliona Hisabati na Hesabu/namba ni msingi wa kila kitu. (binafsi nakubaliana naye sana) kila kitu alichokifikiria alikifikiria kimahesabu na hili linawezekana kuchagizwa sana historia ya Mungu Kiblia jinsi ambavyo kumekuwa na matumizi ya namba katika kila jambo. Aliamini kuwa maandiko ya kwenye Biblia yamekaa kinamba namba. anasema Theology ni muhimu sana. katika mfumo wake wa fizikia Mungu ni chanzo au centre ya kila jambo. Anasema uzuri uso kifani wa jua, sayari na vilivyomo humo ni kutokana tu na kuundwa na kusimamiwa na nafsi kuu yenye nguvu nyingi. Mungu.

Galileo Galilei (1564-1642)
Galileo Galilei huyu jamaa tunamkumbuka jinsi ambavyo alianzisha mgogoro na kanisa katoliki la kirumi. Chapisho lake kuhusiana na solar system au mfumo wa jua alilochapisha mwaka 1633. Halikuwa na uthibitisho wa kuwa jua ni kitovu cha mfumo huo.aliamini dunia ndiyo inalizunguka jua. Unaweza kumsoma zaid kuhusiana na andiko lake na jinsi ambavyo alikuja kukorofishana na Pope na hatimaye kuja kuhukumiwa. Angalia andiko lake pia akizungumzia mmoja ya wanasayansi wengine nguli kama Johannes Kepler (1571-1630) huyu mwanahesabu mahiri kabisa aliyezungumzia mzunguko wa dunia katika jua na alikaribia kufikia nadharia ya newton kuhusiana na universal gravity. Huyu alikuwa Mlutheri wa kutupwa aliyeamini katika utatu mtakatifu.

hawa ni naadhi ya wanasayansi ambao dunia nzima inawakubali na kuwatambua. ni wasomi wazuri kwa kiwango kikubwa cha kuitwa maprofesa au ningesema ni wagunduzi wakubwa wenye mchango mkubwa katika dunia hii walifikia hatua wakakubali uwepo wa Mungu. tutakuja kuangalia wale waliokuwa ni atheism/waliopinga uwepo wa Mungu na kutusababishia mimi na wewe pia tuwe na maswali kama yao kuhusiana na uwepo wa Mungu. Hivi Mungu kweli yupo?

Moderator threads zangu katika jukwaa hili hukaa muda mrefu sana kwa ajili ya moderation. sijafaham hasa kwa nini mimi. but kama kuna vibali maalum mnatoa kwa ajili ya Forum hii basi nami ningependa kupewa ili mjue napokuwa huku nakuwa na kitu tofauti na sehemu nyingine.
 
Halafu unakuta mtu anatokea huko na kukataa hakuna Mungu, huku watu na elimu zao wanakubali
Mungu alikuwepo yupo na atakuwepo milele na milele
 
Mwenyezi mungu ni mwingi Wa rehema na mwenye kurehemu.inshallah tutamke maneno Haya kwa wingi tutapata baraka zaidi.
 
Ningefura kiranga aje hapa akanushe maneno ya wanafizikia hao. Kirangaaa ukuje wameanza tena
 
Augustinian friar and abbot of St. Thomas' Abbey...Georger Mendel

Huyu ni Father of Genetics
 
Jesuits Fathers

Wana contribution Kubwa mno kwenye maswala ya Earth Quake.....

Sesmology Waves Science and its propagation is also known as Jesuits Science
 
Sijawaona Nicolas Tesla na Niels Bohr kwenye orodha hii
 
Hivi manyau-cats, Na wenzake sio wanasayansi?
Vusamazulu Credo Mutwa / ˈkreɪdoʊ ˈmʊtwə/ (born 21 July 1921) is a Zulu sangoma (traditional healer) from South Africa. He is known as an author of books on stories mixing traditional Zulu folklore , extraterrestrial encounters and his own personal encounters. His most recent work is a graphic novel called the Tree of Life Trilogy based on his writings of his most famous book, Indaba my Children
 
Umemsahau DAB huyu alifanikiwa kugundua theory ya kuwakamata wauzaji wa madawa ya kulevya na kuamini kuwa hata kama hamtothamini kazi yake hapa duniani basi siku moja akiwa Mbinguni atathaminiwa.Aliwatia jambajamba akina Yusuph Manji, Prof Gwajima, Mbowe, Nas Haulage,Dj Majizzo, masogange, wema sepenga, Dj Romiyo, TID etc lakini mwishowe hakuna kilichoendelea Zaidi ya kuachiwa na mahakama kwa kuwa ilionekana ni bifu tu kati ya mtuhumiwa na watuhumiwa.

"Tuko kwenye right truck hata kama uchumi unaelekea kwenye great economic depression"
 
Kuna wanasayansi marufu waliamini kwamba jua linazunguka dunia.

Hilo halikufanya jua lizunguke dunia.

Sayansi si habari inayotathminiwa kwa umaarufu wa mtu, bali kwa ubora wa dhana, zinazopimwana kurejewa na kutathminiwa kwa kina zaidi.

Tuongelee ubora wa dhana, si umaarufu wa watu.

Haowatu wenyewe wengi washakufa miaka miaka zaidi ya 100. Einstein kafariki 1955. Hakujua hata habari za String Theory.
Na Mungu wa Einstein anayemsema hapo hata hajachambuliwa, watu wanaweka tu, bila hata ya kujua Spinoza kaandika nini.
 
Kwakweli hapo kwenye Mungu aliyekusudiwa ndio panafikirisha ..nafuu umekuja ""
 
Back
Top Bottom