Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Gharama ya kuleta hilo jiwe duniani sidhani biashara hiyo italipa.kuna sayari ya almasi tupu huko angani,bora waelekeze nguvu zao huko.google"The diamond planet".Sasa dunia itapata vip utajiri!!!
Hilo jiwe tutawauzia arien au??
Sio kila thread ni UKAWA vs CCMSisi tuna-deal na wapinzani huku tukikabiliwa na njaa licha ya kuwa na mito,maziwa na mabonde chungu nzima.
Nina mashaka na data za habari hii. Uchumi wa dunia una thamani ya trilioni 73 za kimarekani?????? Wakati budget ya wizara ya ulinzi marekani yaweza kufika hata trilioni 5 za kimarekani.WANASAYANSI wa Kituo cha Anga cha Marekani (NASA), wamegundua jiwe kubwa lenye utajiri wa kutisha wa madini ya aina mbalimbali linaloelea angani.
Thamani ya utajiri wa madini yaliyopo katika jiwe hilo, unaelezwa kuwa ni zaidi ya uchumi wa dunia nzima.
Kutokana na ugunduzi huo, NASA wanapanga kuruka maelfu ya kilomita angani mwaka 2023 kwenda kwenye jiwe hilo ambalo kama litafanikiwa kurudishwa duniani, linaweza kuleta utajiri wa kufuru.
Likiwa katikati ya Sayari ya Mars na Jupiter, jiwe hilo linaaminika ni kiini cha ndani cha moja ya sayari zilizokufa.
Kwa mujibu wa wanasayansi, jiwe hilo ni la kipekee na limeundwa kwa madini ya metali kwa asilimia 100.
Jiwe hilo lenye umbo la duara lina urefu wa kilomita 200 na lina madini kama chuma, nickel na wanasayansi wanasema upo uwezekano mkubwa wa kuwa na madini adimu duniani kama dhahabu, platinamu na cobalt.
Jiwe hilo ambalo ni sayari mfu, lina thamani ya fedha nyingi mno, chuma peke yake kilichopo katika jiwe hilo, kinaweza kuwa na thamani ya Dola za Marekani 10,000 quadrillion, hii ni kwa mujibu wa mchunguzi mkuu wa jiwe hilo, Profesa Lindy Elkins-Tanton.
Uchumi wa dunia kwa jumla hivi sasa una thamani ya dola za Marekani 73 trilioni.
“Kwa sasa, kwenda kwa NASA katika anga za juu kunaleta dhana halisi ya ugunduzi. Safari hiyo, itawezesha kufika katika sehemu yenye kitu ambacho hakijawahi kuonekana wala kujulikana. Itatoa nafasi kwa wanasayansi kuona kitu ambacho kilikuwa kinafikirika hadi kufikia hivi sasa.
“Bado hatujaweza kufahamu mambo mengi, lakini tunadhani jiwe hili ni kiini cha metali ya sayari ndogo iliyoharibiwa kutokana na nishati kubwa, mwendo kasi wa dunia,” anaeleza Elkins-Tanton
Mpango huo wa kufika katika anga lililopo jiwe hilo, unatarajiwa kuzinduliwa mwaka 2023 na hadi kufikia mwaka 2030 chombo cha anga za juu kitakuwa kimefika eneo lililopo.
Wanasayansi ambao wametumia muda mwingi kulichunguza jiwe hili wanasema ndiyo jiwe kubwa la metali kwenye mfumo wa jua lililopo umbali wa kilomita 300 na inaaminika kuwa na kiasi kikubwa chuma na nickel.
Jiwe hilo kwa mara ya kwanza aliliona mwanaanga wa Kitaliano Annibale de Gasparis mwaka 1852 na kupewa jina la mungu wa roho wa Kigiriki Cupid.
Mwanzoni, ilidhaniwa kuwa ni jiwe la barafu lakini miaka ya 1980 wanaanga walishangazwa kuona rada ikisoma kuwa jiwe hilo lilikuwa linaundwa na metali.
Wanasansi wanaamini kuwa, jiwe hilo limepoteza ganda lake la nje, kutokana na msuguano na msukumano ambao umefanyika kwa mamilioni ya miaka.
Ili kupata ukweli zaidi kuhusiana na ugunduzi ambao bado unaacha maswali mengi, NASA itapeleka chombo chake katika eneo lililopo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kisayansi ambao unatarajiwa kuchukua muda mrefu.
Hii ni nafasi ya ugunduzi wa aina mpya ya dunia ambayo haijawahi kuonekana, si mwamba wala jiwe la barafu bali ni metali tupu,” anasema Elkins-Tanton ambaye ni Profesa katika chuo Kikuu ha Arizona nchini Marekani.
Anaongeza: "Jiwe hili ni aina pekee ya umbo ambalo limeweza kugundulika kwenye mfumo wa jua, ni njia pekee ya binadamu kuona shehemu ya kiini cha sayari iliyokufa. Mara nyingi tumekuwa tukijifunza sehemu ya ndani au kiini kwa kutembelea na kutizama sehemu za juu.
Chombo kitakachokwenda katika anga lililopo jiwe hilo, kitachukua miaka saba kufika. Pia kitakaa kwenye jiwe hilo kwa miezi sita kikijaribu kurekodi vitu mbalimbali kama muonekano, usumaku na vitu vilivyomo ndani yake.
Mpango huo ni sehemu ya mpango wa ugunduzi wa NASA utakaogharimu dola za Marekani milioni 450 wenye lengo la kujifunza kuhusu mfumo wa jua miaka milioni 10 tangu kuzaliwa kwa jua.
Mpango wa pili utazinduliwa mwaka 2021 ambao utalenga kuchunguza mabaki ya maombo ambayo yapo jirani na sayari ya Jupiter.
Chanzo:Mtanzania
Mi napita sina comments [emoji40]
Igwee ukionyesha hata mchango wangu moja wenye maudhui ya matusi nahama kabisa JfMmh tupia hata kidogo lakini isiwe tusi kama kawaida yako, maana umetukana sana humu sasa umeamua umekuja na utambulisho mpya hahahahaha haya buana
Igwee ukionyesha hata mchango wangu moja wenye maudhui ya matusi nahama kabisa Jf
Nimekuchalange thibitisha
Sent from my SM-J110F using
JamiiForums mobile app
Igwee ukionyesha hata mchango wangu moja wenye maudhui ya matusi nahama kabisa Jf
Nimekuchalange thibitisha
Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile
app
that is a chronic ideas never change mkuu.we.are waiting for new Jesus if he will come againAkili zenu zinawaza uccm na uchadema . mtasubiri sana
holy liarsDola10,000auadtrillion hakika ukibadili kuwa sh hiyo pesa haitamkiki aisse
Nazid shangaaa kuwa jiwe lina urefu kwa 200km?? Walishushaje
Wakati sisi lumumba tunapiga katerero na pombe yetu, wenzetu wanatafuta utajiri nje ya sayari hii. Makubwa!Wakati sisi ufipa tuko bize kusafisha mafisadi,
Wenzetu wanasafisha vyombo vyao kwenda anga za mbali
Mwenyewe nimewaza hilihili.InshaAllah tuombe uzima tujioneeNaona harufu ya vita vya dunia very soon. Kutakuwa na scramble ya mataifa makubwa kama Chna, Rasia, usa, uk . Lazima wadundane hawa jamaa kama hii kitu ni kweli ipo