Wanasema Hayati Magufuli Alikuwa Anakubalika sana: Kwanini basi aliiba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020?

Labda ndotoni
 
Sasa mbona huo upinzani haujafa,Kafa yeye.
Unasema upinzani haujafa?
Acha hizo, jiwe alipiga kila kona ktk upinzani kuhakikisha kwamba wapinzani hawapo TZ, na hao watakaobaki kuwa wapinzani ni wale wa kupewa bilioni 6 wanatulia.

Ni kweli yeye ndiye alikufa, ila upinzani wa sasa haupo hot, lbd waje wapinzani wapya wa kizazi Kipya ila sio hao kina Mbowe, Kabwela mzito, na wote wenye akili za kudanganywa kizembe kisha wakapoa kama maji ya mtungini.
 
Wewe ndio unaona aliiba kwa sababu you are foolish. Baada ya uchaguzi hamujaona mahakama mkapinge japo jimbo moja tu. Kuanzia mwenyekiti wa chadema wote mkajidai mumeibiwa kura majimbo yote kitu hakiwezekani. Mumepandikizana imani eti mlishinda uchaguzi kura zikaibiwa😂. Shame on you. Hivi lissu angeweza kumshinda magufuli?
 
Mahakama zipi tungekwenda wewe kmbwembwe Malaya wa Chato ? Mhakama zote zilikuwa zinapokea maelekezo ya DIKTETA
 
Wewe vipi ? Unamsifia hata kwa maamuzi ya korosho kwa kuwa ni maamuzi? Unamkumbuka hata kwa maamuzi ya kutopandisha mishahara wafanyakazi kwa vile ni maamuzi? Be serious Idimi
Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake bro, naheshimu pia mawazo yako kama ambavyo n wewe unapaswa kuheshimu ya kwangu. Kupishana mitazamo wala sio tatizo
 
  • Inaonekana hujui hata Sheria za Uchaguzi,
  • kipindi kile cha Uchaguzi Mkuu wa 2020 Kuna kanuni ilikuwa inatoa hiyari msimamizi wa uchaguzi kutoa Fomu ya matokeo ya uchaguzi, hiyo Fomu ni muhimu Sana kwenye Kuchallenge matokeo ya uchaguzi, na Kwa hakika Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwapa Fomu.
-Kuibiwa kura majimbo yote inawezekana kabisa, ww Jiulize Kwa nini wabunge wa Upinzani walienguliwa kwenye majimbo yote?, Jiulize Kwa nini wagombea wa Upinzani walikuwa wanaporwa Fomu za Kugombea?
  • Mkurugenzi wa Uchaguzi Wa NEC, alipiga kampeni akisema watanzania hawahitaji "Bra bra" au umesahau?
  • Lissu alizuiwa asifanye Kampeni mikoa ya kusini au umesahau?
  • na Kingine Mfumo wa Mahakama wote ulikuwa na hofu
 
Kwanini aachwe wakati wenzake akina Hitler na Idd Amin bado wanaongelewa, kuongelewa huko iwe kwa uzuri au kwa ubaya ndiyo legacy yake hiyo.
 
Katika maamuzi yote aliyofanya "kuua upinzani" ndio uamuzi mbovu uliomwondolea sifa ya kuendelea kuwa rais wa Tanzania, na aliondolewa
Wewe sema tu ukweli kwamba Wewe ni mshabiki wa vyama vya upinzani ndio maana umeweka mtazamo wa namba hiyo lakini sisi ambao hatuna vyama tulimkubali kwasababu ya uchapakazi wake na uzalendo alionao kwa nchi
 
Kuna watu na viatu. Kwamba Uchaguzi wa 2020 ccm haikuiba?

Tutachukua miaka mingi sana tz kuendelea kwa fikra hafifu kama zako.
 
Umemheshumu sana kumjibu. Ulipaswa kumpuuza tu.
 
Kuhusu kukubalika nakataa!
Kwa mtizamo wangu bila sukuma gang kumuharibia kwa ushamba wa utekaji na uuaji wa kisiasa, Bila sukuma gang kumuharibia kwa kuweka maslahi yao mbele kwa wizi na ujambazi waliozoea hadi kuua vyama vyao vya ushirika; ie SHIRECU na Nyanza
Basi Magufuli angekua rais bora Africa!
-Alionyesha msimamo thabiti dhidi ya hujuma za mabeberu kama Putin
  • Alitekeleza kwa vitendo panafricanism!
  • Hakujikomba kwa namna yoyote ile
  • Ujenzi wa miundombinu kwa kiwango cha mbingu
Walaaniwe sukuma gang waliomponza Rais wetu wa Africa.
Tuwatafute kipindi hiki tuwasagesage kama unga!
 
Wewe sema tu ukweli kwamba Wewe ni mshabiki wa vyama vya upinzani ndio maana umeweka mtazamo wa namba hiyo lakini sisi ambao hatuna vyama tulimkubali kwasababu ya uchapakazi wake na uzalendo alionao kwa nchi
Kiongozi yeyote asiyependa upinzani huwa hajiamini, ila anayejiamini huwa hana hofu na upinzani.

Huyo mliye mkubali kwa uchapakazi wa kimihemko alichemsha sana kuua upinzani.

Mungu mwenyewe anaupinzani ndo ije kwa JPM aongoze nchi bila upinzani? Hakuna kitu kama hicho duniani na ndio maana aliondolewa kabla ya muda wake kwisha
 
Tena aliiba kura kiroho akasahau kwamba upinzani unatakiwa bungeni. Alipostuka kwamba wapinzani wako wachache mno ,Ndipo akala njama za kuingiza C-19 bungeni. Tena wengine wakitolewa gerezani usiku kwenda kuapishwa bungeni! Acha Mungu aitwe Mungu tu. Alitufanyia kitu kizuri sana March 17, 2021!
 
Hao unaowahita wapinzani hawakuonesha ni watu wanaoweka maslahi ya Taifa mbele kwenye kipindi chake Cha uongozi walikuwa wanapinga hadi mambo mazuri yaliyokuwa yanafanyika watakuwaje wanakuwa wa maana? Wanawatetea mafisadi kama Manji,hanspope Serikali inapochukua hatua za kifisadi dhidi yao.Wanapinga miradi iliyoanzishwa bila hata hoja za msingi ilimradi tu waonekane wanapinga, wanapinga hatua zilizokuwa zinachukuliwa na Serikali kuhusu mali zetu za asili ikiwemo madini kwa lengo la kulinda our resources utawaitaje hao jamaa wanafaida? Kitu ambacho nadhani umesahau wapinzani ndio walioanzisha vita na Magu walianza na kampeni ya kusema hawamtambui kuwa ni raisi na awakuishia hapo walimzomea kipindi Cha ufunguzi wa bunge na wakawa wanatoa lugha chafu dhidi yake ilipofika hatua ndio Magu akaanza kuwachukia na akapiga marufuku siasa za majukwaani kwasababu aliona wanatumia vibaya uhuru wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…