Wanasema kwa kejeli ati najitia kuijua historia ya Uhuru wa Tanganyika

Mzee wangu, heshima mbele.

Hoja kuu ya watu ni kwamba baadhi ya chambuzi zako ziko upande mmoja (biased) hasa mrengo wa dini yako.

Sote ni mashahidi historia imepindishwa kweli sio tu Tanganyika bali hata Zanzibar , mfano mwepesi mimi siamini na hadi kesho sitokuja kuamini Karume ni mwanamapinduzi sababu waliokuwepo siku hiyo wanamtaja mwanamapinduzi halisi ilhali Karume alikuwa amejifungia chumbani tu.

Je tunafanyaje huyu mwanamapinduzi halisi apewe heshima yake hata kama alikuwa ni mgeni na wa dini ya tofauti na ile jamii aliyofanya mapinduzi.

Nawasilisha.
Colonel...
Historia ya Karume kama kiongozi inafahamika kwa wote.

Yeye aliwakilisha Zanzibar Lancaster House.

Karume ndiye aliyeshirikiana na Nyerere katika kuunda ASP na kuweka mipango yote ya mapinduzi endapo hawatafanikiwa kushika dola kupitia sanduku la kura.

Naamini umenielewa.
 
Chawa...
Ikiwa tutaacha kuieleza historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika tutakuwa tumefanya kosa kubwa sana.

Lazima historia hii isomeshwe kwa watu kila nafasi ikipatikana.
Kitabu Cha Abdul Sykes kilitoka 1998, Nyerere alifariki 1999,vipi,alipata kukisoma kitabu chako?..Kama alisema,taarifa ulizipataje kuwa kasoma!?.. reaction yake ilikuaje kwa mujibu wa duru za Siri?
 
Nimeelewa japo nina maswali kadhaa bado.

Una maana gani uliposema Karume alishirikiana na Nyerere kuunda mkakati wa mapinduzi ya Zanzibar hii ni ( kijeshi au kifedha,)kama ni kijeshi je jeshi la ndani uhusika wake ni upi(frontliners wa mapinduzi) kama ni fedha (fedha za kufadhili mapinduzi zilitoka upande gani TNG/ZN?

Je nani alitoa pendekezo la kumfuata John Okello Uganda ?

Je kwanini siku ya mapinduzi Karume alijifungia ndani , na kama mapinduzi yangefeli kulikuwapo na nafasi mbadala(back up) na je hii back up ilikuwa chini ya nani ?

Je sio Tanganyika wala Zanzibar hakukuwepo na wataalam kimedani kufanikisha mapinduzo sababu yaliwahusu watu wa karibu zaidi kuliko kwenda hadi Uganda?

Je ukweli ni upi hasa baada ya mapinduzi kutimuliwa kwa John Okello visiwani Zanzibar.?

Kwanini nguvu kubwa ilitumika kufifisha wanamapinduzi halisi wakiwemo John Okello na wenzie ,huku ikimpa Karume nafasi kubwa(ujiko) kuliko wahusika?

Nawasilisha .
 
Tayari unaamini kuwa Okello alikuwa kiongozi wa mapinduzi.

Tayari unaamini Karume "alijifungia ndani."

Okello amefuatwa Uganda.

Nk. nk. nk.
Wapi umepata haya?

Nilikuwa Pemba August mwaka huu kwa utafiti na nimefika hadi sehemu inayoitwa Mkanjuni nyumbani kwa Suleiman Mbaruk aliyekuwa Mudir wa Pemba yaani Area Commissioner kabla ya mapinduzi.

Huyu ndiye aliyempokea Okello na kumpa kazi na mahali pa kukaa.

Historia ya Okello na mapinduzi inaanzia hapa.

Lakini ukitaka kuijua historia ya mapinduzi soma kitabu cha Harith Ghassany, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).

Kitabu kinapatikana bure mtandaoni.
 
Kitabu Cha Abdul Sykes kilitoka 1998, Nyerere alifariki 1999,vipi,alipata kukisoma kitabu chako?..Kama alisema,taarifa ulizipataje kuwa kasoma!?.. reaction yake ilikuaje kwa mujibu wa duru za Siri?
In...
Kuna kitabu cha Ali Muhsin, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' (1997).
Ali Mushisn alimueleza Nyerere kwa namna ambayo haikuwahi kufanywa kabla.

Kitabu hiki kilipigwa marufuku kimya kimya kuingia Zanzibar lakini photo
copy ya kitabu iliweza kupenyezwa na kuwafikia baadhi ya watu.

Kila aliyekisoma alipata mshtuko wa aina yake na mmoja wa wasomaji
wa kitabu hiki alikuwa Prof. Haroub Othman.

Mara tu baada ya kutoka kitabu cha Ali Muhsin ndipo kikatoka kitabu
cha Abdul Sykes mwaka wa 1998.

Kama ilivyokuwa kwa kitabu cha Ali Muhsin, kitabu hiki nacho kilikuja
na mengine ambayo yalionekana kuwataabisha baadhi ya watu na
mmoja katika hao waliotaabika alikuwa Prof. Haroub Othman.

Hakuweza kustahamili ndipo alipofunga safari hadi nyumbani kwa
Mwalimu Nyerere, Msasani na kumuomba akijibu kitabu cha Ali Muhsin
Barwani na kitabu cha Mohamed Said kwani vikiachiwa bila majibu
vitaharibu ''legacy'' yake.

Mwalimu Nyerere alikuwa kasoma vitabu vyote viwili na jibu alilompa
Prof. Haroub ni kuwa yeye Haroub atengeneze kamati na yeye atakuja
kueleza yote ili wao waandike historia yake.

Kamati ilitengenezwa lakini hakuna kilichofanyika hadi Mwalimu Nyerere
alipofariki dunia mwaka 1999.
 
Taatizo lako ni UDINI
Lello...
Ningekuwa naandika mafunzo ya Uislam hapa nisingeshinda uandishi bora Jukwaa la Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Tatizo la udini unalo wewe kwa kuwa unataabika kuona Mohamed Said kaandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Historia hii ilifutwa kwa khiyana kwa sababu ilikuwa inaonyesha mchango mkubwa wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wewe kabla ya kusoma niandikayo ulipata kuwajua waasisi wa African Association 1929?

Ulipata kujua kuwa majority walikuwa Waislam?

Ulipata kujua kuwa Julius Nyerere safari ya kwanza UNO hafla ya kumuaga ilifanyika ndani ya jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika)?

Ulijua kuwa mkusanyaji fedha za safari alikuwa Iddi Faiz Mafongo Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

Ulipata kujua historia ya ukoo wa Sykes na uhusiano wake na harakati za kupambana na ukoloni?

Kuandika historia hii ndiyo udini?

Ulitaka Tanganyika isiwe na historia ya kweli?

Jitazame upya.

Naamini unajua baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes historia ya Julius Nyerere imebidi iandikwe upya na Mohamed Said alishirikishwa katika uandishi huo.
 
Chawa...
Ikiwa tutaacha kuieleza historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika tutakuwa tumefanya kosa kubwa sana.

Lazima historia hii isomeshwe kwa watu kila nafasi ikipatikana.
Watu hao wanaosema hivyo wewe umewaona wapi?
 
Mzee wangu, heshima mbele.

Hoja kuu ya watu ni kwamba baadhi ya chambuzi zako ziko upande mmoja (biased) hasa mrengo wa dini yako.

Sote ni mashahidi historia imepindishwa kweli sio tu Tanganyika bali hata Zanzibar , mfano mwepesi mimi siamini na hadi kesho sitokuja kuamini Karume ni mwanamapinduzi sababu waliokuwepo siku hiyo wanamtaja mwanamapinduzi halisi ilhali Karume alikuwa amejifungia chumbani tu.

Je tunafanyaje huyu mwanamapinduzi halisi apewe heshima yake hata kama alikuwa ni mgeni na wa dini ya tofauti na ile jamii aliyofanya mapinduzi.

Nawasilisha.
Yepi hayo? Tuwekee ushahidi.
 
Mzee Mohamed unajua mambo mengi na una kipaji kikubwa cha kuandika. Tatizo ni moja tu, UDINI. Kwenye maandishi yako huwa unakazana kuupigania uislamu na kuaminisha umma kwamba waislamu ndo walipigania uhuru. Umekuwa ukimpandisha Sykes na kumshusha Nyerere kana kwamba Nyerere alikuwa kama mtumishi wa wazee wa Kariakoo. Hutaki kukubali kuwa Nyerere alikuwa msomi mwenye akili nyingi kitu ambacho wazee wengi wa Kariakoo hawakuwa nacho. Ukiweza kuandika historia bila kuleta udini utakubalika na wengi. Kuwa fair hata kwa wakristo na watu wa dini nyingine waliohusika.
 
Mzee wangu, heshima mbele.

Hoja kuu ya watu ni kwamba baadhi ya chambuzi zako ziko upande mmoja (biased) hasa mrengo wa dini yako.

Sote ni mashahidi historia imepindishwa kweli sio tu Tanganyika bali hata Zanzibar , mfano mwepesi mimi siamini na hadi kesho sitokuja kuamini Karume ni mwanamapinduzi sababu waliokuwepo siku hiyo wanamtaja mwanamapinduzi halisi ilhali Karume alikuwa amejifungia chumbani tu.

Je tunafanyaje huyu mwanamapinduzi halisi apewe heshima yake hata kama alikuwa ni mgeni na wa dini ya tofauti na ile jamii aliyofanya mapinduzi.

Nawasilisha.
Okello
 
Back
Top Bottom