Wanasheria Mnisaidie, Kwanini hii Kesi ya Uhaini Haikufunguliwa Mahakama Kuu, ikaja Kufunguliwa Mahakama Ya Kisutu

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
7,885
Reaction score
18,636
Mahakama ya Kisutu ambayo haina uwezo wa kuisikiliza.
Mbona ni kama kupoteza muda na raslimali.

Na Tunaambiwa UHaini ni kosa kubwa sana.

Sasa Kwa nini Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Rekebisheni hapo, haya makosa makubwa yafunguliwe mahakama kuu moja kwa moja.
 
Tatizo la nchi yetu huwa wanamkamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi. Na mtuhumiwa akiwa magereza anapaswa kufikishwa mahakamani kila baada ya siku zisizozidi 14. Kwa hiyo njia inayotumiwa ni kufungua kesi katika mahakama ya chini ili tu mtuhumiwa awe anaonekana (appear) mahakamani. Upelelezi ukikamilishwa kesi inahamia Mahakama Kuu kwa kuanza kusikilizwa. Utaratibu huu pia hutumika kwa kesi za mauaji.
 
Mkuu pengine hiyo ni sababu ya chini ya carpet.

Kisheria utaratibu huu huitwa "committal proceedings" wenye lengo la kufanya "preliminary inquiry," ili kukubaliana kuhusu facts ambazo hazibishaniwi na kuacha zile zinazonishaniwa, kukubaliana kuhusu mambo mengine kama mashahidi, nyaraka n.k.

Katika hatua hi ya Committal proceedings mtuhumiwa hatakiwi kutake plea yaani kujibu shtaka maana kimsingi mahakama Haina jurisdiction ya kusikiliza shauri lake.

Msingi wa committal (in principal and theory) ni kupeleka mashauri haraka. Lakini Kwa maoni yangu Kwa TZ Committal imekua chaka la kupoteza muda. Na hii ndio shida ya copy and paste ya Sheria za nje.

Turudi kwenye committal, baada ya mahakama ya hakimu mkazi kumaliza Preliminary inquiry, itamcommit mtuhumiwa High court yenye jurisdiction (kumcommit ni kama kumtuma/kumpeleka).

Huko high court mtuhumiwa atasomewa INFORMATION, kosa rasmi na atatake plea na kesi itaendelea Kwa mambo yanayobishaniwa.

P.s. Nimechanganya lugha maana hii procedure naielewa zaidi in English. Kumbuka Sheria zetu zipo Kwa English.

Nakubaliana na mtoa COMMENT waendesha mashtaka in practice hutumia hii procedure kupoteza muda wakati lengo la msingi ilikua kusave muda.

Kingine SHERIA hairuhusu kumkamata mtu ikiwa upelelezi haujakamilika. Lakini TZ imekua kawaida watu kusota rumande Kwa maelezo upelelezi haujakamilika. Na mahakama zimeshindwa kusimamia hili.
 
Kwani haiwezi pigwa tarehe ikiwa mahakama kuua?
 
Inawezekana. Lakini pamoja na mambo mengine Committal husaidia mahakama kuu kushungulika na mambo ya msingi tu. Pia hutoa muda Kwa mtuhumiwa na waendesha mashtaka kuandaa kesi zao vizuri. Ili wakifika mahakama kuu shauri liishe haraka. Kuna uwezekano pia wa case kuisha kwenye committal hata kabla ya kufika mahakama kuu.
 
Mkuu pengine hiyo ni sababu ya chini ya carpet.

Kisheria utaratibu huu huitwa "committal proceedings" wenye lengo la kufanya "preliminary inquiry," ili kukubaliana kuhusu facts ambazo hazibishaniwi na kuacha zile zinazonishaniwa, kukubaliana kuhusu mambo mengine kama mashahidi, nyaraka n.k.

Katika hatua hi ya Committal proceedings mtuhumiwa hatakiwi kutake plea yaani kujibu shtaka maana kimsingi mahakama Haina jurisdiction ya kusikiliza shauri lake.

Msingi wa committal (in principal and theory) ni kupeleka mashauri haraka. Lakini Kwa maoni yangu Kwa TZ Committal imekua chaka la kupoteza muda. Na hii ndio shida ya copy and paste ya Sheria za nje.

Turudi kwenye committal, baada ya mahakama ya hakimu mkazi kumaliza Preliminary inquiry, itamcommit mtuhumiwa High court yenye jurisdiction (kumcommit ni kama kumtuma/kumpeleka).

Huko high court mtuhumiwa atasomewa INFORMATION, kosa rasmi na atatake plea na kesi itaendelea Kwa mambo yanayobishaniwa.

P.s. Nimechanganya lugha maana hii procedure naielewa zaidi in English. Kumbuka Sheria zetu zipo Kwa English.

Nakubaliana na mtoa COMMENT waendesha mashtaka in practice hutumia hii procedure kupoteza muda wakati lengo la msingi ilikua kusave muda.

Kingine SHERIA hairuhusu kumkamata mtu ikiwa upelelezi haujakamilika. Lakini TZ imekua kawaida watu kusota rumande Kwa maelezo upelelezi haujakamilika. Na mahakama zimeshindwa kusimamia hili.
Shukran Sana mkuu Kwa ufafanuzi
 
Mahakama ya Kisutu ambayo haina uwezo wa kuisikiliza.
Mbona ni kama kupoteza muda na raslimali.

Na Tunaambiwa UHaini ni kosa kubwa sana.

Sasa Kwa nini Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Rekebisheni hapo, haya makosa makubwa yafunguliwe mahakama kuu moja kwa moja.
Mimi naona tu wanawapotezea muda chadema ili uchaguzi usiwe na upinzani mkubwa.. wanabuy timè hadi mwezi September huko ataachiwa then chadema watashindwa hata kufanya maandalizi ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom