Ukimpeleka mahakamani nae atatoa maelezo yake, akishindwa kujitetea anahukumiwa Kama wezi wengine. Masuala yakusema hoooo afungwe miezi sita hayakuhusu, mahakama inaweza kumpiga mvua 4 au 8 huwezi kuipangia mahakama adhabu.
Kitendo Cha kusema arudishe pesa na afungwe miezi 6 inaonesha bado unahuruma dhidi yake hivyo muache na maisha yake. Kwasababu mpaka Sasa hiyo pesa Hana iliyokamilika, ameshapunguza nauli na kujipanga kimaisha kabla hajaanza biashara zake. Ukimpeleka mahakamani ndugu waliokushauri umsamehe ndio watakao muwekea dhamana, hivyo utaweka ufa kwenye familia.
Huyo mtoto hatujapata maelezo yake huenda akisimulia alivyopambana hapo nyumbani tunaweza kuona hata alichochukua ni kidogo.
Hata ukifungua kesi mahakamani watawaomba mkakae kifamilia Kwanza muyamalize na mzee ukizingua kwenye vikao vya kifamilia, adhabu anapunguziwa yaani atahukumiwa kwenda jera miezi minne bila ghalama au alipe faini ya elfu 50. Yaani hata mia hupati na dogo analipa faini na kesi inakua imeisha.
Nawachukia watoto wasio na adabu lakini siwapendi wazee mabahili Kama wewe.