Wanasheria na wanaharakati badilisheni hili, halina faida kwa nchi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Mtu amempa mimba msichana chini ya umri wa miaka 18 anafungwa miaka 30! Huyu ameua mtu anasamehewa kunyongwa kisa, haki za binaadamu.

Nirudi kwa aliyempa mimba msichana, msichana akisha zaa mtoto atabaki na mama yake huku baba hata muona huenda kabisa kwani miaka 30 mama na baba yake watapotezana.

Huyu mama mtoto asipokuwa na uwezo wa kumtunza mtoto mtoto atapitia maisha yasiyo na mbele yenye neema huenda akaishia kutupwa jalalani au kukimbiwa na mama yake huku hakuna msaada toka serikalini.

Hivyo mama na mtoto hawafaidiki na hukumu, mahakama kazi yake ni kuhukumu bila kujali maisha ya baadae ya mama na mtoto huku serikali nayo haifaidiki zaidi ya kugharamiwa akiwa kifungoni, WHOSE FUTURE IS IT ANYWAY.
 
Umesema vema mkuu, yaani ni kutuongezea gharama ya kuwalea wakiwa gerezani huku watoto waluozaliwa wanazurula mitaani nankuhutaji msaada. MI nashauri serikali kuwa hukumu iwe kiungo cha nje na kuhakikisha kuwa analea mtoto na kusomesha mama mtoto mpaka afike mwisho. Kuwajaza gerezani hakumsaidii mtoto wala mama...
 
Umeona mbali sana ,huyo mtoto atakuwa kashanyimwa haki ya kuwa na wazazi wote kwa wakati husika ...

Ndio maana tukasema hata awe na miaka 14 kama walipeana mimba badala ya kufungwa basi waoane tu ,kama ujinga ulishafanyika kwa wazazi sasa tuangalie future ya mtoto ili apate malezi mazuri maana jambo lishatokea.
 
Kwa akili na hoja yako hapa unamaanisha pia, mtu akiua au akiiba asifungwe kwakuwa kuna watu nyuma yake wanamtegemea na pia ni hasara kwa taifa?

Mhalifu asipewe adhabu kwakuwa akipewa kuna watu wengine watadhurika na adhabu yake, si ndio?
 
Umesema vema mkuu, yaani ni kutuongezea gharama ya kuwalea wakiwa gerezani huku watoto waluozaliwa wanazurula mitaani nankuhutaji msaada. MI nashauri serikali kuwa hukumu iwe kiungo cha nje na kuhakikisha kuwa analea mtoto na kusomesha mama mtoto mpaka afike mwisho. Kuwajaza gerezani hakumsaidii mtoto wala mama...
You are genius,nakubaliana na wew tena atoe report na ya maendeleo pindi anaporeport kituoni na haijalishi hata kama msichana akiamua kutokuwa na yeye kimapenzi aendelee kusomesha na kumhudumia mtoto
 
Kwa akili na hoja yako hapa unamaanisha pia, mtu akiua au akiiba asifungwe kwakuwa kuna watu nyuma yake wanamtegemea na pia ni hasara kwa taifa?

Mhalifu asipewe adhabu kwakuwa akipewa kuna watu wengine watadhurika na adhabu yake, si ndio?
Wewe ulitakiwa ujadili hoja iliyopo, inahusiana na uzazi, kuua kitu kingine, mtoa hoja sijaona sehemu alipoandika adhabu isitolewe.

Hao wanauwa wenyewe, wanatetewa wasinyongwe, nini wazazi wasitetewe, Adhabu ni kali, inafana na mtu mwenye kosa la ujambazi.
 
Hoja iliyopo hapa sio uzazi, ni adhabu ya kosa lililopelekea uzazi.

Kuua ni kitu kingine? Kuua na kubaka yote ni makosa, tofauti ni uzito katika adhabu.
 
“Acha ukito***bi kwa watoto wa shule kuna jela” hiyo ndio quote ya muhimu ya hao unaowaacha watishije isikusumbue sana kichwa
 
Kwa akili na hoja yako hapa unamaanisha pia, mtu akiua au akiiba asifungwe kwakuwa kuna watu nyuma yake wanamtegemea na pia ni hasara kwa taifa?

Mhalifu asipewe adhabu kwakuwa akipewa kuna watu wengine watadhurika na adhabu yake, si ndio?
Anayeua amepunguziwa adhabu kwa kuangalia haki ya binaadamu kuishi japo imesahau haki ya marehemu kuishi, huyu mtoto atakayezaliwa ananyimwa haki ya kulelewa na wazazi wake wawili! Kati ya muuaji na mtoto anayeadhibiwa ni mtoto asiye na hatia, hivyo iko haja ya kuwa na adhabu mmbadala ambayo haitamharibia maisha mtoto.
 
Una hoja ila kuna vitu hujaviangalia.

Hiyo nadharia yako inaweza kufanya kazi endapo intention ya mtuhumiwa ilikua njema. Yani alikua ana mpango wa kuanzisha familia na huyo binti ila it just wasn't a right time!

Lakini What if, huyo kijana anayefanya tukio ni mhuni? Hakua na mpango wa kuanzisha familia na huyo binti? Alitaka apige tu apite hivi (alimlaghai)? Au alimlazimisha (rape) / Kumkomoa n.k.?

Sheria ipo kwamba huruhusiwi kushiriki tendo na mwanafunzi (U18) na ukifanya hivyo ni jela 30 yrs. Hili sheria imeimbwa sana and still mtu anajiamulia kuivunja. Unategemea mahakama ishughulike naye vipi? Mahakama do what Mahakama does, full stop.

Na umeangalia upande mmoja wa damage, mtoto. How about wazazi/ndugu wa mwanafunzi anayepewa mimba? Unadhani kila Familia inaridhia mtoto wao aolewe kirahisi hivyo? Kwamba apewe mimba uchochoroni kinyume na sheria halafu wakae meza moja na mhalifu wao wayajenge? Come on, Bro!

Ukijaribu kugusa angle zote, utaona bora kama ingekua inawezekana, huo mbadala wa kifungo kilichowekwa kisheria, uamuliwe na victims. Wahanga ndio wapewe nafasi ya kumhurumia mtuhumiwa wao as they see fit. Na wakiona bora aozee jela na iwe hivyo!
 
Hiyo adhabu haina ushahidi kuwa imeondoa tatizo zaidi ya tatizo kusukumiwa mtoto asiye na hatia na ni chanzo cha kuzalisha watoto wa mitaani na panyarodi.
 
Una hoja ila kuna vitu hujaviangalia.

Hiyo nadharia yako inaweza kufanya kazi endapo intention ya mtuhumiwa ilikua njema. Yani alikua ana mpango wa kuanzisha familia na huyo binti ila it just wasn't a right time!

Lakini What if, huyo kijana anayefanya tukio ni mhuni? Hakua na mpango wa kuanzisha familia na huyo binti? Alitaka apige tu apite hivi (alimlaghai)? Au alimlazimisha (rape) / Kumkomoa n.k.?

Sheria ipo kwamba huruhusiwi kushiriki tendo na mwanafunzi (U18) na ukifanya hivyo ni jela 30 yrs. Hili sheria imeimbwa sana and still mtu anajiamulia kuivunja. Unategemea mahakama ishughulike naye vipi? Mahakama do what Mahakama does, full stop.

Na umeangalia upande mmoja wa damage, mtoto. How about wazazi/ndugu wa mwanafunzi anayepewa mimba? Unadhani kila Familia inaridhia mtoto wao aolewe kirahisi hivyo? Kwamba apewe mimba uchochoroni kinyume na sheria halafu wakae meza moja na mhalifu wao wayajenge? Come on, Bro!

Ukijaribu kugusa angle zote, utaona bora kama ingekua inawezekana, huo mbadala wa kifungo kilichowekwa kisheria, uamuliwe na victims. Wahanga ndio wapewe nafasi ya kumhurumia mtuhumiwa wao as they see fit. Na wakiona bora aozee jela na iwe hivyo!
Mada yangu hailengi adhabu kwa mtuhumiwa inalenga adhabu kuhamishiwa kwa mtoto, bahati mbaya ujuaji wa Mods umebadili lengo langu la "WHOSE FUTURE IS IT ANYWAY".
Mtuhumiwa aadhibiwe kwa alichotenda lakini adhabu iangalie malezi ya mtoto ambaye ndiye ataadhibiwa kuliko mtuhumiwa.
 
Wewe ulitakiwa ujadili hoja iliyopo, inahusiana na uzazi, kuua kitu kingine, mtoa hoja sijaona sehemu alipoandika adhabu isitolewe.

Hao wanauwa wenyewe, wanatetewa wasinyongwe, nini wazazi wasitetewe, Adhabu ni kali, inafana na mtu mwenye kosa la ujambazi.
Acha waozee jela hao wabakaji wa watoto
 
Nikwambie tu mimi mpaka sasa Kuna mtoto wa Form 2 namuelewa kinyama ila simuingii kwasababu ya hizo sheria Kama ndio zitawekwa Kama unavyosema mimi leoleo hapa nikifika home nayongoza huyu na kumgonga.

Kwa unachosema wewe ni kipi Sasa kitamzuia mtu kufanya Mapenzi na mwanafunzi personally nimejizuia na wanafunzi wengi mpaka Sasa mpaka wengine walinitongoza wewnyewe sheria ingekuwa Kama unavyosema wewe nisingeacha hata mmoja niogope nini Sasa.
 
Unajua kujihusisha na Binti chini ya miaka 18 tafsi yake umebaka?
Hicho unachosema siyo hoja ya Post hii, soma vizuri uelewe. Kwenye Post hii hakuna sehemu yoyote isemayo adhabu isitolewe kwa mtuhumiwa, anzia hapo.
 
Kwaiyo mtu aliyebaka unataka apewe adhabu gani?
 
Back
Top Bottom