Una hoja ila kuna vitu hujaviangalia.
Hiyo nadharia yako inaweza kufanya kazi endapo intention ya mtuhumiwa ilikua njema. Yani alikua ana mpango wa kuanzisha familia na huyo binti ila it just wasn't a right time!
Lakini What if, huyo kijana anayefanya tukio ni mhuni? Hakua na mpango wa kuanzisha familia na huyo binti? Alitaka apige tu apite hivi (alimlaghai)? Au alimlazimisha (rape) / Kumkomoa n.k.?
Sheria ipo kwamba huruhusiwi kushiriki tendo na mwanafunzi (U18) na ukifanya hivyo ni jela 30 yrs. Hili sheria imeimbwa sana and still mtu anajiamulia kuivunja. Unategemea mahakama ishughulike naye vipi? Mahakama do what Mahakama does, full stop.
Na umeangalia upande mmoja wa damage, mtoto. How about wazazi/ndugu wa mwanafunzi anayepewa mimba? Unadhani kila Familia inaridhia mtoto wao aolewe kirahisi hivyo? Kwamba apewe mimba uchochoroni kinyume na sheria halafu wakae meza moja na mhalifu wao wayajenge? Come on, Bro!
Ukijaribu kugusa angle zote, utaona bora kama ingekua inawezekana, huo mbadala wa kifungo kilichowekwa kisheria, uamuliwe na victims. Wahanga ndio wapewe nafasi ya kumhurumia mtuhumiwa wao as they see fit. Na wakiona bora aozee jela na iwe hivyo!