Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomhusu mhe. Mbowe na wenzake watatu unatia mashaka, tangu mwanzo wa kesi upande wa mashitaka umekua na visingizio vingi vya ugonjwa vinavyowahusu mashahidi, hawa mashahidi 24 wenye maradhi dhidi ya washitakiwa 4 wenye afya imekua kama mchezo wa kuigiza.
Nia hasa ya upande wa mashitaka kufanya njama hizi inaanza kuonekana kama kuwakomoa washitakiwa ambao hawana haki sawa ya kusikilizwa na mahakama kama waliyonayo upande wa mashitaka, ni wazi washitakiwa wangefanya kama wafanyavyo upande wa mashitaka wangekwisha onywa na mahakama.
Wanasheria, TLS na wanaharakati pazeni sauti zenu mbadili mwenendo huu wa kesi wenye mashaka ili haki itendeke na mawakiri wa utetezi wapunguziwe mateso ya kupoteza muda wa kuwatetea washitakiwa.