Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Ndugu, hapa duniani chini ya jua, kila kitu kinaweza kuhojiwa hata kama kimewekwa kwenye sheria kwamba hakiwezi kuhojiwa...
Kumbuka, kinachohojiwa si mshindi bali utaratibu mbovu uliopelekea ushindi...
NEC Wakimtangaza mshindi, kitakacho hojia si mshindi bali process nzima, hii ikifanyika, hata ushindi pia utakuw nullified.

utaratibu ukiwa mbovu, kwa mfano una au ume breach- principles of natural justice, right to fair hearing, equal treatment, transparency na mlolongo wote huo... basi uchaguzi mzima utakuwa batili...

kinacho natakiwa kufanywa na wadau ni kuifungulia kesi NEC na ku- prove kwamba ime breach fundamental freedoms, rights and responsibilities.. Hii ikifanyika maana yake ni kwamba NEC Hawatakuwa na uwezo kwa kuendelea na mchakoto wao wa uchaguzi kwa maana watakuwa hawana legitimacy ya kumtangaza mgombea kwa kwa kuwa process nzima ilikiuka rules of natural justice, breached fundamental rights na pia freedoms to free and fair election... Ubatili huo ukiwa proved, basi hata kile walicho kitangaza hakitakuwa na maana kisheria...

Angalizo:

NEC chondechonde: Watanzania tumeamuka toka usingizini, na nunajua ni nini kinachoendela....
tafadhalini saana ndugu zetu NEC, wapeni vyama vyote haki sawa, vinginevyo ni majibishano na vurugu mechi zisizo na maana na sintofahamu nyingi...

Judge Kaijage, najua unasoma humu: Wewe wajua kwamba United nation security council ni supreme kila kona duniani humu, lakini maamuzi yao huwa hupingwa na hata mahakama katika regional bodies... kumbuka kesi ya Kadi -- kadi case (1 and 2, academic summary yake inapatikana hapa:
kadi 1: Kadi v. Council and Commission - Case Brief for Law Students | Casebriefs
kadi 2: Kadi Case – Constitutional Core Values and International Law – Finding the Balance? )
Usiipeleke nchi katika sintofahamu kwa kuwa mtaalam wa kutafsifi sheria.. kazi hiyo ulisha istaafu na sasa uko pembeni bench; wale ulio waacha ndio wenye kazi hiyo...

Chonde chonde Kaijage...
 
"Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais" (Pascal Mayalla, 2020).

Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka.

Askofu Bagonza alijibu vizuri sana hoja ya uanaharakati na uongozi. It is just a head and tail on a same coin!
 
Mkuu sijasoma Uzi mzima,Ila Tanzania ingekuwa na vyombo huru na taasisi imara,sidhani Kama Magu angetakiwa hata kuchukua form maana ananuka jinai Kila sehemu ya mwili wake, ila kwa kuwa serikali ya Tanzania imeporwa kutoka kwa watanzania na kumilikishwa kwa ccm,acha Mpinzani yeyote wa hawa waroho na walevi wa madaraka ccm apewe hizo jinai zenu
 

Pascal sio kwamba umeileta hii hoja kwa bahati mbaya, ila umeileta kwa madhumuni kamili baada ya kuona kinachoendelea kwenye mizunguko ya Lisu. Na sehemu kubwa umeongozwa na wivu wa kisiasa, maana unajua fika Magufuli hana uwezo wa siasa za ushindani, na hatakaa aziweze. Hivyo hii post yako imekuja kuweka uamuzi ambao tayari Magufuli anao. Lakini kwa hiki kinachoendelea kwa muda huu mfupi, sio wewe, sio Magufuli sio wanaccm, wote mmejua kuwa watu wengi hawaipendi ccm, na hakuna uwezekano wowote wa wananchi wa nchi hii kukubali kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi kwa ridhaa yao.
 
Wakuu,hivi yule aliye mtafutia mama yake mme,yule aliyemwambia DAs wa kisarawe akagombee wanaume na DC ofisini,yule aliyewauliza wananchi wa huko Kanda ya Kati wanataka kupanuliwa wapi,anacheo gani nchi hii,Mimi ni nimezaliwa Leo wakuu naombeni msaada
 
Wewe ni CCM. Kwa kuwa ni CCM tena yulw uliyefanya vibaya na wajumbe,basi hii hoja yako haina mashiko hata kidogo.

Chochote ulichoandika ni kujipendekeza kwa jiwe tu hasikusahau kwenye teuzi zako. Acha njaaa ndugu yangu.
 
Aliwahi kusema anatishiwa vyombo vya usalama vikadharau kilichotokea tunakifahamu. Sasa wewe ni nani useme hatishiwi wakati kila siku akina Musiba wanasema hadharani kabisa na hawaulizwi chochote. Hii nchi bwana
Hivi hakuna wananchi wenye uwezo wa kujichukulia Sheria mkononi na kumpa msiba haki yake?yaani hata kumsingizingia mwizi tu kujustify kupigwa kiberiti watu imewashinda?
 
Background
Wewe ni kaka Ake TL
Wewe ndie ulimshauri agombee urais
Haaa haaa kwahyo ulimshauri ili aje kuenguliwa mbona hujamshauri aende akagombee ubunge?
Why hujamshauri atulie amalize kwanza kesi zake mahakamani?
 
Nina mawili kwako comrade. Not a legal perspective but simply logical:

1. Ushauri kwako binafsi for your own well being:
Huu uzi wako umedhamiria kuwachochea wapinzani na usijeshangaa kuwa unaweza kuwa qualified huko baadaye na ICC kama "instigation to trigger partsan-driven hate and violence". Kwa hiyo usione ajabu kwa wewe kujikuta u miongoni mwa watakaoburuzwa ICC when sh..t hits the fan!

2. Matumizi ya lugha yenye staha kwa presidential candidate:
Hapa chini nime-quote jinsi ulivyomshambulia Tundu Lissu kwa kauli zake ulizoziita hazifai kwa mtu anayewania urais. Lakini inaonekana umejisahaulisha kidogo kuhusu kauli zinazotolewa na JPM huku akiwa rais ambazo actually nyingi ni worse kuliko za Lissu ambaye hata siyo rais. So, ushauri huu au hili karipio lako ungelielekeza kwa mwenyekiti wa chama chetu CCM kwanza kabla hujaanza kuwashambulia kina Lissu. Ondoa boriti lililoko ndani ya jicho lako badala ya kung'ang'ania kuondoa kibanzi kilichomo ndani ya jicho la mwingine.


Ni hayo tu, comrade!
 
Pascal mayala Ni mwandishi wa habari na Ni mwanachama wa CCM. Sijajua miiko ya kazi yenu ipoje ya uandishi wa habari na kazi za siasa hasa kudeclare wewe Ni mwanachama wa chama Fulani.

TAALUMA zetu zisaidie kuijenga Tanzania yetu. Vyama sio Taifa
 
Kutuhumiwa sio kosa na jinai ni pale tu unapotiwa hatiani.

Iweje sasa ulete mamneno mfu ya mke wa Kaisari?

Zama zile busara ya mfalme ilikuwa inatawala na hatupo tena huko, vingine kila mja akituhumiwa tu nje ya ulingo.

Every body will remain innocent till when will be found GUILTY and Convicted by the LAW (Court)..
 
Leo umedhalilika na ndio tatizo la nchi hii. Haki haitendwi wala kuonekana inatendwa.

Mahakama ndio chombo pekee cha kumtia mtu hatiania. Kabla ya hapo presumption ya innocence ndio kiongozi!! Kwa kuwa mpaka anachukua form na kabla ya kupitisha wagombea - mahakama ilikuwa haijamtia hatiani, hakuna jambo linaweza kufanywa kwa kufikirika tu.

Unataka aondolewe kuhombea halafu mahakama imuachie baadae na wakti huo akose kugombea kwa sababu uchaguzi umepita?? Ni vipi akaachiwa anagombea na hata akishinda atolewe kwa mujibu wa sheria??

Katiba imeainisha aina ya makosa yanayoweza kumnyima sifa mgombea. Nayo yanahusiana na uhaini na kodi. Au kama aliwahi kuadhibiwa kwa kifungo zaidi ya miezi 6. Katiba haitaji mtu spotless - usitengeneze sheria as you go along.

Kwa mawazo haya - hamtaki ushindani. Mnataka Rais aliyepita bila kupingwa???
 
ila dunia bwana!,yaani unapigwa ma risasi,mungu anakuokoa,unapona,unarudi nyumbani unazabwa mi KESI,jamani haya Mambo Yana warahisishia wananchi kujua na Kuona kwamba haki hamna na kukosa imani na serikali yao,Yani ukiwa na mtazamo tofauti ni NONGWA!
 
Sasa Paskali unaenda mbele na kurudi nyuma? Kwamba wewe ndio ulimshauri agombee urais halafu unakuja tena kuleta hoja za kuenguliwa kwake. Hujioni kama ni mnafiki fulani hivi mahiri ambaye unataka kuwa Mr. Nice upendwe na kila mtu?

Declaration yako kuwa "kwa sasa ni kada wa ccm", inalenga nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…