Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Lissu mwenyewe Gwiji la Sheria hivyo Hata hao Majaji wanaojaribu kutumia vifungu vya Sheria nk.wanaangalia na mtu wa kumuwekea figisu figisu,Chadema mwaka huu wamejipa Hadhi ya kipekee, Mgombea anachambua sera mpaka unasisimkwa, 2015 tulipoteza kwa Lowassa hatupotezi tena.
 
Yaan anachanganya mambo huyu mzee Pascal, Ni bora angesema yeye ni mwanaCCM na angependa Tundu Lissu aondolewe tu ..!!
Et sijui kuingilia uhuru wa mahakama, tume iamue kumuondoa, sasa huko si ndo kuingilia mahakama ..!! Sijui kwanin wanajikomba kupita kiasi
 
Nitashangaa sana kama Lissu hataenguliwa na NEC kwa kigezo cha kuwa na kesi mahakamani. Najiuliza tu kwenye fomu zake za kugombea uraisi atajaza nini kwenye kipengere kinachohusu kuwahi kushitakiwa na kuwa na kesi mahakamani.
 
Huu uzi unachochea chuki kwenye jamii. Ni uzi uliojaa nia ovu.

Paskali lazima aje na uzi wa hivi, kwanza unamfanya aonekane mwanaccm, na hivyo kumsogeza kwenye meza ya uteuzi. Pia ni kama sehemu ya kujibu mashambulizi, kwani anashambuliwa sana na wapinzani huku jukwaani. Jana uliletwa uzi wa kumnanga kuwa kafulia baada ya kupigwa spana na wajumbe. Hivyo hapa na yeye kuamua kumwaga ugali, kwani sasa hivi hili jukwaa kwake limegeuka shubiri, na wanaomnyima raha ni wapinzani.

Asichojua Paskali ni kuwa hapa tulipofikia hatuogipi tena hujuma za watawala, maana tunajua wamechoka kushindana. Toka Magufuli aingie madarakani chaguzi zote zimekuwa zikinajisiwa kwa maagizo ya huyo anayejipendekeza kwake ili ampe ulaji, na alikuwa kimya bila kuleta huu ushauri wake uchwara. Hivyo hahitaji kujificha kwenye vifungu vya kisheria, kwani hata yeye ni mwanasheria. Yeye atoke na kusema anataka Tundu Lisu aenguliwe kwa vifungu kadhaa, maana anajua fika Magufuli hawezi kushindana na Lisu, hivyo amtetee atakayeweza kumpa ulaji. Paskali hana uzalendo wowote, bali ni mtu aliyeshuka daraja, huku umri ukiwa umetupa mkono.

Cc: Paskali Mayalla
 
Kesi zote za Mahakamani hazimzuii Kuwa Rais wa JMT. Ambacho watu wengi hwakijui ni Kwamba Lissu mwenye ni Mwanasheria Mashuhuri, Hawezi endelea kupoteza muda wake wakati anajua fika kesi zake zitamzuia.Hivyo hivyo CCM walidai Lissu angeweza kukosa kuchukua Fomu za kugombea Urais 8/8/ Kwa sababu ilikua ni siku kuu ya Wakulima kitaifa na Ofisi za Tume zingekua Zimefungwa.Lakini Lissu alichukua Fomu za Kugombea nafasi ya juu katika Nchi siku hiyo kwa sababu Lissu alikua na Taarifa kuhusu Ofisi ya Tume.Hivyo Lissu anayajua yote hayo ndio maana anajiamini kuliko wenye Mamlaka.
Nitashangaa sana kama Lissu hataenguliwa na NEC kwa kigezo cha kuwa na kesi mahakamani. Najiuliza tu kwenye fomu zake za kugombea uraisi atajaza nini kwenye kipengere kinachohusu kuwahi kushitakiwa na kuwa na kesi mahakamani.
 
Hahaaa mtu mzima hovyo tena hovyo watu kama nyie mshafeli maisha mnategemea ccm iwainue dah hata mnayemsifia ana kaz sana ndio maana anawateua upinzani.
 
Ok tuvute subira, tutapata majibu muda si mrefu.
 
Mkuu. Ukweli tunajua kabisa Lisu ni comedian tu.
Hana pumzi hata ya kumsogelea tu JPM. Ila tumeshajipanga na makelele. kwa sababu mabeberu watatuelewaje tukikaa kimya?
 
Paskalli analifahamu hili akiwa kama mwanasheria na mwandishi sasa jiulize kipi kimemkumba hadi kuandika alicho andika. Ni juzi juzi tu kwenye uzi wake mmoja alituambia yeye hana chama na mara ghafla bin vuu huyo anapambana na wajumbe. Tumemuuliza kadi ya CCM kaipata lini hadi kesho hajajibu.
Ni wazi jamaa anataka Tundu Lissu aenguliwe hata kama anaremba vipi. Si wakumuamini tena kwani tunajua anasimamia wapi. Ana conflict of interest ambayo inaondoa credibility yake na sasa iko wazi. AENDE TU akifanyie kazi CCM na si kujifanya mchambuzi huru kwenye forum kama hii.
 
JF sasa inamtambua Paskalli wa kweli ni nani. Alifanya uanachama wake wa CCM kuwa siri na sasa si siri tena. Bahati mbaya anajifanya kupuliza huku akiuma. Hana nia nzuri na Lissu FULLSTOP. Katika hili amejivuruga mwenyewe. Tungekuwa na kura ya kupoteza imani (Vote of no confidence) kura yangu ingemkataa.
 
Kwa sasa anafosi kingi. Ameamua kuomba nafasi kwa sauti ya juu maana hakuna anayemuona tangu alipoambiwa Mayala kwa Kisukuma maana yake ni njaa [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]. Sonona ya mama yake Kabendera haitamuacha salama.
 
Pole sana mayala ..ulitabiri lissu hawezi rudi lkn ikawa kinyume chake ..lissu ndo rais wa JMT ameandaliwa hvyo mpende msipende hbr ndo hyo ...na mnasubiriwa kwa hamu mumuengue ndo mtaipata fresh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…