Wanasheria wa CCM sasa ni wakati wa kuwashitaki watu wanachafua haiba ya chama chenu

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Imekuwa kawaida sasa wanasiasa wa upinzani hasa CHADEMA wakikamatwa na polisi kwa makosa wanaihusisha CCM na kukamatwa kwao. Naona ipo haja ya kuwapeleka hawa watu mahakamani ili wathibitishe maneno na madai yao ili waone kuwa nchi hii inaendeshwa kwa sheria
 
Utii bila shurti ni muhimu sana
 
Yaani hao unawaambia wanakuona zwazwa 😄😄😄😄
 
Kwa maana ile ile ya kuwanyamazisha bila kujali uhuru wa maoni,ila pia ni pale mkiwa angalao na aliyemwadilifu na aendeshe kesi yenyewe kwa uadilifu .
 
Chizi sio mpaka aokote makopo. Badala uwe chawa mwenye akili unakuwa kupe mng'ang'anizi , wewe sio mwana ccm mwenzangu ningekujibu ila ni mwanafisiemu
 
Kama wewe unaweza kuwaleleka mahakamani bila ushahidi fanya hivyo, polisi wanakamata kwa kutumwa ila wanakwama kwenye kufungua kosa, inabidi wawaachie.
 
Tuanze na Rostam Azizi, baada ya hapo tufuatilie ya maagizo kutoka juu, hapo juu ni wapi na kuna nani na ana wadhifa gani kwenye chama cha CCM. Tukigundua hili nafikiri tutakuwa tumetibu ugonjwa huu wa kamata kamata ya viongozi na wanachama wa upinzani
 
Kama ni hivyo basi mbona itakuwa rahisi kabisa; wewe haribu haiba yao, wakupeleke mahakamani kwenye hizo unazosema ni mahakama fata maagizo halafu uone kama utapona
 
chama chenu mmekichafua ninyi wenyewe, na kimechafuka kwelikweli na hakitakuja kusafishikwa kwa chochote. ni cha kutupa tu kwenye jalala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…