mzee Mengi anahisi serikali inwakingia kifua mafisadi na inawasaidia kuwakandamiza wanaopinga ufisadi. Mh!, tusubiri....
, sio anahisi, bali anajua wazi ndio maana anachokifanya sio kuwashitaki mafisadi kwa wananchi, bali kuwashitaki kwa wananchi, hawa wanaowakingia kifua mafisadi hata kama kwa kauli anadai anamsaidia mkulu, infact ndio anamzamisha.
kwa upande wangu, sitishwi na wanaopigishana kelele, Mangi na Manji, bali natishwa na wanaokaa kimya kama ma 'don' wa mafia.
Pia kusema ukweli, mzee Mengi ni mtu mwenye inferiority complex ya ajabu, hivyo kitendo cha kuvurumishiwa makombora ya jana, kimemprovoke, atajibu kwa ukali, kwa hasira na anaweza kujikuta pia anatema na utumbo.
Kwa ushauri wangu wa bure, Mzee wetu Mengi ushauri, asiendelee kujibizana na mafisadi papa ili kuilinda heshima yake.
Kitendo pekee cha kuwataja kwa majina ni japo kinyume cha sheria, ni cha ushujaa wa ajabu kumfanya awe shujaa wa taifa, sasa asiuharibu huo ushujaa kwa kuipiga zaidi hii ngoma yake, mwishowe itampasukia.