Wanasheria wetu ni uchwara? Kutuuliza sisi tusiokuwa na taaluma ya sheria ni kutuchochea tu.

Wanasheria wetu ni uchwara? Kutuuliza sisi tusiokuwa na taaluma ya sheria ni kutuchochea tu.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Wakili anatoka kwenye chumba cha mahakama ambako kesi fulani bado inaendelea kusikilizwa. Baada ya kesi kuahirishwa wakili huyo msomi anatoka nje kidogo tu ya jengo la mahakama na kukusanya vyombo vya habari vya ndani na nje pamoja na kundi la wananchi ambao pia walikuwepo ndani ya ukumbi wa mahakama kufuatilia kesi hiyo na kuanza kusema mtuhumiwa hana kosa, Jaji hakutenda haki, kesi ifutwe mara moja na mtuhumiwa aachiwe bila mahariti.

Hata sisi tusiojua sheria na taratibu za kesi tunaona kabisa hii sio sawa. Jamaa anatuambia sisi raia mwenendo wa kesi ili tufanye nini? Kwanini kesi inaendelea na hukumu bado kutolewa lakini yeye anatuambia mtuhumiwa hana kesi, Jaji ana makosa na mtuhumiwa aachiwe bila mashariti? Maana yake anatuaandaa sisi tujue mtuhumiwa anaonewa, mahakama haina weledi hivyo tufanye fujo kama mahakama itamtia hatiani mtuhumiwa. Huu ni uchochezi kwakweli, lazima upigwe marufuku.


View: https://youtu.be/srrplkQng5c?si=rHm3q20EIbbjyY23
 
Muda huongea...


Cc: Mahondaw
Hebu ona huu uchwara mwingine. Sasa humu mitandaoni wanatafuta nini? Hii mitandao tunaitumia vibaya nadhani. Swala la mahakani liishie mahakamani hukohuko. HAKUNA aliye juu ya sheria, kama amekamatwa subiri asomewe shitaka lake kisha mkamtetee huko mahakamani, sisi laymen wa sheria anataka tufanye nini?. Unapoichokoza mahakama au serikali uko peke yako lakini ukikamatwa unataka tuwe wote, upuuzi gani huu?

View: https://youtu.be/7n15NrC2nMg?si=fmiGvoEDFszoqmFr
 
Back
Top Bottom