Wanasiasa acheni kutuaminisha kwamba Umachinga na Bodaboda ni suluhisho la ajira kwa vijana

Wanasiasa acheni kutuaminisha kwamba Umachinga na Bodaboda ni suluhisho la ajira kwa vijana

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Naandika nikiwa na masikitiko makubwa sana.

Ina maana viongozi wetu hawaoni kwamba umachinga na bodaboda sio suluhisho la uhakika kuhusu ajira? Viongozi wote wa Chama Tawala na upinzani kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia makundi haya mawili ku-boost agenda zao za kisiasa wakati wakijua hizo ajira sio suluhisho la tatizo.

Wanaofanikiwa kiuchumi kupitia umachinga na bodaboda ni wachache mno kulinganisha na idadi ya wanaopata madhara ya kiafya ikiwemo ulemavu wa kudumu.

Pia vifo kwa ajali ya bodaboda ni vingi hivyo nguvukazi ya taifa kupungua. Na kwa upande wa Machinga hakuna wanachozalisha zaidi ya kusaidia viwanda vya China huku tukipoteza fedha za kigeni. Hata hawa matajiri wetu wengi wa Kkoo na miji mikubwa ni matajiri feki wanaopata pesa kwa uchuuzi badala ya uzalishaji na kufanya export. Kimsingi Wengi tunajua ukweli kuhusu haya makundi makubwa mawili.

Suluhisho kuu la tatizo la ajira ni kuingiza vijana wengi kwenye kilimo na ufugaji. Hii nchi imebarikiwa ardhi kubwa yenye rutuba na kwa bahati hakuna majanga mengi ya asili hasa mafuriko kulinganisha na nchi zingine. Kilimo nachozungumza hapa ni cha kisasa kwa maana ya umwagiliaji.

Hata ufugaji ni wa kisasa sio huu wa asili wa wamasai na wasukuma. Serikali ikija na sheria na sera nzuri za kilimo zitavutia sana vijana. Hizo sheria na sera zilenge kupunguza gharama za kulima kilimo cha kisasa na pia zisaidie kwenye kupata masoko.

Kuendelea kuonekana watetezi wa bodaboda na machinga huku tukijua hawa watu huwa wakiugua ndo mwisho wa kuingiza kipato ni unafiki usio na sababu.

Wabunge piganieni sheria na sera nzuri za kilimo na ufugaji badala ya kuweka nguvu nyingi kuhamasisha mambo yenye mchango mdogo kwa taifa.
 
Watu wenye akili kubwa kama huyu mleta mada ndo unakuta hawapati nafasi kubwa za kufanya maamuzi, badala yake unakutana na wapiga sarakasi. Kongole sana mleta mada, ila watu wenyewe hao unaowaambia sasa, hiiiiiiiiii
 
Niko Mikoani, na karibu kila wiki tunazungukia vijijini.
Sijawahi kumuona kijana hata mmoja kwenye jembe zaidi ya wazee-wazee na watu wazima.
 
Back
Top Bottom