Wanasiasa ambao Mama hawezi kuwafukuza, wanafunguka, anaoweza kuwafukuza wako kimya, na hata hawamtetei wala kummunga mkono?Unagundua nini?

Wanasiasa ambao Mama hawezi kuwafukuza, wanafunguka, anaoweza kuwafukuza wako kimya, na hata hawamtetei wala kummunga mkono?Unagundua nini?

Bwana Job anasema ipo siku Bongo itapigwa mnada, Mama anasema lazima akope.

Magufuli alitubana tulipe kodi akaonekana mbaya, Mama hataki tulipe lodi twende tukakope anaonekana mbaya.
kwani deni kubwa kakopa nani, na matozo yakwenye sim aliweka nani? Ndugai kasema kama waliamua wananchi walipe kodi kwann tuendelee kukopa?
 
Mama hataki tulipe lodi twende tukakope anaonekana mbaya.
Mwenzetu wewe wa nchi gani, hujasikia kuhusu tozo za miamala ya simu, tozo za manunuzi ya luku na wananchi walipolalamika wakaambiwa wahamie Rwanda?
 
Magufuli hakuweka tozo ila makusanyo TRA yalikuwa juu na hata kukopa alikopa kwa strategy na miradi ikaonekana na akaipeleka Tanzania uchumi wa kati na ya tisa kiuchumi Afrika kwa sababu alitambua Tanzania ina rasilimali nyingi mno kama madini,vivutio vya utalii n.k vikitumika ipasavyo hakuna haja ya tozo na mikopo chefuchefu
 
Mkuu mbona unakuwa mgumu kuelewa? Wakati wa jpm kuna ambacho hakikupanda kulinganisha na alipopokea toka kwa jk?
Sukari ilikuwa 1, 500, unakumbuka jpm ameacha ikiwa shilingi ngapi? Mafuta petrol ilikuwa 1, 750, unajua jpm ameniacha petrol ikiwa shilingi ngapi?
Huyu mtu wenu alikuwa mtu wa kawaida sana wacheni hii tabia ya kum-overate!!!
Ukiacha mafuta na sukari kipi kilipanda tena?

Nondo ilikuwa inauzwa elfu 30 kama ilivyo sasa?
Mafuta yalikuwa yanauzwa 2600 kama ilivyo sasa?
Ukikuwa unalipia maelfu kadhaa ukifanya miamala kama ilivyo sasa? Hivi utalinganisha upandaji wa sukari na huu uliopo sasa hivi?
 
Kuna kule kupanda kwa kawaida kutokana na mazingira ya uchumi! Mfano hututegemei gunia la mahindi lilikuwa likiuzwa elfu 20 mwaka 2010 liendelee kuuzwa elfu 20 mpaka leo.

Lakini unapoona vitu binapanda hovyo mafuta yanapanda, vifaa vya ujemzi vunapanda, tozo kila kona, hapo lazima kuna shida.

Huu wa sasa ni mfumuko wa bei
 
Ukiacha mafuta na sukari kipi kilipanda tena?

Nondo ilikuwa inauzwa elfu 30 kama ilivyo sasa?
Mafuta yalikuwa yanauzwa 2600 kama ilivyo sasa?
Ukikuwa unalipia maelfu kadhaa ukifanya miamala kama ilivyo sasa? Hivi utalinganisha upandaji wa sukari na huu uliopo sasa hivi?

Umezungumzia kutopanda wakati wa Magufuli na mifano nimekupa. Sasa kusema haikupanda kama sasa sijui unamaanisha nini.
 
Fafanua kwenye hiyo tirioni 20 riba ya mikopo ya nyuma tirioni ngapi?

Riba ilianza kupanda kwenye utawala wake? Marais wote toka Nyerere hadi JK anatoka madarakani deni lilifika 39t+, yeye 20t+ ndani ya miaka mitano. Hujiulizi tu?
 
Umezungumzia kutopanda wakati wa Magufuli na mifano nimekupa. Sasa kusema haikupanda kama sasa sijui unamaanisha nini.
Kwa hiyo upandaji wa bei kipindi cha Magu ni sawa na sasa?
 
Bro uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara, Magufuli alitubana tulipe kodi akaonekana mbaya, kisha deni la taifa likapaa kwa 20t within 5yrs! Sasa tunalipa kodi, lakini anakopa offcamera!
anaekopa mbele ya kamera unajua mashart ya iyo mikopo au camera inamuonyesha yeye masharti amuyaoni
 
na makusanyo ya TRA kila mwezi hivi bado wanatangaza!!
 
Kodi tulizolipa kwa Magufuli?

Mkapa kwa miaka yake 10 ya Urais alikopa tirion 20.

Kikwete kwa miaka yake 10 ya Urais alikopa trion 23.

Magufuli kwa miaka yake 5 ya Urais alikopa trion 29.

Anayesema Magufuli hakukopa ni kuonewa huruma maana atakuwa anafanikisha ajenda zake binafsi.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
Lazima ujue trilioni 10 miaka ya Mkapa ni sawa na trilioni ngapi miaka ya JPM (miaka 20 baadaye). Ujifanya mahesabu hayo utaona JPM alikuwa sawa kukopa Trilioni 29.
 
Bwana Job anasema ipo siku Bongo itapigwa mnada, Mama anasema lazima akope.

Magufuli alitubana tulipe kodi akaonekana mbaya, Mama hataki tulipe kodi twende tukakope anaonekana mbaya.
Mkuu hakuna binadamu wa wapuuzi kama watz..yaani ni matope yamejaa vichwani..hawaelewek wanataka nn..magu aliwakaba mabwenyewe wakwepa kodi walipe..alaf mswahil tu wa magomeni ambae yy hahusik chochote anamsema magu kuwa hafai..yaan injii hii ina laanaaa
 
Hao chawa wa Magu 2025 awarudi tena kwenye siasa Acha wabweke tu sasa wamalizie hasira zao.
 
Back
Top Bottom