Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kwanza fulctuation ni kubadilika badilika kwa bei na wala si kupanda kwa bei. watu wanazungumzia mfumko wa bei ambao kwa kiingereza ni "Inflation rate".Sasa sio kazi ya serikali kuwafanya wakulima wawe maskini miaka na miaka Ili wewe wa mjini ununue buku jero.
kubadilika badilika kwa bei ndiyo husababishwa na vitu kama kupungua kwa bidhaa na kuongezeka kwa bidhaa hizo hizo katika muda mfupi ama kuongezeka kwa mahitaji na kupungua kwa mahitaji katika muda mfupi. Lakini mfumko wa wa bei husababishwa zaidi na upungufu wa muda mrefu wa bidhaa bila ya kuwa na uhakika wa bidhaa hiyo kupatika katika muda mfupi ujao.
Sababu za kubadilika badilika kwa bei kunaweza pia kuwa chanzo cha kupanda kwa bei kama hali hiyo haitadhibitiwa kwa wakati. Kwa ivo Mkoa mmoja kuwa na maharage kwa bei ya shilingi 3,800, na kwingine 3,000 haimaanishi hakuna mfumko wa bei. Swali la msingi kwa kawaida kwenye maeneo hayo bei ya Maharage huwa ni shilingi ngapi!!??