Angalia hiyo makala very interesting
Nilichojifunza hapo kuna uzembe mkubwa sana upande wa polisi kupunguza ivyo vifo.
Kuna hatua zimepigwa on partnership working kati ya jeshi la polisi, asasi za kiraia na serikali ya mtaa I.e (ustawi wa jami na wenyeviti wa mitaa). Wote hao wakipokea kesi wanatakiwa waripoti polisi. Ila hapo kwenye ‘interagency team work’ shule pia inatakiwa ziingizwe na vituo vya afya ata wao wakiona mtoto ana alama za abuse shuleni au hospitali kuna mgonjwa ambae majeraha yake sababu ni kipigo wanatakiwa kuripoti polisi kupeleleza.
Sasa katika hiyo interagency working kwenye hiyo makala wanaolewa cha kufanya ili kupambana na hizo changamoto ni asasi za kiraia ya kuwa serikali iache mzaha kuachia watu kirahisi.
Ila alienisikitisha ni ofisa wa polisi anaesimamia dawati la ukatili wa watoto na wanawake. Kwanza lugha yake surely polisi wanakuwa trained on tone of language na choice of words kwenye press conference au interview wanapotoa ujumbe kwenye jambo ambalo serious. Yeye anaongea kama vile anabembelezana ata mtu ukimsikiliza uwezi mchukulia serious.
Pili eti anadai kuna watu huko chini wanafuta kesi kwa kuwapatanisha au kuzimaliza kifamilia hivyo wanashindwa shitaki. Mi sijawahi sikia upuuzi kama kesi za unyanyasaji ni criminal offence na polisi inaweza shitaki ata kama victim ataki kuendelea na case, pili ustawi wa jamii na mwenyekiti wa mtaa hawana mamlaka ya kutatua hizo jinai zaidi ya jeshi la polisi. Sasa ulitegemea polisi atoe onyo wanaozimaliza hizo case huko chini bila ya kuzifikisha kwao na wenyewe wanavunja sheria kwa sababu hiyo ‘abetting’ kusaidia mvunja sheria kwenye jinai na kosa hilo kisheria lenye adhabu yake.
Kwa kifupi jeshi la polisi inabidi lijitazame jinsi linavyosimamia haya mambo; unaweza kuta wanawake wengi wanaouwawa shida zao zilishafika kwa mwenyekiti wa kijiji au ustawi wa jamii but necessary actions were not taken, huko mbeleni jitu limeshaona alijafanywa kitu kwa muda mrefu mwishowe anaua.
Poor role ya jeshi la polisi ni sehemu kubwa ya haya matatizo.