John Kwambaza
Member
- Jul 15, 2021
- 6
- 4
Nadhani kama ningepewa task ngumu zaidi ni kutafuta mwanasiasa mmoja asiye mzandiki. Nalazimika kuhukumu kwamba pengine siasa ni uzandiki na uzandiki ndio siasa yenyewe.
Mjadala wenye afya kwa taifa unakuwa mzuri, Hadi pale wanasiasa wanapouteka nyara. Hoja ya katiba mpya na bandari ni mifano hai. Muda mwingine wanajisahau na kutamka maneno yenye maslahi kwa upande wao tu.
Huko kwenye majukwaa ndio taifa limegawanywa kimkakati katika makundi mawili, yaani CCM na non CCM. Kiufupi Kama wewe sio CCM manake ni kinyume chake, nadhani huu ni uzandiki wa hatari Sana kwa afya ya taifa.
Ikitokea mtu anatoa maoni yake kuhusu katiba mpya au Bandari, inatokea tu kwamba msimamo wake huchukuliwa katika misimamo ya kisiasa, hakuna maoni nje ya siasa.
Je, haiwezekani mtu akakosa mrengo wa kisiasa na bado akatoa maoni kama Mtanzania?