Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,618
- 4,605
Viongozi wa dini. Hili eneo wengi wanaliogopa ila ni eneo hatari sana linaloathiri ustawi wa watu wetu. Lina uhusiano mkubwa sana na politicians. Eneo la dini limekuwa hatarishi sana kukwamisha ustawi wa watu wetu. Viongozi wanajipatia ukwasi usiomithirika kwa kuwanyonya wananchi mafukara sana kwa kuuza leso, chimvi na maji na kuwabrain wash watu wetu huku hao wanaojiita mitume na manabii wakijilimbikizia mali chafu kutoka kwa jamii fukara hii hali inaumiza sana.
Uhusiano wa moja kwa moja wa viongozi wa dini na wanasiasa. Viongozi wa dini wanatumia ujinga unaosababishwa na wanasiasa na ufukara uliotopea katika jamii kutokana na kukosa pa kwenda ila kuona kuwa dini itamaliza matatizo yao mfano wengi wana wagonjwa wasio na matumaini ya kupona , ufukara na ujinga uliokithiri. Wanasiasa wameshindwa kuweka sheria na mifumo ya kusimamia utapeli huu. Ila pia uoga wa nguvu za hawa matapeli wa dini inawapa kigugumizi kuchukua hatua. Serikali zote duniani zinalinda masilahi ya watu wao ila kwa watanzania na waafrika wengi imekuwa saratani.
Wanasiasa
Hili ni kundi lingine la kutupia macho na jamii yetu. Kwani limekuwa kundi selfish la aina yake. Percent kubwa ya rasilimali zenye mchango mkubwa wa ustawi wa jamii huishia kwa hili kundi mfano , kujipendelea kwa kujipatia magari ya gharama kubwa imekuwa kufuru na new normal . malipo ya wawakilishi wa hawa watu mafukara aka wabunge , mpango wa kuwalipa wake wenza wa viongozi hata kama washachuma wasivyokuwa na kazi navyo. Kujipangia benefiti kama nyumba za bure , kutolipa kodi na hata pamoja na hayo yote kundi hili ndilo linaongoza kuiba rasilimali za Taifa kuanzia ngazi za juu hadi chini kabisa.
Kama kungekuwa na Takwimu kamili za mapato yanayonyonywa na viongozi hawa waliojivisha ngozi ya kondoo na hawa wanasiasa basi jamii ingeamka.
Kuna symbiotic relationship kati ya makundi haya mawili . Moja likitegemea kuchuma uungwaji wa hawa mafukara wasiojitambua na lingine likitumia uhohehae, na ujinga uliozalishwa na hili kundi la pili kuwatapeli na ndo maana kundi moja ambalo lingekuwa mwarobaili liko kimya.
Napendekeza kama jamii tunge review maadui wa maendeleo tuka update na kupachika haya makundi labda mambo yangebadirika maana hali ya mwananchi wa kawaida kabisa ukilinganisha na haya makundi japo yana uhusiano wa moja kwa moja ni mbingu na ardhi.
Shangwe kwa vijana wa Gen Z la nchi jirani kwa kujitambua na kulikalia kooni kwa kutambua janja janja ya hili kundi kuu ambalo limemwaga manyanga na kukata matumizi kila sehemu mfano magari kufuru, bajeti janja janja za kuliibia taifa , pesa za wake wenza nk . Naamini siku moja isiyotabirika mafukara na wajinga wetu nao watagundua janja ya makundi haya.
Nawasilisha.
Nakala kwa bwana Mwanshambwa.