Wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa hujiona spesho sana!

Wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa hujiona spesho sana!

Unaijua mbinu ya kung'ata na kupuliza kwa kupigapiga kwa upole mgongoni aisee.Upo vizuri.Pale Lumumba watakuambia weye ni msemakweli hadi basi.
Mimi ni mwanahabari kazi yangu ni kukumbusha tuu kile kichosemwa humu.

Kwa vile sii wengi wanaijua karma, hivyo wakati wakitenda matendo yao maovu, no one keeps track ya matendo hayo, sasa siku wakilipwa ndio watu mnashangaa kwa bakora na mapigo ya karma na wanaokula bakora hizo wala hawakumbuki walifanyaga nini!.
Hivyo mimi I keep a very good record humu, mfano walipunuonea ZZK na kumtimua kama mwizi, niliwaeleza humu, Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!" lakini na ZZK mwenyewe pia nilimuonya Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!

Sasa Chadema imenyauka ZZK anachanua!.
Karma is real!.
P
 
Serikali yoyote duniani Ina kitengo cha uuaji!

Kitengo rasmi Cha kuwashughulikia wahuni, wenye kuhatarisha usalama wa raia, amani ya Nchi, au wenye kuhatarisha mustakabali na utulivu wa serikali inayotawala!

Leo hii tunaona serikali inavyowashughulikia raia wake kwa kututanabaisha kuwa wao ni panya road! Na Jamii inafurahi! Na tutake tusitake, wapo wanaouawa humu si panya road! Haya Ni mauaji ya serikali, na damu hii inabebwa na mtawala husika!

Huo ni mfano tu wa mauaji yaliyo wazi na halisi, yapo yaliyo gizani pia! Serikali yoyote humwaga damu za raia wake!

Point yangu ni nini?
Point yangu Ni kuwakumbusha wanasiasa wasijione spesho kuliko wengine! Kama serikali imeweka idara za kuua raia, basi wawe tayari kushughulikiwa Kama wamebainika kuwa hatari kwa amani na usalama wa Nchi, au wanadhalilisha serikali yao. Ni kosa la kiusalama kudhalilisha serikali!

Leo hii tunaona ni sahihi kuua panya road, lakini uchunguzi wa kipolisi ungebaini kuwa mwanasiasa Fulani, au mfanya biashara mkubwa anafadhili genge la panya road ili kuharibu taswira ya Nchi, basi hapo tungelalamika Sana iwapo mwanasiasa huyo angeuawa!

Wanasiasa wajue hawana thamani yoyote mbele ya Mungu ya kuwazidi raia wengine. Nanyi munastahili kuuawa Kama raia wengine! Kama hamustahili Basi na raia wengine wasiuawe pia!

Leo hii kelele ni nyingi za kumsema JPM Ni muuaji. Ukiuliza amemuua nani? Unatajiwa Ben saanane, Azori, na risasi za Lisu. Hawa Ni wanasiasa. Mauaji kule kibiti hayatajwi, kwasababu tu hakuna mwanasiasa aliyekufa.

Kama Ben saanane ameuawa bila hatia, dhambi yake Ni sawasawa na "panyaroad" aliyeuawa bila hatia!
Kama Lisu alipigwa risasi bila hatia, dhambi yake ni ileile ya kumpiga risasi "panyaroad" asiye na hatia!

Tutulie, tuendelee kushuhudia mauaji ya raia kwa raia, Serikali kwa raia!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sawa panya road tumekusikia,wazo lako tunalifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom