LIKUYU SEKA
Member
- Nov 15, 2013
- 53
- 24
Salaam za dhati Watanzania wenzangu,natumai mungu amewajaalia Afya njema na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.
Lengo la kijiwaraka hiki ni kusema nanyi watanzania wenzangu kidogo kuhusu mchakato Wa katiba yetu,binafsi tangu bunge la katiba kumaliza muda wake na katiba kusambazwa kwenye makundi mbalimbali kumeibuka mjadala mpana juu ya katiba pendekezwa lakini chakusikitisha mjadala huu umekuwa Wa upande mmoja tumekuwa tukiwachagulia watu cha kujadili wengi wakisema tusipigie kura katiba hiyo na wanaenda mbali sana hadi kufikia kutoa matamko ya kuhalalisha misimamo yao,jambo ambalo ni kubaka Uhuru Wa mawazo kwa wengine.
Tumesikia wanasiasa wakituambia kuhusu vipengele lukuki vyenye mapungufu kwa muono wao lakini cha kushangaza hawatuelezi mazuri yaliyopo kwenye katiba,hivi Tujiulize kigugumizi cha kutosema mazuri kinaanzia wapi?na kwanini wanafanya hivyo????hivi wanafanya hivyo kwa kujua au kutojua??haya ni maswali tunayopaswa kujiuliza kabla ya kuwashabikia kwa moyo Wa dhati .
Kama taifa lenye watu makini hatupaswi kufanya mzaha kwenye mchakato Wa katiba Maana katiba ni Moyo Wa taifa lolote duniani,mjadala huu Wa katiba unapaswa kuwa huru kwa watu kusoma katiba na wale wataalamu kuelimisha watu kujua yaliyomo kwenye katiba pendekezwa, ni vyema tukawaacha watanzania wenyewe kufanya maamuzi juu ya mustakabali Wa Taifa lao .
Wanasiasa tuwaache walala hoi wafanye maamuzi kuhusu mustakabali Wa taifa lao,wakati umefika watu waachwe wenyewe wasome katiba na wafanye maamuzi kutokana na walichosoma wao,Tukumbuke kuwa Tanzania ni yetu sote wenye sauti za kusema,wasio na sauti,walalahoi na walala doro.
Tujitoe kwa dhati kusoma katiba pendekezwa watanzania tusikubali wanasiasa kutupigia ramli kwenye katiba hizi si zama za kuhadithiana ni zama za kusikiliza na kufatilia sisi wenyewe...
Katiba yetu kwanza mengine Baadae..