Wanasiasa Tuachieni Katiba Yetu

Wanasiasa Tuachieni Katiba Yetu

LIKUYU SEKA

Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
53
Reaction score
24
Salaam za dhati Watanzania wenzangu,natumai mungu amewajaalia Afya njema na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.

Lengo la kijiwaraka hiki ni kusema nanyi watanzania wenzangu kidogo kuhusu mchakato Wa katiba yetu,binafsi tangu bunge la katiba kumaliza muda wake na katiba kusambazwa kwenye makundi mbalimbali kumeibuka mjadala mpana juu ya katiba pendekezwa lakini chakusikitisha mjadala huu umekuwa Wa upande mmoja tumekuwa tukiwachagulia watu cha kujadili wengi wakisema tusipigie kura katiba hiyo na wanaenda mbali sana hadi kufikia kutoa matamko ya kuhalalisha misimamo yao,jambo ambalo ni kubaka Uhuru Wa mawazo kwa wengine.

Tumesikia wanasiasa wakituambia kuhusu vipengele lukuki vyenye mapungufu kwa muono wao lakini cha kushangaza hawatuelezi mazuri yaliyopo kwenye katiba,hivi Tujiulize kigugumizi cha kutosema mazuri kinaanzia wapi?na kwanini wanafanya hivyo????hivi wanafanya hivyo kwa kujua au kutojua??haya ni maswali tunayopaswa kujiuliza kabla ya kuwashabikia kwa moyo Wa dhati .

Kama taifa lenye watu makini hatupaswi kufanya mzaha kwenye mchakato Wa katiba Maana katiba ni Moyo Wa taifa lolote duniani,mjadala huu Wa katiba unapaswa kuwa huru kwa watu kusoma katiba na wale wataalamu kuelimisha watu kujua yaliyomo kwenye katiba pendekezwa, ni vyema tukawaacha watanzania wenyewe kufanya maamuzi juu ya mustakabali Wa Taifa lao .

Wanasiasa tuwaache walala hoi wafanye maamuzi kuhusu mustakabali Wa taifa lao,wakati umefika watu waachwe wenyewe wasome katiba na wafanye maamuzi kutokana na walichosoma wao,Tukumbuke kuwa Tanzania ni yetu sote wenye sauti za kusema,wasio na sauti,walalahoi na walala doro.

Tujitoe kwa dhati kusoma katiba pendekezwa watanzania tusikubali wanasiasa kutupigia ramli kwenye katiba hizi si zama za kuhadithiana ni zama za kusikiliza na kufatilia sisi wenyewe...

Katiba yetu kwanza mengine Baadae..
 
Bora wewe umenena maana watu wengine bhana wamekuwa watata humu ndani.
 
Wanasiasa watakuachiaje katiba yako wakati wao (wanasiasa) ndio walioitengeneza na kuipitisha kwa kukatika mauno pale Dodoma..? Mnajifanya mmesahau maoni ya Watanzania yaliokusanywa na Tume ya Jaji Warioba yalitupiliwa mbali na hao wanasiasa..?

Kuna muwakilishi yeyote ambae wewe ulimchagua ili akakuwakilishe kwenye bunge maalumu la kutunga katiba..?

Katiba hii ni ya wanasiasa.. imepitishwa na wanasiasa ili kulinda maslahi yao.. Kwa hivyo ni katiba hii siyo ya wananchi na haifai hata mkiipigia debe..
 
We endelea kupiga jero jero huko za Ukawa, c umetumwa uje kuipinga wala watu hawakushangai we endelea maan ndo mlo wako huo kila kukicha, hahahah kama imekuuma kuhusu katiba hii nenda kajinyonge.
 
Salaam za dhati Watanzania wenzangu,natumai mungu amewajaalia Afya njema na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.

Lengo la kijiwaraka hiki ni kusema nanyi watanzania wenzangu kidogo kuhusu mchakato Wa katiba yetu,binafsi tangu bunge la katiba kumaliza muda wake na katiba kusambazwa kwenye makundi mbalimbali kumeibuka mjadala mpana juu ya katiba pendekezwa lakini chakusikitisha mjadala huu umekuwa Wa upande mmoja tumekuwa tukiwachagulia watu cha kujadili wengi wakisema tusipigie kura katiba hiyo na wanaenda mbali sana hadi kufikia kutoa matamko ya kuhalalisha misimamo yao,jambo ambalo ni kubaka Uhuru Wa mawazo kwa wengine.

Tumesikia wanasiasa wakituambia kuhusu vipengele lukuki vyenye mapungufu kwa muono wao lakini cha kushangaza hawatuelezi mazuri yaliyopo kwenye katiba,hivi Tujiulize kigugumizi cha kutosema mazuri kinaanzia wapi?na kwanini wanafanya hivyo????hivi wanafanya hivyo kwa kujua au kutojua??haya ni maswali tunayopaswa kujiuliza kabla ya kuwashabikia kwa moyo Wa dhati .

Kama taifa lenye watu makini hatupaswi kufanya mzaha kwenye mchakato Wa katiba Maana katiba ni Moyo Wa taifa lolote duniani,mjadala huu Wa katiba unapaswa kuwa huru kwa watu kusoma katiba na wale wataalamu kuelimisha watu kujua yaliyomo kwenye katiba pendekezwa, ni vyema tukawaacha watanzania wenyewe kufanya maamuzi juu ya mustakabali Wa Taifa lao .

Wanasiasa tuwaache walala hoi wafanye maamuzi kuhusu mustakabali Wa taifa lao,wakati umefika watu waachwe wenyewe wasome katiba na wafanye maamuzi kutokana na walichosoma wao,Tukumbuke kuwa Tanzania ni yetu sote wenye sauti za kusema,wasio na sauti,walalahoi na walala doro.

Tujitoe kwa dhati kusoma katiba pendekezwa watanzania tusikubali wanasiasa kutupigia ramli kwenye katiba hizi si zama za kuhadithiana ni zama za kusikiliza na kufatilia sisi wenyewe...

Katiba yetu kwanza mengine Baadae..
Ni kweli watuache wenyewe tuisome Katiba Inayopendekezwa na tufanye uamuzi sahihi bila kulazimishwa wala kupelekeshwa. Hapo ndugu yangu umenena. Let's not be biased!
 
Sosoliso nafikiri hukusoma vizuri hiyo post ndugu yangu.

Tunaposema wanasiasa watuachie katiba yetu tunataka wasituamulie chakufanya...halafu unasema hatukuwachagua kutuwakilisha umesahau wabunge tuliowachagua waoikuwepo kwenye bunge maalum la katiba???na je rais alipoteua wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali hujui alifanya hvyo kwa maslahi ya umma....#Wanasiasa watuachie katiba yetu...Wakati ni sasa usikaririshwe soma mwenyewe katiba
 
Wanasiasa watakuachiaje katiba yako wakati wao (wanasiasa) ndio walioitengeneza na kuipitisha kwa kukatika mauno pale Dodoma..? Mnajifanya mmesahau maoni ya Watanzania yaliokusanywa na Tume ya Jaji Warioba yalitupiliwa mbali na hao wanasiasa..?

Kuna muwakilishi yeyote ambae wewe ulimchagua ili akakuwakilishe kwenye bunge maalumu la kutunga katiba..?

Katiba hii ni ya wanasiasa.. imepitishwa na wanasiasa ili kulinda maslahi yao.. Kwa hivyo ni katiba hii siyo ya wananchi na haifai hata mkiipigia debe..

Cha msingi hapo ni wewe kutambua nafasi yako ya maamuzi acha kuishi kwa hisia,mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya ni wetu sote ila kuna baadhi ya watu wachache wanaofikiri Katiba ni ya kwao wamefikia hatua ya kutengeneza makundi/kambi utafikiri tuko vitani ha ha ha ha hao ndo hatuwataki hao ni sawa na mchwa wanaotafuna kwa ndani afu kwa nje ubao unauona uko poa baada ya muda ana fall down, huo sio mpango watuache tuipe kura za ndiyo ili taifa letu liendelee kupata mafanikio!
 
Salaam za dhati Watanzania wenzangu...

Katiba yetu kwanza mengine Baadae..

Mbona unalalamika na kutia huruma kuona wanaharakati wanaongelea mabaya tu pekeake na si kuongelea mazuri yaliyomo?

Wanavyoongelea mabaya Hawajasema kwamba hakuna mazuri la hasha! Hujawaelewa hawa watu, wanajua kwamba mazuri yapo ila wanachotaka ni kuwaonyesha watu mabaya hayo ili ipigiwe kura ya hapana, then ije irekebishwe ili itoke katiba iliyo bora zaidi.

Umesema katiba ni kama moyo wa nchi, inakuaje moyo ukawa unafanya baadhi ya kazi vizuri lakini ukawa una baadhi ya kasoro. Je moyo ukiwa una kasoro hicho kiumbe kitaishi kwa furaha na amani? Hiyo itakua ni sawa sawa na mgonjwa wa moyo! Anaishi lakini kwa shida.

Unapozungumzia wanasiasa kuipinga hii katiba unawalenga kina nani labda?
Maana wanaoipinga hii katiba pendekezwa sio wanasiasa pekeake, wengi wanaoipinga ni taasisi mbali, wanasheria binafsi na mashirika ya kutetea haki za binadamu, je hao wote ni wanasiasa?

Kwa hiyo wanasiasa wakiipigia debe katiba pendekezwa ni sawa! Ila wakitokea wanaoipinga hawako sawa, hivyo ndo mnavyotaka enhee?

Kama suala ni kuwaamulia wananchi hao wanasiasa wanowataka wananchi waipigie kura ya ndio wao ndo hawawaamulii wananchi enhee?

Tafakari acha ushabiki kwenye suala muhimu katika taifa!
 
Wote unaowataja pamoja na makundi yao walituma wawakilishi wao huko mjengoni sasa kelele za nini?kawaulize nini walichokwenda kukifanya kama sio kula posho tu,waliokuwa makini ndo walifanikisha kupatikana kwa katiba inayopendekezwa!
 
Sosoliso nafikiri hukusoma vizuri hiyo post ndugu yangu.

Tunaposema wanasiasa watuachie katiba yetu tunataka wasituamulie chakufanya...halafu unasema hatukuwachagua kutuwakilisha umesahau wabunge tuliowachagua waoikuwepo kwenye bunge maalum la katiba???na je rais alipoteua wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali hujui alifanya hvyo kwa maslahi ya umma....#Wanasiasa watuachie katiba yetu...Wakati ni sasa usikaririshwe soma mwenyewe katiba

Mkuu kuna mbunge yoyote ambae wewe ulimchagua kwa ajili ya kujadili na kupitisha rasimu ya katiba..? Wabunge waliokuwa pale wote ni wanasiasa ambao walichaguliwa kwa ajili ya kuwakilisha wananchi kwenye bunge la muungano..

Kwa taarifa yako ili tupate katiba ambayo sio ya wanasiasa kulitakiwa wapatikane wawakilishi wa wananchi ambao walichaguliwa kwa ajili ya kujadili na kupitisha katiba ya wananchi.. Yaani kungefanyika uchaguzi wa kuwapata wawakilishi (ambao sio wanachama wa chama chochote cha kisiasa).. Hao ndo wangekuwa wengi kwenye bunge la katiba na hawa wanasiasa wabunge wangetakiwa kuwa wachache pamoja na makundi tofauti.. Hii ndo ilifanyika Kenya na nchi nyingine na hivyo kuwa na uhalali wa kuiita katiba ya wananchi..

Hii iliotengenezwa Dodoma ni ya wanasiasa na imewekwa ili kulinda maslahi ya wanasiasa hao walioipitisha.. Mfano kipengele cha wananchi kuwa na uwezo wa kumuondoa mbunge wao kwa kutowajibika au ugonjwa wa muda mrefu.. Kwanini wamekitoa..? Huoni walikuwa wanajilinda wao..? Kuingiza miiko ya uongozi kwenye katiba.. Kwanini wameiondoa.. Huoni walikuwa wanajilinda wao..? Kuweka kikomo cha ubunge.. kwanini wameondoa.. Huoni walikuwa wanajilinda wao..? Halafu uje hapa useme ati ninakaririshwa.. Hiyo ni katiba ya wanasiasa na itabaki kuwa ya wanasiasa na kamwe haitapita..

Hii id ya Jay Milionea ndo mnaitumia kwa mipasho ya taarabu eeh... Katiba haipiti kwa mipasho ya taarabu au kukata miuno..
 
Last edited by a moderator:

SOSOLISO unaenda mbele na kurudi nyuma afu unachomeka hoja zako zisizo na nguvu humu!!hujui mamlaka ya wananchi katika jambo hili au unafanya makusudi? Wao wamekaa Dodoma na sisi tutakaa kwenye box la kura kusema NDIYO au HAPANA hulijui hilo?

Suala la maadili ya viongozi wa umma limewekwa vizuri kwenye katiba inayopendekezwa na wala halijaondolewa kama unavyodai soma vizuri sura ya 1 sehemu ya pili ibara ya 30 na 31 utaona kipengele kinachozungumzia Utii wa Miiko ya Uongozi wa Umma na Marufuku kwa baadhi ya vitendo.Naomba usome vizuri kiongozi wangu ili twende sawa maana masuala ya ukomo wa ubunge si liko mikononi mwako sasa unataka nini? Au unataka Katiba ikuwekee wabunge, mbunge kama unampenda anaweza kukaa miaka kibao anza na UKAWA utawaona wabunge wao wamevuta miaka kibao, vivyo hivyo chama tawala nao kama kawa miaka kibao na wananchi hao hao ndo wamewapa ridhaa ya kuwawakilisha!unasemaje hapo?
 
nadhani tatizo si siasa bali siasa zimegeuka mapango na maficho na vitu vingine ambavyo vinatumia migongo ya siasa kufanya mambo ya kipuuuzi.
 
Jitokeze kujiandikisha ili uweze kushiriki kupiga kura ya maoni kwa kuipigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa
 
nadhani tatizo si siasa bali siasa zimegeuka mapango na maficho na vitu vingine ambavyo vinatumia migongo ya siasa kufanya mambo ya kipuuuzi.
Sasa wakati ndo huu uisome katiba hii inayopendekezwa then upige kura ya ndiyo maaa ndiyo sukuhisho ya kero zote kijana.
 
Mkuu kuna mbunge yoyote ambae wewe ulimchagua kwa ajili ya kujadili na kupitisha rasimu ya katiba..? Wabunge waliokuwa pale wote ni wanasiasa ambao walichaguliwa kwa ajili ya kuwakilisha wananchi kwenye bunge la muungano..

Kwa taarifa yako ili tupate katiba ambayo sio ya wanasiasa kulitakiwa wapatikane wawakilishi wa wananchi ambao walichaguliwa kwa ajili ya kujadili na kupitisha katiba ya wananchi.. Yaani kungefanyika uchaguzi wa kuwapata wawakilishi (ambao sio wanachama wa chama chochote cha kisiasa).. Hao ndo wangekuwa wengi kwenye bunge la katiba na hawa wanasiasa wabunge wangetakiwa kuwa wachache pamoja na makundi tofauti.. Hii ndo ilifanyika Kenya na nchi nyingine na hivyo kuwa na uhalali wa kuiita katiba ya wananchi..

Hii iliotengenezwa Dodoma ni ya wanasiasa na imewekwa ili kulinda maslahi ya wanasiasa hao walioipitisha.. Mfano kipengele cha wananchi kuwa na uwezo wa kumuondoa mbunge wao kwa kutowajibika au ugonjwa wa muda mrefu.. Kwanini wamekitoa..? Huoni walikuwa wanajilinda wao..? Kuingiza miiko ya uongozi kwenye katiba.. Kwanini wameiondoa.. Huoni walikuwa wanajilinda wao..? Kuweka kikomo cha ubunge.. kwanini wameondoa.. Huoni walikuwa wanajilinda wao..? Halafu uje hapa useme ati ninakaririshwa.. Hiyo ni katiba ya wanasiasa na itabaki kuwa ya wanasiasa na kamwe haitapita..

Hii id ya Jay Milionea ndo mnaitumia kwa mipasho ya taarabu eeh... Katiba haipiti kwa mipasho ya taarabu au kukata miuno..
Wewe mbumbu usiyejua kitu, hii ni ya wananchi na itapita tuuuu upende usipende, kama huitaki ya kwako iko wapi? Tuachie Tanzania yetu bhana kama huipendi jinyonge, kama una kipaji cha kuimba hizo taarabu ruksa weka mipasho yako kwenu huko na sio hapa ndani, nahc una matatizo ya akili wewe sio bure.
 
Jitokeze kujiandikisha ili uweze kushirki kura ya maoni na hatimaye tupate katiba mpya,tanzania ya sasa na ijayo iko mikononi mwako,shiriki kulijenga taifa lako
 
lipo tatizo hapo kwa maana wapo wasiopenda vichaka vya wezi na wababaishaji viondolewe lakini nijukumu la wananchi wote kuweka katiba yao sawa.

kila mwananchi atambue maendeleo yake atajiletea yeye mwenyewe. kwa vipi ni kwa kuweka mambo sawa na hili linaanzia katika kuhakikisha katiba inayomtumikia yeye.

Sasa wakati ndo huu uisome katiba hii inayopendekezwa then upige kura ya ndiyo maaa ndiyo sukuhisho ya kero zote kijana.
 
lipo tatizo hapo kwa maana wapo wasiopenda vichaka vya wezi na wababaishaji viondolewe lakini nijukumu la wananchi wote kuweka katiba yao sawa.

kila mwananchi atambue maendeleo yake atajiletea yeye mwenyewe. kwa vipi ni kwa kuweka mambo sawa na hili linaanzia katika kuhakikisha katiba inayomtumikia yeye.
Sasa unadhani hayo maendeleo yatakujaje bila ya wewe kusema ndiyo kwa katiba hii, nakushauri bwana ego ukaisome hii katiba maana imesheeni mambo mengi sana ambayo naamini wewe mengine huyajui lakn unaonekana uko kimaslahi yako ya kuendeleza kuipinga hii katiba.
 
mjinga ndiye anayeweza kufundishwa apige kura gani, na mjinga ndiye anayedhani anaweza kumfundisha mwananchi mwenzake kura yake iweje.

mwelevu yeyote anatambua kuwa kila mwananchi ana maamuzi yake juu ya katiba.

kama anaona katiba imekidhi au haijakidhi basi anapiga kura na matokeo ya kura ndiyo yataamua kama katiba ifanyiwe marekebisho kwa maana wananchi wameikataa kuwa kuna mambo ya muhimu hayajawekwa au iko vizuri kwa maana kila kitu wananchokihitaji wananchi kimewekwa na imebaki utekelezaji tu.

kila mwananchi anafanya maamuzi yake labda mjinga wa kuelewa ndiye anasaidiwa na wenzake kuweka dole la ndio au hapana.

Sasa unadhani hayo maendeleo yatakujaje bila ya wewe kusema ndiyo kwa katiba hii, nakushauri bwana ego ukaisome hii katiba maana imesheeni mambo mengi sana ambayo naamini wewe mengine huyajui lakn unaonekana uko kimaslahi yako ya kuendeleza kuipinga hii katiba.
 
nadhani tatizo si siasa bali siasa zimegeuka mapango na maficho na vitu vingine ambavyo vinatumia migongo ya siasa kufanya mambo ya kipuuuzi.

Tafakari na uchukue hatua kwa kuipigia Kura Katiba mpya!
 
Back
Top Bottom