Wanasiasa wa Afrika ni wauaji na wabinafsi

Wanasiasa wa Afrika ni wauaji na wabinafsi

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Unajiuliza waliwezaje kupokea pesa za Covid-19 na kudai wanazipeleka kwenye kujenga madarasa mengine wanaweka na tiles na ac?

Wanaacha watoto wadogo wanakufa kwa kukosa matibabu na bima inasitishwa kwa madai kuwa michango haitoshi. Lakini hawa wanasiasa wananunuliana magari ya kifahari sana kwa pesa za hawa maskini ambao wameachwa wafe kama panya.

Shetani kazi yake ni kuua na kuharibu. Siku zote. Na ndicho ambacho tuna ona kwa watu maskini. Wao wanaachwa wafe. Watoto wao nao wanakosa matibabu. Ila wanasiasa hawa wanapata matibabu kwa pesa za maskini hawa ambazo wananyonywa.

Mnapewa misaada kupitia Watanzania kisha mnagawana pesa na kuwaacha Watanzania wafe.
 
Unajiuliza waliwezaje kupokea pesa za Covid 19 na kudai wanazipeleka kwenye kujenga madarasa mengine wanaweka na tiles na ac?

Wanaacha watoto wadogo wanakufa kwa kukosa matibabu na bima inasitishwa kwa madai kuwa michango haitoshi. Lakini hawa wanasiasa wananunuliana magari ya kifahari sana kwa pesa za hawa maskini ambao wameachwa wafe kama panya.

Shetani kazi yake ni kuua na kuharibu. Siku zote. Na ndicho ambacho tuna ona kwa watu maskini. Wao wanaachwa wafe. Watoto wao nao wanakosa matibabu. Ila wanasiasa hawa wanapata matibabu kwa pesa za maskini hawa ambazo wananyonywa.

Mnapewa misaada kupitia watanzania kisha mnagawana pesa na kuwaacha watanzania wafe. Wanasiasa wa hivi ni mashetani kabisa.
Kabisa, watu wanakufa kwa kukosa dawa au fedha ndogo tu kama 100,000 wakati wanasiasa wanaendesha magari ya 250M!
 
Paza paza paza sauti zaidi ili usikike mkuu, why Botswana 🇧🇼 wana almost zero corruption sisi tusiweze?

Yaani idara za kutoa haki hapa nchini ndizo zinaongoza kwa rushwa, mahakama, afya, home affairs hasa immigrations na police why why why
 
Nilishawahi kusema kama ingekuwa amri yangu kiumbe yeyote anaijiita mwanasiasa akiwa mbele yangu nikutandika mikwaju, akitokea mwanasiasa mwingine akiuliza naye mikwaju hivyo hivyo hawa wanasiasa nakubaliana na wewe kuwa ni mawakala wa shetani.
 
Paza paza paza sauti zaidi ili usikike mkuu, why Botswana 🇧🇼 wana almost zero corruption sisi tusiweze?,yaani idara za kutoa haki hapa nchini ndizo zinaongoza kwa rushwa, mahakama, afya,home affairs hasa immigrations na police why why why

Kwa Tanzania rushwa inaanzia ngazi za chini kabisa, yaani huku mitaani tunakoishi.

Ili rushwa iishe inabidi tabia zetu kwa ujumla wetu tubadilike...
 
"Mwafrika hawezi kujitawala" Botha

Viongozi wa Afrika wanawaza chaguzi tu ili wabaki kwenye madaraka na sio kutatua changamoto za wananchi.
 
Kwakweli ukifikiri kwa umakini kidogo tu inauma sana. Hakuna namna yoyote binadamu mwenye fikra za kibinadamu anaweza Fanya hivi. Tukipiga total cost tu ya magari yote ya kifahari serikali nzima hapa Tanzania, ni garama zingeweza kutatua gap kubwa ktk sekta muhimu kama huduma za afya, shule na maji hasa kwa vijijini. Swali rahisi kwanini nguvu haielekezwi huko ilihali kitu kama gari sio emergency..... Niuwakala tu wakishetani. Yani watu masikini wataabike wafe tu.
 
Ona kwa mfano sasa madarasa yapo wanashindwa nini kufanya bajeti ya kuwaajiri walimu? Ambapo wajiajiri walimu watapunguza wimbi la vijana waliokosa ajira, vilevile hawa walimu watalipa kodi, na wataongeza mzunguko wa uchumi pindipo wanapofanya manunuzi, Nchi inakopa hela kwajili ya kugharamia ofisi, arafu mwl mmoja wa baiolojia anafundisha shule mzima arafu watu wanapongezana eti naishukuru serikali kwa kumwaga ajira kweli!☹️☹️☹️
 
Unajiuliza waliwezaje kupokea pesa za Covid-19 na kudai wanazipeleka kwenye kujenga madarasa mengine wanaweka na tiles na ac?

Wanaacha watoto wadogo wanakufa kwa kukosa matibabu na bima inasitishwa kwa madai kuwa michango haitoshi. Lakini hawa wanasiasa wananunuliana magari ya kifahari sana kwa pesa za hawa maskini ambao wameachwa wafe kama panya.

Shetani kazi yake ni kuua na kuharibu. Siku zote. Na ndicho ambacho tuna ona kwa watu maskini. Wao wanaachwa wafe. Watoto wao nao wanakosa matibabu. Ila wanasiasa hawa wanapata matibabu kwa pesa za maskini hawa ambazo wananyonywa.

Mnapewa misaada kupitia Watanzania kisha mnagawana pesa na kuwaacha Watanzania wafe.
Dah! Nashindwa ata jinsi ya kukoment ila kama tumeumbwa na Mungu natukawekwa katika hii inchi Ili sote tuifaidi ila wachache tuliowapa dhamna ya ungozi badala yetu Ili wawe wanaorganise mambo alfu ndo wanatuumiza namna hii tulio wengi INAUMA SANA ZAIDI

Wakusanye Kodi kutoka kwetu,wakusanye toza na mapato mbalimbali kutoka kutoka kwenye vitega uchumi vya nchi yetu sote alafu waje kutulambisha kidogo kitu kingi Wale wao,ukiwahoji WA kutishe Kwa vitu vilivyo nunuliwa Kwa Kodi zetu,DAH![emoji58][emoji17][emoji18]

Sasa hivi mtu hata kama unajua chochote kile kinavyotakiwa kwenda Kwa usahii unalazimika kukaa KIMYA KIMYAAAA.
SI UNAKULA UGALI NA MAHARAGE NA UNASHIBA BASI TULIA USITAKE MAMBO YAWE MENGI

.ILA WAKUMBUKE NIYETU SOTE HII NCHI NA WAWE NA UTU NA WAJIFUNZE KUHISI MAUMIVU TUNAYO YA HISI WENGINE KUTOKANA NA HALI ISIYO HALI
 
Unajiuliza waliwezaje kupokea pesa za Covid-19 na kudai wanazipeleka kwenye kujenga madarasa mengine wanaweka na tiles na ac?

Wanaacha watoto wadogo wanakufa kwa kukosa matibabu na bima inasitishwa kwa madai kuwa michango haitoshi. Lakini hawa wanasiasa wananunuliana magari ya kifahari sana kwa pesa za hawa maskini ambao wameachwa wafe kama panya.

Shetani kazi yake ni kuua na kuharibu. Siku zote. Na ndicho ambacho tuna ona kwa watu maskini. Wao wanaachwa wafe. Watoto wao nao wanakosa matibabu. Ila wanasiasa hawa wanapata matibabu kwa pesa za maskini hawa ambazo wananyonywa.

Mnapewa misaada kupitia Watanzania kisha mnagawana pesa na kuwaacha Watanzania wafe.
Umechanganya mambo ila ultimately upo ukweli.Maskini ni mdanganyika.Yeye anatumika kwa kisingizio cha kumletea maendeleo,lakini si kweli.Yeye kiuhalisia anatumika kama chambo tu cha kuchukulia mikopo, kwa hiyo realistically anatumika kuiibia nchi rasilimali zake bila yeye kujua.

Viongozi uchwara wanaingia mikataba uchwara kwa ahadi za kupewa mikopo ambayo hata hivyo ikija inaishia mifukoni mwa viongozi hao hao uchwara,huku kiasi kikubwa kikichukuliwa kwa hila na mashirika hayo hayo au nchi zilizotoa mikopo.Kusema kweli ni uovu na udanganyifu ulio kithiri.No wonder miaka nenda miaka rudi nchi inachukua mikopo lakini hatua inayopiga kimaendeleo ni negligible.Tungepaswa kuwa mbali sana kimaendeleo but here we are,ahadi hewa kila kukicha,huku tuki rudi nyuma kimaendeleo.

Tumedanganywa kwamba maendeleo ni mabadiliko chanya ya vitu vinavyoweza kuturahisishia maisha yetu.Lakini he hii ni kweli? Jibu ni Hapana.Maendeleo ni mabadiliko chanya ya vitu vinavyoweza kuturahisishia maisha yetu na kuboresha afya zetu. So chochote ambacho kinarahisha kazi lakini hakiboreshi Afya zetu si maendeleo.
 
Yaani ugaidi wanaofanya wanafanya wanasiasa ni mkubwa ukilinganisha na huo unaoweza wewe wakujifunga mabomu na kuua watu wawili stand. Ndiyo hayo mwizi wa kuku tunapiga mawe, harafu hii mijizi inayokwamisha miradi tunaisifia☹️☹️☹️
Sina Tatizo na maudhui yako. Nina tatizo na Bandiko kuu Yani mada haijengi na inavutia Ugaidi na mashambulizi dhidi ya Mwafrika badala ya kuleta suluhishi. Ssa kwanini msiwakamate na mkwaoiga kama wezi wa Kuku basi. Nini kinachokuzuia? Manake hukuweka Suluhisho lolote like zaidi ya kutukana Jamii yako! How are you going to reconcile yourself, knowing you can could have used other solutions to build around the problem instead of, rather, using a Wrecking ball to tear down the fabric of your existence.

Waafrika tunajidharaulisha tukitegemea kwa kufanya hivyo ndiyo tunajijenga. Hatahivyo siamini wewe ni Mwafrika, haiiniingii akilini. Kama kweli unao huo ushahidi, mkamate, mtie kwenye tenga mburuze mahakamani....tabia hizi za wizi na rushwa unafanyika kwa Wazungu zaidi unavyofanyika Afrika au Tanzania. Ndugu hatuwezi kuwa tunajenga kwa kubomoana. Nakuhakikishia hata huko mnapotaka kufanya ulinganishi huo, hawawezi kutumia Lugha mnazotumia.
 
Ukiingilia shughuli ya mwanasiasa, usipokuwa ngangari utaondolewa katika uso wa dunia.
 
Unajiuliza waliwezaje kupokea pesa za Covid-19 na kudai wanazipeleka kwenye kujenga madarasa mengine wanaweka na tiles na ac?

Wanaacha watoto wadogo wanakufa kwa kukosa matibabu na bima inasitishwa kwa madai kuwa michango haitoshi. Lakini hawa wanasiasa wananunuliana magari ya kifahari sana kwa pesa za hawa maskini ambao wameachwa wafe kama panya.

Shetani kazi yake ni kuua na kuharibu. Siku zote. Na ndicho ambacho tuna ona kwa watu maskini. Wao wanaachwa wafe. Watoto wao nao wanakosa matibabu. Ila wanasiasa hawa wanapata matibabu kwa pesa za maskini hawa ambazo wananyonywa.

Mnapewa misaada kupitia Watanzania kisha mnagawana pesa na kuwaacha Watanzania wafe.
Umeandika vizuri mkuu. Umejenga hoja vema. Keep it up.
 
Back
Top Bottom