Wanasiasa wa Tanzania kama hamna Upendo na nia ya kweli dhidi ya Kuwakomboa Wakulima acheni Kuwapenda Kinafiki kwani inakera!!

Wanasiasa wa Tanzania kama hamna Upendo na nia ya kweli dhidi ya Kuwakomboa Wakulima acheni Kuwapenda Kinafiki kwani inakera!!

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Sasa ni mwaka wa 20 huu nawasikia tu Wanasiasa wa Tanzania kila mara wakisema wanawapigania Wakulima na wanawapenda lakini kila Siku nasikia mpaka Kushuhudia Vilio vya Wakulima kiasi cha mpaka kutia Huruma.

Tanzania ingekuwa na Viongozi imara tena wasio na Unafiki mwingi ndani yake nina uhakika Sekta ya Kilimo ingekuwa ndiyo Jibu tosha la tatizo la Ajira nchini Tanzania na ingewafanya pia Wakulima wa Tanzania wawe na Maisha mazuri tofauti na walivyo sasa lakini pia Sekta hii ingekuwa ni Chachu ya Kukuza Uchumi wa Taifa letu.

Wanasiasa wa Tanzania tafadhalini hebu tuacheni kuwatumia Wakulima kama Ngazi yetu ya Kujiimarisha Kisiasa, kutafuta Huruma ya Kiushawishi kutoka Kwao na kuwafanya kama vile ni Mazuzu / Wapumbavu wakati Kiuhalisia wao ndiyo wanatulisha na kutufanya tutambe na Matumbo yetu tukiwa huku Mijini huku wao Kutwa wakihangaika na Magugu, Miba na Nyoka huko Mashambani Vijijini.

Tuwaheshimu Wakulima wa Tanzania!!!!
 
Back
Top Bottom