Wanasiasa wa Upinzani wajitafakari: Je, wako upande wa Demokrasia au wanajali matumbo yao kwanza?

Wanasiasa wa Upinzani wajitafakari: Je, wako upande wa Demokrasia au wanajali matumbo yao kwanza?

Kalamu ya Mwananchi

Senior Member
Joined
Oct 27, 2020
Posts
100
Reaction score
552
Ili uchaguzi uaminike unahitaji vitu vikuu vitatu: uhuru, uwazi na haki.

Uchaguzi wa mwaka huu haukua na chochote kati ya hayo. Haukua uchaguzi wa kidemokrasia.

Moja ya njia ya kupinga dhuluma yoyote ile ni kugoma.

Mgomo wa kwanza uliotishwa nchi nzima na wanasiasa wa upinzani haukufanikiwa.

Lakini sasa hivi wanasiasa hao hao wamepata chance ya kugoma, sio tena kwa kuingia barabarani bali kwa kutokukubali kwenda bungeni kupitia viti maalumu.

Kwasababu, mtu hawezi akakudhulumu wazi wazi tena kwa nguvu na vipigo, halafu baadaye mkae meza moja na kujadili maswala mengine kama vile hakijatokea kitu. Huko ni kupelekeshwa.

Wasiache fursa hii ipite. Huu ndo wakati wao wakuonyesha msimamo.

Je, wako upande wa demokrasia au wanajali matumbo yao kwanza?
 
Back
Top Bottom