Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Tupo kwenye mwaka mmoja na nusu ambapo kamati za miradi na ujenzi za makanisa na misikiti zinapanga mipango mingi ya kukusanya fedha kwa wanasiasa
Ni kipindi ambacho taasisi za dini uacha kuangalia uchafu wa fedha na kupima vyanzo vya fedha husika. Ni kipindi cha wanasiasa kupokea mialiko mingi yakichangia harambee.
Je, vyama vya upinzani vimetenga bajeti ya kazi hii kama chama tawala? Wananchi wengi ni waumini wa dini na nyumba za ibada zinakwenda kutumika kama majukwaa ya kampeni. Je, upinzani mnakwenda kutumia mbinu gani kunusuru watanzania maskini wasimezwe kwenye siasa zinazoongozwa na viongozi wao wa dini?
Tumeanza kusikia watabiri na siku zote utabiri wao haujawahi kupingana na wishes za chama tawala......mtafanyaje kudhibiti rushwa ya imani kutumika kuomba kura?